Matokeo ya uchaguzi mkuu Chadema yametangazwa ambapo Freeman Mbowe amepata ushindi wa Tsunami. Mbowe ambaye amekiongoza chama hicho kwa miaka kumi na tano sasa alishangiliwa mno na wajumbe wakati matokeo yakitangazwa na msimamizi wa uchaguzi Sylivester Masinde.
Mbowe amepata ushindi wa asilimia 93.5 ya kura zote huku mpinzani wake Cecil Mwambe akiambulia kura 59.Tundu Antipass Lissu amezoa kura karibu zote kwa asilimia 98.8.
View attachment 1296858
Matokeo yote ya uchaguzi CHADEMA ni kama yanavyoonyesha chini.
MWENYEKITI WA TAIFA
1.Freeman Mbowe-886-93.5✔
2.Cecil David Mwambe- 59
3.HARIBIKA -3
MAKAMU MWENYEKITI BARA
1.Tundu Antipas Lissu-930-98.8%✔
2.Sophia H.Mwakagenda-11- 1..2%
HARIBIKA 9
MAKAMU MWENYEKITI ZANZIBARI
SAID ISSA MOHAMED
NDIYO 859-88.7%✔
HAPANA 95
HARIBIKA 1
Uchaguzi umefanyika kwa utulivu mkubwa huku wagombea wakipewa nafasi ya kujinadi kwa wajumbe bila hofu yoyote na kwa uhuru mkubwa.
Wajumbe kadhaa wa mkutano mkuu wakitoa maoni yao baada ya matokeo kutangazwa wamepongeza kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa kwa demokrasia na kusema hiyo ni heshima kubwa kwa chama chao ndani na nje ya nchi.
Baraza Kuu linatarajiwa kukutana leo kumchagua Katibu Mkuu wa chama hicho na manaibu wake wawili watakaopendekezwa na Mwenyekiti aliyechaguliwa Freeman Mbowe.
#NoHateNoFear