X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,605
- 1,843
Matempla na Misri ya zamani
Wanachoelewa wanahistoria wengi kuhusiana na Frimansori ni kuwa chimbuko la Jumuiya hii ni vita vya msalaba. Ukweli ni kuwa ijapokuwa Mansori , kimsingi iliasisiwa na kutambuliwa rasmi nchini Uingereza mwanzoni mwa karne ya kumi na nne, mizizi ya Jumuiya hii imeanzia katika vita vya msalaba mnamo karne ya kumi na mbili. Katika mkasa huu mashuhuri ndimo linamokutwa kundi la wanamgambo wa vita hivyo vya msalaba waliojulikana kama Knights Templar au Templars. Katika mfululizo wetu tumekuwa tukitumia tafsiri isiyo rasmi ya majina hayo ambayo ni Matempla. Kwa mapana na marefu historia ya Matempla imeelezewa katika kitabu kiitwacho The New Masonic Order. Hivyo basi katika mfululizo huu tumeielezea kwa mukhtasari tu. Kwani kuichambua kwetu mizizi ya Mansori na athari zake katika Duniya kwatosha kabisa kufichua maana nzima ya Frimansori. Ijapokuwa baadhi ya watu wanashikilia kuwa vita vya msalaba vilikuwa ni vita vilivyofanywa kwaajili ya Imani ya Kikristo, lakini kimsingi vita hivyo vilifanywa kwa maslahi ya kiuchumi. Katika kile kipindi ambacho Ulaya ilikuwa katika hali ya umasikini na ufukara, Waislamu wa mashariki ya kati walikuwa katika hali bora ya kiuchumi. Mafanikio hayo ya kiuchumi pamoja na utajiri wa Mashariki ya kati uliwatamanisha sana wazungu wa Ulaya.
Uchu wa utajiri waliokuwanao Wazungu hao wa Ulaya ukavikwa sura ya kidini na kupambwa kwa sifa za Ukristo, japo kwa kweli wazo hasa la kuanzisha vita hivyo lilitokana na tamaa ya maslahi ya kiDuniya. Ndio sababu kukawa na mabadiliko ya ghafla katika sera za Wakristo wa Ulaya. Wakaachana na zile sera za amani na utulivu walizokuwa nazo katika nyakati za mwanzo za historia yao na badala yake wakachukuwa mwelekeo wa vita vya kijeshi. Mwanzilishi wa vita vya Msalaba alikuwa Papa Urban wa Pili au Pope Urban II. Papa huyu aliitisha mkutano wa baraza lake, Council of Clermont mnamo mwaka 1095. Katika mkutano huo ile itikadi ya awali ya utulivu waliyokuwanayo Wakristo ikatupiliwa mbali. Vikatangazwa vita vitakatifu kwa shabaha ya kuzipora nchi takatifu kutoka mikononi mwa Waislamu. Kufuatia tangazo hili la vita, Jeshi kubwa la wanamgambo walioitwa Crusaders likaundwa. Kwa kiswahili tutatumia neno makruseda hapa na pale katika kutafsiri neno hilo Crusaders. Jeshi hilo lilijumuisha askari waliokuwa na mafunzo ya kijeshi pamoja na makumi kwa maelfu ya watu wa kawaida. Wanahistoria wanaamini kuwa hila ya Papa Urban wa pili kuanzisha vita hivyo ilitokana na tamaa yake ya kushinda kinyanganyiro cha Upapa.
Isitoshe Wafalme, wana wa wafalme, watawala na watu wengine wa Ulaya waliupokea wito wa Papa kwa furaha kwani walikuwa na malengo ya kujipatia maslahi ya kiDuniya kama alivyosema bw. Donald Queller wa Chuo kikuu cha Illinois, kwamba mashujaa wa Ufaransa walitaka tu kujiongezea nchi. Nao wafanyabiashara wa Italia walitumai kupanua biashara yao mashariki ya kati .. Idadi kubwa ya makapuku au walala hoi walijiunga na misafara hii ya kijeshi ili kukimbia maisha magumu waliokuwa wakiishi makwao. Kote lilikopita, Jeshi hili la wachumia tumbo lilichinja Waislamu na hata mayahudi kwa tamaa ya kujipatia dhahabu na vito vya thamani. Makruseda hawa walitumbua matumbo ya watu waliowaua ili eti watowe dhahabu na madini ya thamani ambayo wahanga huenda waliyameza kabla ya kufa. Tamaa ya mali iliwazidia mno Makruseda kiasi ambacho hawakusita kuvamia na kuteka jiji la Wakristo la Constantinople (Istanbul) katika vita ya nne ya Msalaba. Baada ya safari ngumu na ndefu na baada ya kufanya unyanganyi na uporaji sambamba na mauaji ya Waislamu, kundi hili la wauaji waloitwa Makruseda likafika Jelusalem mnamo mwaka 1099. Makruseda hawa waliingia katika jiji hili baada ya kulizingira kwa takriban majuma matano. Walifanya ushenzi wa kupindukia. Waislamu na Mayahudi wote wa jiji hilo walifyekwa mapanga. Kwa maneno ya mwana historia mmoja, Makruseda waliua Warabu, Waislamu na Waturuki wote waliowakuta humo Wanaume kwa Wanawake. Mmoja wa Makruseda hao, bwana Raymond alijitapa hivi kwa hujuma waliyoifanya:
Baadhi ya watu wetu walifyeka vichwa vya maadui zao, wengine wakawachoma mishale, wengine waliwatesa sana kwa kuwatupa maadui kwenye moto. Malundo ya vichwa, mikono na miguu yalionekana katika mitaa ya jiji. Ilibidi mtu akanyage miili ya watu na farasi ili aweze kupita njia. Lakini yote haya ni madogo kulinganisha na yale yaliyotokea kwenye hekalu la Suleiman mahala ambapo ibada za kidini hufanyika mara kwa mara Kuanzia ndani ya hekalu hadi kwenye baraza ya hekalu hilo, watu walipita kwenye madimbwi ya damu ambapo damu ilizamisha miguu yao hadi magotini. Kwa muda wa siku mbili tu jeshi la makruseda liliwaua kinyama Waislamu wapatao 40,000. Baada ya hapo Makruseda wakaifanya Jelusalem kuwa mji wao mkuu na wakaanzisha utawala wa kifalme wa kilatini uliojitandaza kutoka mipaka ya Palestina hadi Antiokia. Baadaye tena makruseda wakaanzisha mapambano ya kuimarisha mamlaka yao mashariki ya kati. Ili kuidumisha dola waliyoianzisha, ilibidi waiunganishe. Katika kutimiza lengo hilo wakaanzisha Komandi za Kijeshi ambazo hazikuwa na mfano wake hapo kabla. Watu waliounda komandi hizi walitokea Ulaya kwenda Palestina na wakaishi katika majengo mithili ya yale ya Watawa ambamo walipatiwa mafunzo ya kijeshi ili kupambana na Waislamu. Mojawapo ya Komandi hizi ilikuwa tofauti kabisa na nyinginezo. Yenyewe ilibadilika muundo na kubadili mwelekeo wa historia. Komandi hii ilikuwa ya Matempla.