Freeman Mbowe, Said Issa na Tundu Lissu, washinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu CHADEMA

Freeman Mbowe, Said Issa na Tundu Lissu, washinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu CHADEMA

Matokeo ya uchaguzi mkuu Chadema yametangazwa ambapo Freeman Mbowe amepata ushindi wa Tsunami. Mbowe ambaye amekiongoza chama hicho kwa miaka kumi na tano sasa alishangiliwa mno na wajumbe wakati matokeo yakitangazwa na msimamizi wa uchaguzi Sylivester Masinde.

Mbowe amepata ushindi wa asilimia 93.5 ya kura zote huku mpinzani wake Cecil Mwambe akiambulia kura 59.Tundu Antipass Lissu amezoa kura karibu zote kwa asilimia 98.8.
View attachment 1296876
Matokeo yote ya uchaguzi CHADEMA ni kama yanavyoonyesha chini.

MWENYEKITI WA TAIFA
1.Freeman Mbowe-886-93.5✔
2.Cecil David Mwambe- 59
3.HARIBIKA -3

MAKAMU MWENYEKITI BARA
1.Tundu Antipas Lissu-930-98.8%✔

2.Sophia H.Mwakagenda-11- 1..2%
HARIBIKA 9

MAKAMU MWENYEKITI ZANZIBARI
SAID ISSA MOHAMED
NDIYO 859-88.7%✔
HAPANA 95
HARIBIKA 12

Zaidi, soma:

Mungu ndiye muweza wa yote.....peoples...power
 
Nipo sana, naanda bandiko la pongezi.
P
pongezi za nini wakati maombi yako kwa MH. MBOWE hayakuwa tofauti na ya chama chenu cha fisiem.. endeleeni kuloga.
Sasa tunasubiri tuone upande wenu kama mnaweza demokrasi ebu jaribuni kufanya yaliyofanywa na chama cha wenye AKILI nyingi.
tunataka MEKO apate mshindani sio mumpitishebila kupingwa wakati humo ndani yenu wapambananji wapo wengi mnawazuia DEMOCRACY hamuiwezi na hamtoiweza.

Freeman Mbowe Achaguliwa Tena Kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kwa Asilimia 93.5
on December 18, 2019 in News

Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amechaguliwa tena katika nafasi hiyo baada ya kupata kura 886 sawa na 93.5% dhidi ya mpinzani wake Cecil Mwambe aliyepata kura 59 sawa na 6.2%. Mbowe atatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

Matokeo hayo yametangazwa leo Alhamisi Desemba 19, 2019 saa 11 alfajiri na msimamizi wa uchaguzi, Sylvester Masinde, akibainisha kuwa kura tatu ziliharibika.

Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Baada ya Masinde kumtangaza Mbowe kuwa mshindi, idadi kubwa ya wajumbe wa mkutano mkuu walinyanyuka kwenye viti na kumfuata mbunge huyo wa Hai kwa ajili ya kumpongeza.


 
TARATIBU MKUU, muache pascal, bado anatafakari ataadika nini
Acha nidhamu ya woga mkuu, akili yake naijua kupitia threads zake, Pascall hana akili za kianalogy kama unavyodhani labda, sema tu kaamua kukaa kimya aka kuchunia na kumshtua ni muhimu maana napenda kujua mawazo yake pia kwenye hili.
 
Hii nayo ni Breaking News kweli? Watanzania walikuwa wanajua tu huyo Mwenyekiti wa Kudumu atapita. Wala hakuna cha ajabu mkuu!
Mbona ulikuwa unasema "Mwambe tuvushe" kama ulijua Mbowe kisha pita?
 
Hongera kwao...

Sasa kinachofuta hapa ni kuanza mchakato wa ku mu 'IMPEACH' msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Ila CCM haina adabu. Kuna tetesi kuwa mwana habari wa Azam TV anaitwa Jamal Hashimu eti siku ya kwanza tu alishawishiwa na CCM asirushe kinachoendelea kwenye ukumbi wa Mikutano wa mlimani City! Nasikia Ivona Kamtu jaribu kumshitua aruke hewani wapi! Jamal kagandwa na kada mmoja wa CCM. Hivi hizi habari ni za kweli? Uongozi wa Azam TV utuondolee hili wingu.
 
Patriot, Mbowe anawauma sana. Na figisu zote za kuhama hama vyama ila lengo lao la kumuondoa mbowe na kuweka pandikizi lao vimeshindikana. Sasa vinena vimeanza kuvimba kwa hasira. Mbowe ni jemedari kweli kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli Moshi yote inafahamu ujemedari wa Mbowe! Sasa sisi makabila mengine munatuomba kura na uanachama wa CHADEMA wa nini?

Hicho kinaitwa chama cha ushirika Kilimanjaro. Planning mbovu! Huwezi kupita M/kiti kutoka Kilimanjaro, halafu uteue katibu toka Kilimanjaro, MC wa mkutano Kilimanjaro, etc. Halafu eti uimarishe chama na kushinda uchaguzi. Hata kampeni zipitie mbinguni, huyo ni msanii na mwanasiasa-biashara tu!
 
Hivi mwaka huu wa 2019 unaweza kuwa na chama ambacho M/kiti ni form 4 a 6, katibu Form 6?
 
Yaani kwa kugombea tu dhidi ya Mbowe, mnamwita pandikizi! Iko wapi haki na demokrasia mnayoihubiri?

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana,, matamshi yake kabla ya kugombea yalileta hisia za kuwa huyu siyo mwenzetu! jana hata wakati wa kuhesabu kura na kutangaza matokeo alishaondoka zamani ukumbini! huyo kweli ni wa CDM damuni?
 
kwa hiyo wewe shida yako ni kubadilisha mtu?? we kweli mbumbumbu.
Ndiyo maana ya democracy, chama siyo duka kumilikiwa na mtu mmoja.

Fanya kwa mda uwaachie na watu wengine waje na mawazo mbadala chama kisonge mbele. Mawazo yale yale, techniques zile zile zisizoshinda hata mara moja miaka nenda rudi maana yake jitihada za m/kiti hazitoshi lakini yeye ataki kuliona hilo amegangania tu, hizo siyo siasa bali ni masirahi ndiyo motive ya yeye kukomalia pale mpaka either afe, au chama chenyewe kife mikononi mwake.

Inawezekana kweli mimi mbumbumbu ila wewe waweza kuta ndio mbumbumbu zaidi yangu.
 
CCM watabisha hata hili, maana wao kuchaguana hawajui wamezoea KUTEULIWA.


By the way, CHADEMA huwa wanapiga kelele sana kuwa nchi haina democrasia,
hivi can you compare CHADEMA with CCM on democracy? There is no democracy in CHADEMA! Chama kinaongozwa na mwenyekiti yule yule miaka nenda miaka rudi, wengine wakijaribu wanawekewa zengwe! Chama gani hicho!
 
Ndiyo maana ya democracy, chama siyo duka kumilikiwa na mtu mmoja.

Fanya kwa mda uwaachie na watu wengine waje na mawazo mbadala chama kisonge mbele. Mawazo yale yale, techniques zile zile zisizoshinda hata mara moja miaka nenda rudi maana yake jitihada za m/kiti hazitoshi lakini yeye ataki kuliona hilo amegangania tu, hizo siyo siasa bali ni masirahi ndiyo motive ya yeye kukomalia pale mpaka either afe, au chama chenyewe kife mikononi mwake.

Inawezekana kweli mimi mbumbumbu ila wewe waweza kuta ndio mbumbumbu zaidi yangu.


Tatizo ni kuwa CHADEMA ni mali ya watu fulani, sio umma. Hivi unafikiri akiondoka Mbowe kitabaki nini? Utakuwa ndiwo mwisho wa chama. CDM ni kama Pertinership business au unlimited company!
 
By the way, CHADEMA huwa wanapiga kelele sana kuwa nchi haina democrasia,
hivi can you compare CHADEMA with CCM on democracy? There is no democracy in CHADEMA! Chama kinaongozwa na mwenyekiti yule yule miaka nenda miaka rudi, wengine wakijaribu wanawekewa zengwe! Chama gani hicho!
Hahaha demokrasia gani ccm ya kuteua na kuteuliwa badala ya kuchagua?!
Hata mwenyekiti ccm hachaguliwi, maana anaye teuliwa kuwa rais ndiye anakuwa mwenyekiti by default.
Umewahi kusikia kuna uchaguzi wa mwenyekiti ccm?!
Mwenyekiti wa CHADEMA anagombea kila baada ya miaka 5, anachaguliwa yeye hiyo ni demokrasia ukilinganisha na hii ya kuteua ya ccm.
 
Tatizo ni kuwa CHADEMA ni mali ya watu fulani, sio umma. Hivi unafikiri akiondoka Mbowe kitabaki nini? Utakuwa ndiwo mwisho wa chama. CDM ni kama Pertinership business au unlimited company!
Labda kama ni hivi unavyosema hapo nitaelewa kwa nini ni yeye muda wote. Vinginevyo sioni sababu ya yeye kuwa mwenyekiti wa kudumu.
 
Kama Mbowe tu ndiyo mwenye uwezo wa kuiongoza chadema?

Kwanini Magufuli Pombe asibadili katiba na kuendelea kugombea na kuongoza kwa vipindi vingine zaidi
Huwenda pia yeye ndiyo anafaa tu kuwa rais nchi hii

Chadema wana maoni gani juu ya katiba kubadilishwa na Magu kuendelea kugombea urais?

Kwa kweli naanza kuidharau chadema baada ya Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom