Freemasons Inside - Out: Who are they? How they operate? How to join them?

Freemasons Inside - Out: Who are they? How they operate? How to join them?

Status
Not open for further replies.
Matempla na Misri ya zamani

Wanachoelewa wanahistoria wengi kuhusiana na Frimansori ni kuwa chimbuko la Jumuiya hii ni vita vya msalaba. Ukweli ni kuwa ijapokuwa Mansori , kimsingi iliasisiwa na kutambuliwa rasmi nchini Uingereza mwanzoni mwa karne ya kumi na nne, mizizi ya Jumuiya hii imeanzia katika vita vya msalaba mnamo karne ya kumi na mbili. Katika mkasa huu mashuhuri ndimo linamokutwa kundi la wanamgambo wa vita hivyo vya msalaba waliojulikana kama Knights Templar au Templars. Katika mfululizo wetu tumekuwa tukitumia tafsiri isiyo rasmi ya majina hayo ambayo ni Matempla. Kwa mapana na marefu historia ya Matempla imeelezewa katika kitabu kiitwacho The New Masonic Order. Hivyo basi katika mfululizo huu tumeielezea kwa mukhtasari tu. Kwani kuichambua kwetu mizizi ya Mansori na athari zake katika Duniya kwatosha kabisa kufichua maana nzima ya Frimansori. Ijapokuwa baadhi ya watu wanashikilia kuwa vita vya msalaba vilikuwa ni vita vilivyofanywa kwaajili ya Imani ya Kikristo, lakini kimsingi vita hivyo vilifanywa kwa maslahi ya kiuchumi. Katika kile kipindi ambacho Ulaya ilikuwa katika hali ya umasikini na ufukara, Waislamu wa mashariki ya kati walikuwa katika hali bora ya kiuchumi. Mafanikio hayo ya kiuchumi pamoja na utajiri wa Mashariki ya kati uliwatamanisha sana wazungu wa Ulaya.

Uchu wa utajiri waliokuwanao Wazungu hao wa Ulaya ukavikwa sura ya kidini na kupambwa kwa sifa za Ukristo, japo kwa kweli wazo hasa la kuanzisha vita hivyo lilitokana na tamaa ya maslahi ya kiDuniya. Ndio sababu kukawa na mabadiliko ya ghafla katika sera za Wakristo wa Ulaya. Wakaachana na zile sera za amani na utulivu walizokuwa nazo katika nyakati za mwanzo za historia yao na badala yake wakachukuwa mwelekeo wa vita vya kijeshi. Mwanzilishi wa vita vya Msalaba alikuwa Papa Urban wa Pili au Pope Urban II. Papa huyu aliitisha mkutano wa baraza lake, Council of Clermont mnamo mwaka 1095. Katika mkutano huo ile itikadi ya awali ya utulivu waliyokuwanayo Wakristo ikatupiliwa mbali. Vikatangazwa vita vitakatifu kwa shabaha ya kuzipora nchi takatifu kutoka mikononi mwa Waislamu. Kufuatia tangazo hili la vita, Jeshi kubwa la wanamgambo walioitwa Crusaders likaundwa. Kwa kiswahili tutatumia neno makruseda hapa na pale katika kutafsiri neno hilo Crusaders. Jeshi hilo lilijumuisha askari waliokuwa na mafunzo ya kijeshi pamoja na makumi kwa maelfu ya watu wa kawaida. Wanahistoria wanaamini kuwa hila ya Papa Urban wa pili kuanzisha vita hivyo ilitokana na tamaa yake ya kushinda kinyang’anyiro cha Upapa.

Isitoshe Wafalme, wana wa wafalme, watawala na watu wengine wa Ulaya waliupokea wito wa Papa kwa furaha kwani walikuwa na malengo ya kujipatia maslahi ya kiDuniya kama alivyosema bw. Donald Queller wa Chuo kikuu cha Illinois, kwamba mashujaa wa Ufaransa walitaka tu kujiongezea nchi. Nao wafanyabiashara wa Italia walitumai kupanua biashara yao mashariki ya kati…….. Idadi kubwa ya makapuku au walala hoi walijiunga na misafara hii ya kijeshi ili kukimbia maisha magumu waliokuwa wakiishi makwao. Kote lilikopita, Jeshi hili la wachumia tumbo lilichinja Waislamu na hata mayahudi kwa tamaa ya kujipatia dhahabu na vito vya thamani. Makruseda hawa walitumbua matumbo ya watu waliowaua ili eti watowe dhahabu na madini ya thamani ambayo wahanga huenda waliyameza kabla ya kufa. Tamaa ya mali iliwazidia mno Makruseda kiasi ambacho hawakusita kuvamia na kuteka jiji la Wakristo la Constantinople (Istanbul) katika vita ya nne ya Msalaba. Baada ya safari ngumu na ndefu na baada ya kufanya unyang’anyi na uporaji sambamba na mauaji ya Waislamu, kundi hili la wauaji waloitwa Makruseda likafika Jelusalem mnamo mwaka 1099. Makruseda hawa waliingia katika jiji hili baada ya kulizingira kwa takriban majuma matano. Walifanya ushenzi wa kupindukia. Waislamu na Mayahudi wote wa jiji hilo walifyekwa mapanga. Kwa maneno ya mwana historia mmoja, Makruseda waliua Warabu, Waislamu na Waturuki wote waliowakuta humo…Wanaume kwa Wanawake. Mmoja wa Makruseda hao, bwana Raymond alijitapa hivi kwa hujuma waliyoifanya:

Baadhi ya watu wetu walifyeka vichwa vya maadui zao, wengine wakawachoma mishale, wengine waliwatesa sana kwa kuwatupa maadui kwenye moto. Malundo ya vichwa, mikono na miguu yalionekana katika mitaa ya jiji. Ilibidi mtu akanyage miili ya watu na farasi ili aweze kupita njia. Lakini yote haya ni madogo kulinganisha na yale yaliyotokea kwenye hekalu la Suleiman mahala ambapo ibada za kidini hufanyika mara kwa mara…Kuanzia ndani ya hekalu hadi kwenye baraza ya hekalu hilo, watu walipita kwenye madimbwi ya damu ambapo damu ilizamisha miguu yao hadi magotini. Kwa muda wa siku mbili tu jeshi la makruseda liliwaua kinyama Waislamu wapatao 40,000. Baada ya hapo Makruseda wakaifanya Jelusalem kuwa mji wao mkuu na wakaanzisha utawala wa kifalme wa kilatini uliojitandaza kutoka mipaka ya Palestina hadi Antiokia. Baadaye tena makruseda wakaanzisha mapambano ya kuimarisha mamlaka yao mashariki ya kati. Ili kuidumisha dola waliyoianzisha, ilibidi waiunganishe. Katika kutimiza lengo hilo wakaanzisha Komandi za Kijeshi ambazo hazikuwa na mfano wake hapo kabla. Watu waliounda komandi hizi walitokea Ulaya kwenda Palestina na wakaishi katika majengo mithili ya yale ya Watawa ambamo walipatiwa mafunzo ya kijeshi ili kupambana na Waislamu. Mojawapo ya Komandi hizi ilikuwa tofauti kabisa na nyinginezo. Yenyewe ilibadilika muundo na kubadili mwelekeo wa historia. Komandi hii ilikuwa ya Matempla.
 
Matempla

Watu waliounda Komandi hizo walitoka Ulaya kuja Palestina na wakaishi katika nyumba za kitawa ambamo walipewa mafunzo ya kijeshi ili kupambana na Waislamu. Kundi moja miongoni mwa vikundi hivi lilitofautiana na makundi mengine. Lenyewe likabadilika muundo na kubadili mwelekeo wa historia. Kundi hili lilikuwa la Matempla. Matempla au kwa jina kamili askari dhaifu wa Yesu Kristo na hekalu la Selemani ni kundi lililoanzishwa mwaka 1118 yaani miaka 20 baada ya Makruseda kuitwaa Jelusalem. Waanzilishi wa kundi hili walikuwa Askari wa Ufaransa, Hugh dee Payens na mwenziye Godfrey d St. Omer. Mwanzoni kabisa kundi hili lilikuwa na watu tisa lakini baadaye likazidi kukuwa. Sababu iliyowapelekea kujiita jina hilo (Matempla) ambalo linatokana na Nomino Temple ni kuwa sehemu waliyochaguwa kuwa ngome yao ni mahali ambapo lipo hekalu la Selemani (Temple of Solomon) au pia panaitwa Temple Mount (kilima cha hekaluni). Japo Matempla walijiita “askari dhaifu” lakini kwa kipindi kifupi tu wakawa matajiri wakubwa. Mahujaji wa Kikristo waliotoka Ulaya kuja Palestina wote walikuwa chin i ya himaya ya kundi hili na kutokana na fedha zao wakatajirika sana. Mbali na hivyo, kwa mara ya kwanza kabisa matempla wakaanzisha mfumo wa hundi na karadha, sawa na ule wa Benki. Kwa mujibu wa waandishi wa kingereza, Michael Baigent na Richard Leigh, matempla ndio walioanzisha mfumo wa kibepari wa zama za kati na ndio waliotoa mwelekeo wa kuanzishwa mfumo wa sasa wa Benki unaojengeka kwa misingi ya riba. Walikuwa ni hawa Matempla waliohusika kwa kiasi kikubwa na mashambulizi ya makruseda na mauaji ya Wailsmu. Kwas sababu hii Kamanda mkuu wa Waislamu Saladin aliyelishinda Jeshi la Makruseda katika vita vya Hattin 1887, na baadaye kuikomboa Jelusalem, aliwahukumu Matemplsa adhabu ya kifo kwa mauaji waliyoyafanya, na akawasamehe Wakristo wengi sana. Ingawaje waliipoteza Jelusalem na kupata madhara makubwa, bado matempla waliendelea kuwepo. Na licha ya kupungua kwa idadi ya Wakristo nchini Palestina, Matempla waliimarisha mamlaka yao barani Ulaya kuanzia Ufaransa hadi nchi nyingine hivyo pakawa na dola ndani ya dola. Hapana shaka kuwa nguvu zao za kisiasa ziliwaweka roho juu wafalme wa Ulaya. Aidha kulikuwa na jambo jingine ambalo liliweka Taasisi ya Ukasisi katika hali mbaya. Kundi hili la matempla lilianza kidogo kidogo kujitoa katika Imani ya Kikristo. Na wakati walipokuwa bado wapo Jelusalem, walianza kufuata itikadi za ajabu za kikuhani. Pia kulikuwa na uvumi kuwa walikuwa wanafuata utaratibu wa ajabu wa sala unaorandana na Itikadi hizo. Hatimaye, mnamo mwaka 1307, Mfalme wa Ufaransa Filip le Bel aliamua kuwakamata wafuasi wa kundi hili. Baadhi yao wakafau lu kutoroka lakini wengi wao walitiwa mbaroni. Papa Clement wa tano, naye akaunga mkono hatua hiyo. Kufuatia kipindi kirefu cha mahojiano na mashtaka, matempla wengi walikiri kufuata imani mpya kwamba waliikana Imani ya Kikristo na kumtukana Yesu katika mikutano yao.

Mwishowe viongozi wa Matempla ambao waliitwa “Mabwana wakubwa” kuanzia yule kiongozi wao mkubwa kabisa bwana Jacques de Molay wote walinyongwa kwa amri ya Mfalme na Kanisa mwaka 1314. Wengi miongoni mwao walifungwa Jela na kundi likasambaratika na kutokomea. Baadhi ya Wanahistoria wanakasumba ya kuielezea kesi ya Matempla kama ni njama ya Mfalme wa Ufaransa na kuwatoa hatiani Matempla. Lakini tafsiri hii ya mambo ina upungufu katika vipengere kadha wa kadha. Mwanahistoria mashuhuri wa Uingereza Nesta H Webster ambaye ana ufahamu mkubwa wa historia ya mambo ya siri anavichambua vipengele hivi katika kitabu chake, Secret Societies and Subversive Movements.

Kwa mujibu wa mwanahistoriya huyu ile kasumba ya kuwaondoa hatiani Matempla kwa mambo ambayo wenyewe walikiri kuyafanya katika kile kipindi cha mashtaka haina mashiko. Mosi wakati wa mahojiano, si matempla wote walioteswa licha ya kukabiliwa na shitka moja. Vyovyote iwavyo kesi ya Matempla ilikwisha sambamba na kukomeshwa kwa kundi lao. Lakini, ijapokuwa kundi hili lilikoma rasmi hata hivyo halikutoweka kabisa. Katika ile kamata kamata ya kushitukiza mwaka 1307, baadhi yao walinusurika. Kwa mujibu wa tasnifu zilizoegamia nyaraka mbali mbali za kihistoria, idadi ndogo ya matempla ilipata hifadhi katika utawala pekee wa kifalme barani Ulaya ambao haukutambua mamlaka ya Kanisa Katoliki katika karne ya 14, huo ni utawala wa Scotland. Huko walijikusanya upya chini ya hifadhi ya mfalme wa nchi hiyo, Robert The Bruce. Baada ya muda fulani wakabuni mbinu muafaka ya kujificha ili waendelee kuwepo kwa siri. Wakajipenyeza katika jumuiya moja kubwa kwenye visiwa vya Uingereza- Wall builders’lodge na baadaye wakapata mamlaka kamili ya kudhibiti Maskani za Jumuiya hiyo. Mwanzoni mwa zama hizi, jumuiya hii ikabadili jina lake, sasa ilijiita “Masonic Lodge.” Kaida ya Scotland ndio tawi kongwe kabisa la Masonri ambalo limeanza tokea karne ya 14 kwa wale Matempla waliopata hifadhi nchini Scoland. Kwa kifupi matempla hawakutoweka moja kwa moja falsafa yao, Imani zao na Ibada zao bado zingalipo chini ya mwamvuli wa Friimansuri. Dhana hii inathibitishwa na ushahidi mwingi wa kihistoria na inakubaliwa na wanahistoria wengi wa Magharibi wale wa Friimansuri na wasio Friimansori. Katika kitabu, The New Masonic Order ushahidi huu umeelezwa kwa kina.

Jarida liitwalo Mimar sinan linaelezea uhusiano kati ya lile kundi la Mtempla na Frimansori kwa maneno yafuatayo:

Mnamo mwaka 1312 pale Mfalme wa Ufaransa alipolikomesha kundi la matempla kwa shinikizo la kanisa, harakati za matempla hazikukomeya hapo. Matempla wengi sana walijificha katika maskani za Frimansori za Ulaya. Kiongozi wa Matempla, Mabeignac pamoja na wafuasi wengine wachache walipata hifadhi nchini Scottland wakijificha chini ya jumuiya ya Wall builder kwa kutumia jina la Macbenach.

Mfalme wa Scotland Robert the Bruce akawakaribisha na kuwaruhusu kujijengea nguvu kubwa katika maskani za Masoni nchini humo. Matokeo yake maskani hizo zikajipatia umuhimu mkubwa kutokana na kazi zao za ufundi na mawazo yao. Hivi leo Frimansori wanalitumia kwa heshima jina la Macbenach. Masoni wa Scotland waliorithi mila ya matempla wakaenda nayo ufaransa miaka mingi baadaye na huko wakajenga msingi wa Kaida (rite) ijulikanayo kama Kaida ya Scotland (Scottish Rite). Aidha Jarida hilo limetoa maelezo mengi kuhusiana na uhusiano baina ya Matempla na Frimansori. Katika makala yenye kichwa “Templars and Freenasonry” inaelezwa kuwa sala za sherehe za uzinduzi wa ile Komandi ya Matempla ni sawa kabisa na zile za Frimansori hivi leo. Kwa mujibu wa makala hiyo hiyo, kama ilivyo kwa Mansori, wafuasi wa kundi la Matempla nao pia walikuwa wakiitana kwa jina la Brother (ndugu).


Katika sehemu ya mwisho ya makala hiyo tunasoma haya yafuatayo:


Kundi la Matempla na jumuiya ya Masoni ni pande mbili ambazo zimeathiriana kwa kiasi kikubwa. Hata sala za washirika hawa zinalingana zikiwa zimeigwa kutoka kwa matempla. Kwa ajili hii Masoni, kwa kiasi kikubwa wanafanana na matempla na hivyo yaweza kusemwa kuwa ile inayoonwa kama itikadi ya siri ya masoni imerithiwa kutoka kwa Matempla. Hivyo inadhihirika wazi kuwa mizizi ya frimansori inaanzia kwa Matempla na kwamba Masoni wamefuata falsafa ya matempla. Masoni wenyewe wanakubaliana na jambo hili. Lakini hapa, jambo muhimu kwetu ni chanzo cha falsafa hii. Kuna maswali haya; kwa nini matempla waliachana na Ukristo na kuwa kundi lenye itikadi mpya? Nini kilichowapelekea kufanya hivyo? Kwanini walibadilika kule Jelusalem? Kupitia shirika la Masonri kumekuwa na athari gani ulimwenguni kutokana na falsafa hii iliyofuatwa na Matempla?
 
Matempla na Kabbalah

Kitabu kiitwacho The Hiram Key kilichoandikwa na Masoni wawili Christopher Knight na Robert Lomas kinafichuwa mambo muhimu kuhusu mizizi ya frimansori. Kwa mujibu wa waandishi hawa, ni dhahiri kuwa Mansonri ni muendelezo wa Matempla. Mbali na hivyo waandishi hawa pia wamevitafiti vyanzo vya Matempla. Kwa mujibu wa tasnifu yao, Matempla walibadilika kwa kiasi kikubwa wakati walipokuwa Jerusalem. Badala ya Ukristo, Matempla walifuata itikadi nyingine. Katika mabadiliko haya kuna siri kubwa ambayo Matempla waliigundua katika hekalu la Selemani kule Jerusalem.

Waandishi hawa wamefafanua kuwa Matempla walitumia kisingizio cha kuwalinda mahujaji wa Kikristo waliokuwa wakitembelea Palestina kwa minajili ya kufikia malengo mengine kabisa:

Hakuna ushahidi wowote kuwa Matempla hawa waliwahi kutoa ulinzi wowote kwa mahujaji hao bali badala yake tunaona kuwa kuna ushahidi kamili kuwa walikuwa wakifanya kazi kubwa ya kuchimba Magofu ya hekalu…

Si waandishi hawa pekee waliogundua jambo hili. Mwana historia wa Kifaransa Gaetan Delaforge naye anazungumzia jambo hilo hilo:

Kazi kubwa ya wale Matempla tisa ilikuwa ni kufanya utafiti katika eneo lote ili kupata masalio na maandiko yenye maudhui juu ya tamaduni za siri za dini ya Uyahudi na Misri ya zamani.

Mwishoni mwa karne ya 19 Charles Wilson alianza kufanya utafiti wa mambo ya kale mjini Jerusalem, akatoa maoni yake kuwa Matempla walikwenda Jerusalem kwa lengo la kutafiti mabaki ya hekalu. Wilson aliona alama ya chimba chimba na fukuwa fukuwa chini ya misingi ya hekalu na akasema kuwa haya yalifanywa kwa zana za Matempla. Zana hizi hadi leo zipo katika hifadhi ya Robert Brydon ambaye anamiliki nyaraka nyingi zenye maelezo kuhusu matempla.

Waandishi wa kitabu cha Hiram key wao wanadai kuwa chimba chimba hii ya Matempla haikutoka kapa (haikuishia patupu), kwamba Matempla waligundua mambo fulani ambayo yalibadili mtazamo wao juu ya ulimwengu. Aidha watafiti wengi wanakubaliana na jambo hilo. Lazima kuna jambo fulani tu ambalo liliwapelekea Matempla kufuata utaratibu wa imani na falsafa iliyotofautiana kabisa na ile ya Ukristo licha ya ukweli kuwa kabla ya hapo walikuwa Wakristo na isitoshe walitoka katika ulimwengu wa Kikristo. Kwa fikra za watafiti wengi jambo walilogundua Matempla ambalo lilibadili mtazamo wao ni Kabbalah. Maana ya neno hili Kabbalah ni Oral Tradition (Fasihi simulizi). Kamusi mbali mbali zinaliainisha neno hili kama ni tawi la siri na la kikuhani la dini ya uyahudi. Kwa mujibu wa ainisho hili Kabbalah inafichua maana iliyofichikana ya Taurati na maandiko ya dini ya Uyahudi. Lakini tunapolichungua jambo hili kwa undani tunaona kuwa kuna mambo mengine kabisa. Mambo haya ndiyo yanayotupelekea kufikia hitimisho kuwa Kabbalah ni utaratibu ambao mzizi wake unatokea katika ibada ya masanamu ya wapagani. Hii ni kuwa Kabbalah ilikuwepo kabla ya Taurati na ilitumbukizwa katika dini ya Uyahudi baada ya kufunuliwa Taurati. Ukweli huu wa kusisimua juu ya Kabbalah unafafanuliwa hivi: Frimasoni wa Kituruki Murat Ozgen katika kitabu chake, Masonluk Nedir ve Nasildir? (Ni nini frimansori na ikoje?), anasema:

“Hatujuwi vyema wapi ilikotokea Kabbalah na jinsi ilivyostawi. Hili ni jina la jumla la falsafa ya ajabu, ya siri na ya kikuhani hususani ile inayohusiana na dini ya Uyahudi. Inasadikika kuwa ni Itikadi ya kikuhani ya kiyahudi lakini baadhi ya mambo yaliyomo katika itikadi hiyo yanaonesha kuwa ni Itikadi iliyojengwa zamani kabla ya Taurati”.

Mwana historia wa Kifaransa anayeitwa Gougenot des Mousseaux ameeleza kuwa Kabbalah ni kongwe mno kuliko itikadi ya uyahudi. Naye Mwanahistoria wa Kiyahudi Theodore Reinach anasema kuwa Kabbalah ni sumu isiyofahamika ambayo iliingia kwenye mishipa ya Uyahudi na kuidhuru itikadi nzima. Salomon Reinach anaiainisha Kabbbalah kama ni mojawapo kati ya pogo mbaya sana za akili ya binadamu. Sababu ya dai hili la Reinach ni kuwa itikadi ya Kabbalah kwa kiasi kikubwa inahusiana na uchawi. Kwa maelfu ya miaka, Kabbalah imekuwa msingi wa kila itikadi ya kichawi. Inasadikiwa kuwa “magwiji” wa Kiyahudi wenye elimu ya Kabbalah wana nguvu kubwa za kimazingara. Halikadhalika watu wengi wasiokuwa Mayahudi wameathiriwa na Kabbalah na wamekuwa wakijaribu kufanya uchawi kwa kutumia mafundisho yake. Zile tamaduni za siri ambazo zilikuwa na nguvu Ulaya mwishoni mwa zama za kati, kwa kiasi kikubwa mizizi yake ilitokea katika Kabbalah.

Waandishi kadhaa waliothibitisha kuwa Matempla walibadili muelekeo baada ya kugundua siri fulani kwenye mabaki ya Hekalu la Selemani. Siri hiyo ni Kabbala. Kabbala ni utaratibu unaotokea katika ibada ya masanamu ya wapagani. Kwamba, itikadi hii ilikuwepo zamani kabla ya kufunuliwa kwa Taurati. Jambo la ajabu ni kuwa Uyahudi ni dini iliyoamini Mungu mmoja iliyotokana na ufunuo wa Taurati kwa Mussa (a.s). Lakini ndani ya dini hii umo utaratibu unaoitwa Kabbalah unaofuata mafundisho ya uchawi yaliyoharamishwa na dini hiyo. Jambo hili linathibitisha yale tuliyoyaeleza awali kuwa Kabbalah ni kitu ambacho kimeingia katika Uyahudi kutoka sehemu nyingine. Lakini nini chimbuko la kitu hiki? Mwanahistoria wa Kiyahudi Fabre d’Olivet anasema kuwa kabbalah ilitoka katika nchi ya Misri ya zamani. Kwa mujibu wa mwandishi huyu mizizi ya kabbalah imetambaa kutoka Misri ya kale. Kabbalah ni utamaduni ambao baadhi ya viongozi wa Waisrael walijifunza katika nchi ya Misri. Na wao wakaurithisha utamaduni huo kwa kizazi hadi kizazi kwa njia ya fasihi simulizi. Kwa sababu hii hatuna budi kuiangalia hiyo Misri ya kale ili tuvione vyanzo vya msingi vya mfungamano wa Kabbalah, Matempla na Frimansori.
 
mkuu maelezo haya mazuri ial rekebisha font size! Inaumiza macho pili haivutii kusoma! Font hii ni ndogo mno!

na ni ndefu mno bana....haiwezi kufupishwa
 
mkuu maelezo haya mazuri ial rekebisha font size! Inaumiza macho pili haivutii kusoma! Font hii ni ndogo mno!
Mkuu pole sana, ukitaka kuongeza font size just click Ctrl pamoja na alama ya (+) na ukitaka kupunguza font size unabonyeza Ctrl pamoja na alama ya (-).
 
Wachawi wa Misri ya kale

Misri ya kale ya Mafirauni ilikuwa moja ya jamii kongwe Duniyani. Ilikuwa ni moja ya jamii za kidhalimu mno. Minara mikubwa ambayo bado ipo tokea enzi hizo za Misri ya Kale-Mapiramid yalijengwa na mamia kwa maelfu ya watumwa waliofanyishwa kazi kwa mijeledi na vitisho vya kunyimwa chakula. Mafirauni ndio waliokuwa watawala wakuu wa Misri ambao walistahabu kuitwa miungu na kuabudiwa na watu. Moja ya vyanzo vya habari juu ya Misri ya kale ni maandiko yao wenyewe. Maandiko haya yaligunduliwa katika karne ya 19. Na baada ya jitihada kubwa, herufi za Kimisri zikasomeka na kutoa mwanga mkubwa wa maelezo juu ya nchi hiyo. Lakini kwa vile maandiko haya yaliandikwa na wanahistoria waliofanya kazi serikalini, yalijaa maelezo ya kuisifu dola. Kwa upande wetu chanzo cha habari cha hakika juu ya jambo hili ni Qur’an. Ndani ya Qur’an, katika kisa cha Mussa, tunapata maelezo muhimu juu ya mfumo wa utawala wa Misri ya wakati huo. Aya zinabainisha kuwa kulikuwa na mihimili miwili ya utawala; Firauni na Baraza lake la ndani. Baraza hili lilikuwa na kazi ya kutoa ushauri muhimu kwa Firauni. Mara nyingi Firauni alikutana nalo na kufuata maoni ya baraza hilo. Aya zifuatzo zinaonyesha ushawishi wa baraza hilo kwa firauni:

Na Musa alisema: Ewe Firauni! Hakika mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. Inafaa nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila lilio la Haki. Nami hakika nimekujieni na dalili waziwazi kutokana na Mola Mlezi wenu. Basi waache Wana wa Israili wende nami. Akasema Firauni: Ikiwa umekuja na Ishara, basi ilete ukiwa ni katika wasemao kweli. Basi akaitupa fimbo yake, na mara ikawa nyoka dhaahiri.
Na akatoa mkono wake, mara ukawa mweupe kwa watazamao.
Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Hakika huyo ni mchawi mjuzi.
Anataka kukutoeni katika nchi yenu. Basi mnatoa shauri gani?
Wakasema: Mwache kidogo yeye na nduguye, na watume mijini wakusanyao,
Wakuletee kila mchawi mjuzi.

Q 7:104-112

Ikumbukwe kuwa hapa limetajwa Baraza lililokuwa likimshauri Firauni ambapo hapa linamshawishi Firauni kupambana na Musa na linapendekeza mbinu za kukabiliana naye. Tukiangalia kumbukumbu za Historia ya Misri, tunaona kuwa Baraza hili lilikuwa na matapo mawili; tapo la jeshi na tapo la makasisi. Hakuna haja ya kufafanua umuhimu wa jeshi. Kimsingi Jeshi ndilo lililojenga nguvu za tawala za Mafirauni. Tunachopaswa kukiangalia hapa ni jukumu la Makasisi. Makasisi wa Misri ya kale ni tabaka ambalo katika Qur’an linaitwa kama tabaka la wachawi. Wao waliwakilisha tabaka la wachawi lililounga mkono utawala. Ilisadikiwa kuwa watu hawa walikuwa na nguvu fulani na walimiliki elimu ya siri. Kutokana na mamlaka waliyokuwa nayo, Makasisi walikuwa na ushawishi kwa jamii ya Wamisri na kujihakikishia nafasi yao ndani ya utawala wa Mafirauni. Tabaka hili ambalo katika kumbukumbu za Misri lilijulikana kama Makasisi wa Amon, liljishughulisha na uchawi na kulipa nafasi tabaka la wapagani. Aidha walijifunza Sayansi mbali mbali kama vile unajimu, mahesabu na jeometri. Tabaka hili la makuhani lilikuwa ni kundi la siri lililomiliki elimu mahususi. Makundi kama haya hujulikana kama mashirika ya siri.

Katika Jarida liitwalo Mason Dergisi (Masonic Journal) ambalo huchapishwa na kusambazwa kwa masoni wa Kituruki, kuna maelezo kuwa mizizi ya Frimansori inatokea katika kundi hili la siri na hasa linatajwa lile la makasisi wa Misri ya kale. Kadri akili ya mwanadam inavyokuwa, ndivyo Sayansi inavyopiga hatua za maendeleo na kadri sayansi inavyopiga hatua za maendeleo ndivyo idadi ya mambo ya siri inavyoongezeka katika elimu ya Utamaduni wa siri. utamaduni huu wa siri ambao kwanza ulianzia mashariki; China na Tibeti na kisha kuenea India, Mesopotania na Misri ndio uliojenga msingi wa elimu ya kikuhani ambayo imefuatwa kwa maelfu ya miaka na kuunda msingi wa nguvu ya Makasisi nchini Misri. Sasa panawezaje kuwepo mahusiano baina ya falsfa ya siri ya makuhani wa Misri ya kale na Mafrimasoni wa leo? Utawala wa Misri ya kale ambao katika Qur’an unapigiwa mfano kama utawala wa kisiasa uliomkana Mungu ulitoweka maelfu ya miaka iliyopita. Je waweza kuwa na athari zozote hivi leo? Ili kupata jibu la maswali haya, hatuna budi kuiangalia Imani ya Makuhani wa Misri ya kale juu ya chanzo cha ulimwengu na maisha.
 
Imani ya Misri ya kale juu ya dhana ya Evolusheni ya Kilahidi

Katika kitabu chao The Hiram Key waandishi wa kimasoni Christopher Khight na Robert Lomas wanadai kuwa Misri ya kale inachukuwa nafasi muhimu kuhusiana na chimbuko la Masonri. Kwa mujibu wa waandishi hawa, dhana kuu ambayo imepandikizwa kwa Masonri wa hivi sasa kutoka Misri ya Kale ni lile la ulimwengu kutokea na kujiendesha wenyewe yaani kutokea kwa bahati nasibu. Wanaifafanua dhana hii ya kuchekesha kwa maneno haya:

Wamisri waliamini kuwa Maada ndiyo iliyokuwepo wakati wote; kwao wao halikuwa jambo la kimantiki kumfikiria Mungu kuwa ndiye aliyeumba kila kitu kutokana na hamna. Dhana yao ilikuwa hii kwamba Duniya ilianza pale utulivu ulipokuja baada ya mparaganyiko wa vitu na kwamba tangu wakati huo kumekuwa na ugomvi kati ya nguvu za umoja na nguvu za utengano… Ile hali ya mvurugiko iliitwa Nun, sehemu zote zilikuwa giza totoro, nguvu ya maumbile iliyokuwa ndani yake ikaamuru maisha yaanze. Nguvu hii isiyoonekana ambayo ilikuwemo ndani ya ile hali ya msambaratiko yenyewe nayo haikujitambua kama ilikuwepo.
 
Kushabihiana kwa Imani ya Misri ya kale na dhana ya Evolusheni.

Katika toleo lililopita tulinukuu maelezo kutoka kwenye kitabu kinachoitwa Hiram Key kilichoandikwa na waandishi wa Kimasoni Christopher Knight na Robert Lomas ambao wanadai kuwa Misri ya kale inachukuwa nafasi muhimu katika vyanzo vya Masoni. Kwa mujibu wa waandishi hawa, dhana kuu ambayo imeibuka kwa Masonri ya leo kutoka Misri ya kale ni ile ya ulimwengu kutokea kwa bahati nasibu na kujiendesha wenyewe.

Izingatiwe kuwa dhana hii inashabihiana na madai ya Walahidi ambayo yanatiwa nguvu na ajenda ya jumuiya ya wanasayansi kwa kutumia maneno haya; “Theory of Evolution” (nadharia ya evolusheni), “Chaos Theory” (nadharia ya mparaganyiko) na the essential organization of matter(chanzo cha mkusanyiko wa maada). Waandishi hawa wanaongeza kusema kuwa, kuna uwiano kati ya imani za kale za Misri na Sayansi ya leo lakini Sayansi wanayoimaanisha wao ni zile dhana za kilahidi. Licha ya ukweli kwamba nadharia hizi hazina msingi wowote wa kisayansi bado zimewekwa kinguvu nguvu katika fani ya sayansi kwa takribani karne mbili zilizopita na zinawasilishwa kama nadharia zilizohalalishwa kisayansi. Sasa tumefika kwenye nukta muhimu, hebu tufanye ufupisho wa maelezo ya kile ambacho tumekisoma hadi kufikia hapa:

1. Lipo kundi la Matempla linalodhaniwa kuwa ndio chimbuko la Masonri. Tumeona kuwa japo kundi hili lilianzishwa likiwa na imani ya Kikristo lakini matempla hawa wakaathiriwa na itikadi fulani za siri walizozikuta Jerusalem. Wakaachana kabisa na Ukristo na kujiundia jumuiya iliyopingana na dini.

2. Tmeona kuwa kimsingi itikadi iliyowaathiri matempla ilikuwa kabbalah.

3.
Tulipoichunguza Kabbalah, tukapata uthibitisho kuwa ingawaje itikadi hiyo imenasibishwa na Uyahudi lakini ilikuwa ni itikadi ya kipagani na ya zamani kuliko Uyahudi. Kwamba itikadi hii ilitumbukizwa tu katika dini hii na kwamba mizizi yake halisi inaonekana katika Misri ya kale.

4.Misri ya kale ilitawaliwa kwa mfumo wa kipagani wa Firauni na huko ndiko ilikokutwa dhanna inayounda msingi wa falsafa za sasa zinazomkana Mungu: Kwamba ulimwengu unajiendesha wenyewe, na umetokea kwa bahati nasibu.

Kwa hakika haya yote yanatupa picha ya wazi kabisa. Sasa swali ni je ni kwa bahati nasibu tu kwamba falsafa ya makuhani wa Misri ya kale ipo hadi leo, na kwamba vipo vielelezo vya mfungamano (Kabbalah-Matempla-Masonri) ambao ndio umehusika na uboreshaji wa dhana hii hadi kufikia leo hii?

Je yawezekana kuwa wale Masoni walioweka kumbukumbu yao katika historia ya Duniya tangia karne ya 18, wakifanya mapinduzi wakijenga falsafa na mifumo ya kisiasa ndio warithi wenyewe wa wachawi wa Misri ya kale? Ili kuliweka wazi zaidi jawabu la swali hili, hatuna budi kuchunguza kwa undani ambayo tumeeleza kwa kifupi.
 
Habari ya ndani juu ya kabbalah

“Kutoka” ni jina la kitabu cha pili cha Taurati. Kitabu hiki kinaelezea jinsi wana wa Israel, chini ya uongozi wa Mussa, walivyohama Misri kuepuka udhalimu wa Firauni. Firauni aliwashurutisha wana wa Israel kuishi kama watumwa na alikataa kuwaachia huru. Lakini alipokumbana na miujiza aliyoonesha Mwenyezi Mungu kupitia kwa Musa na maangamizi aliyowapelekea watu wake, Firauni alitulia. Kwa hiyo usiku mmoja wana waisrael wakajikusanya na kuanza safari ya kuhama Misri. Baadaye Firauni akawashambulia wana wa Israel lakini Mungu akawanusuru kwa muujiza mwingine alionesha kupitia kwa Mussa. Lakini katika Qur’an ndimo tunamokuta maelezo sahihi zaidi ya kuhama kwao kutoka Misri, hii ni kwa sababu Taurati imehujumiwa baada ya kufunuliwa kwa Mussa. Ushahidi madhubuti wa hili ni kuwa katika vitabu vitano vya Taurati; Kitabu cha mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na kumbu kumbu la Taurati kuna migongano mingi. Ukweli kuwa kitabu cha kumbukumbu na Taurati kimeishia na maelezo ya kufa na kuzikwa kwa Mussa ni ushahidi usiopingika kuwa sehemu hii itakuwa imeongezwa baada ya kifo cha Mussa. Katika maelezo ya Qur’an juu ya kuhama kwa wana wa Israel kutoka Misri hakuna mgongano hata kidogo kama yalivyo maelezo mengi mengineyo. Kisa hiki kimeelezwa kwa usahihi kabisa. Isitoshe kama zilivyo habari nyingine, Mwenyezi Mungu anatufunulia hekima na siri nyingi katika jambo linalozungumziwa. Kwa sababu hii pale tunapoziendea habari hizi kwa undani, tunweza kupata mafundisho mengi ndani yake.
 
Ndama wa dhahabu.

Miyongoni mwa mambo muhimu kuhusiyana na kuhama kwa wana wa Israel kutoka Misri, kama ilivyoelezwa katika Qur’an ni kuwa waliiasi dini iliyofunuliwa kwao na Mwenyezi Mungu licha ya ukweli kwamba Mwenyezi Mungu aliwanusuru na udhalimu wa Firauni kupitia kwa Mussa. Wana wa Israel hawakuweza kuielewa ile Tawhiid ambayo Mussa aliwafikishia badala yake wao walizidi kuielekea ibada ya sanamu. Qur’an inauelezea hivi muelekeo huu wa ajabu: (Na tukawavusha wana wa Israel baharini wakasalimika na balaa la Firauni) na ikawafikia watu waliokuwa wakiabudu masanamu yao.

“...Wakasema: Ewe Musa! Hebu tufanyie na sisi miungu kama hawa walivyo kuwa na miungu. Musa akasema: Hakika nyinyi ni watu msio jua kitu. Hakika haya waliyo nayo watu hawa yatakuja angamia, na hayo waliyo kuwa wakiyafanya yamepotea bure.

Q 7:138-139).

Licha ya maonyo ya Mussa, wana wa Israel waliendelea na upotevu wao na pale Mussa alipowaacha na kwenda Mlima wa Sinai, upotevu wao ukadhihirika zaidi. Akitumia fursa ya kutokuwepo kwa Mussa, mtu mmoja aliyeitwa Samir akawajia na kuwashawishi watengeneze sanamu la ndama na kuliabudu.

Mussa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na masikitiko. Akasema: Enyi watu wangu! Je Mola wenu hakukuahidini ahadi nzuri? Je umekuwa mrefu kwenu muda (wa) ahadi hiyo (mnaona hazitimizwi) au mmetaka ikushukieni ghadhabu kutoka kwa Mola wenu; na kwa hivyo mmevunja ahadi yangu? Wakasema: Sisi hatukuvunja ahadi yako kwa hiyari yetu walakini tulibebeshwa mizigo ya watu (vyombo vya dhahabu tulivyoviazima kwa wanawake wa Kimisri) tukaitupa (motoni ikayayuka ikaundwa mungu). Na namna hivi hivi alitia Samir (sehemu yake). Na akawatolea (Akawaundia katika myeyusho huo) Ndama, Kiwiliwili kamili kinacholia. Na wakasema: Huyu ndiye mungu wenu na mungu wa Mussa. Lakini Mussa amesahau
(Q 20:86-88).

Kwanini wana wa Israel walikuwa na msimamo wa ukaidi namana hiyo katika kukita masanamu na kuyaabudia? Ni nini chanzo cha muelekeo huu?

Ni dhahiri kuwa jamii ambayo hapo kabla haikuwahi kuamini masanamu, isingeweza kwa ghafla kufuata mwenendo huo wa kipumbavu wa kutengeneza sanamu na kuanza kuliabudia. Ni wale tu ambao ibada ya sanamu ilikuwa ya kawaida kwao ndio ambao wangeweza kuamini upuuzi huo. Lakini, wana wa Israili walikuwa ni watu ambao hapo kabla waliamini Mungu mmoja tangia zama za mzee wao Ibrahim. Jina hili, “Waisraili” au “wana wa Israili” mwanzoni kabisa lilitolewa kwa watoto wa Yaqubu, mjukuu wa Ibrahim. Baadaye jina hili likatumika kwa Wayahudi wote waliotokana naye. Waisraili walikuwa wameichunga ile imani ya Mungu mmoja ambayo waliirithi kutoka kwa wazee wao; Ibrahim, Is-haqa na Yaqubu (a.s). Wakiwa pamoja na Yusufu (a.s), walikwenda Misri na wakaichunga Imani yao ya Mungu mmoja kwa kipindi kirefu licha ya ukweli kwamba waliishi pamoja na Washirikina wa Misri. Katika maelezo yaliyotolewa katika Qur’an, inabainika wazi kuwa pale Musa alipowajia, Waisraili bado walikuwa watu walioamini Mungu mmoja. Isipokuwa tu, ni kuwa pamoja na kuamini kwao Mungu mmoja, Waisraili waliathiriwa na wapagani waliokuwa wakiishi nao na wakaanza kuwaiga, wakibadili dini waliyochaguliwa na Mwenyezi Mungu na badala yake kufuata Ibada ya sanamu ya jamii nyingine.

Tunapolichunguza suala hili kwa undani na kwa kuzingatia kumbu kumbu za historia, tunaona kuwa itikadi ya kipagani iliyowaathiri Waisraili ilikuwa ni ile ya Misri ya kale. Ushahidi muhimu wa kushadidia hitimisho hili ni kuwa yule ndama wa dhahabu waliyemuabudia Waisraili wakati Musa alipokwenda mlima Sinai alikuwa mfano halisi wa Masanamu ya Wamisri, Hatha na Aphis. Katika kitabu chake, Too Long in the Sun, Mwandishi wa Kikristo bw. Richard Rives ameandika hivi:

Hatha na Aphis Ng’ombe jike na fahari miungu ya Misri ilikuwa ikiwakilisha ibada ya jua. Ibada yao ilikuwa ni muendelezo wa historia ya utukuzo wa jua. Yule ndama wa dhahabu wa mlima Sinai ni ushahidi tosha wa kuthibitisha kuwa karamu iliyotangazwa ilihusiana na ibada ya jua…

Athari za dini ya kipagani ya Misri zilionekana katika sura nyingi tofauti. Mara baada ya kuwashinda wapagani Imani yao ya kishirikina ikadhihirika wazi kama aya inavyosema: Ewe Musa! Tufanyie miungu na sisi (yaani masanamu) kama wao walivyo na miungu. (7:138). Na kumbukeni habari hii pia (mliposema ewe Musa hatukuamini mpaka tumuone mungu wazi wazi (2:55).

Maneno yao haya yanadhihirisha kuwa nao walitaka kuabudu Mungu wa kimaada ambaye wangemuona kwa macho kama dini ya kipagani ilivyowapatia Wamisri mungu kama huyo. Mwelekeo huu wa Waisraili kufuata upagani wa Misri ya kale ambao tumeuelezea hapa, ni muhimu ueleweke kwani ndio unaotupa ufahamu wa jinsi kilivyohujumiwa kitabu cha Taurati na unatufahamisha chanzo cha Kabbalah. Tukiyatafakari mafundisho haya kwa mazingatio, tutaona kuwa ni katika vyanzo hivi unapokutikana upagani wa Misri ya kale na falsafa ya Kilahidi.
 
Amani na rehma za Allah ziwe juu yako X-paster.....useful quotes.

Wazayuni/Mayahudi ni kizazi kitukutu,inabidi tutosheke na namna walivyokuwa wakaidi wa amri za Mungu licha ya favor zote alizowapa: kuwatoa kwenye utumwa wa Firaun,kuwavukisha bahari kwa miujiza,kuwashushia chakula wanachotaka kutoka mbinguni etc......pia argument na Mungu juu ya ng'ombe gani achinjwe(refer chapter 2 quran).

Karibu 70% ya fitna zote zinazotokea duniani zinasababishwa na hawa jamaa,na wanajua openly kwamba sumu yao ni muumin wa kweli wa Allah...that's why they are so much afraid of sincerely faithful muslims (surah 59 quran)..na ndio maana tunasema Palestinians wataendelea kula kichapo sana na Wayahudi unless wasafishe tawheed zao na wajipange kama waislam wa kweli kuliko kupigania uarabu kama wanavyofanya sasa.

Waislam huwa hawashindi kwenye vita kwa nguvu zao bali kwa iman zao na kujiuzia kwao na maovu as well as kwa sababu ya uovu wa maadui zao,kwa hiyo ukiwa hauko tofauti na muovu....ujue kichapo ni halali yako ukizingatia unatenzwa nguvu za kijeshi.Hadi gay soldiers wanawashinda waislam...ujue hapo kuna hitilafu ya imaan

Wayahudi wanajua wazi zahma itakayowakuta kutoka kwa faithful believers in Allah kabla ya kiyama...........bali kwa ukaidi wao wanajaribu kuzuia kwa mikono yao kama alivyowafanyia Firaun kuwaua watoto wao kiume ili asitokee Mussa,lakini kwa uwezo wa Allah alizaliwa Mussa na akawekwa ndani ya bahari na kulelewa na Firaun mwenyewe.

Freemansory and other activities shud not make u unease,,,,,,dawa ni kusafisha nafsi yako na kuwa a sincere n true believer in Allah.Firmly abide with Quran and the prophetic teachings.
 
Rehma na Amani ya Allah hiwe pia nawe... shukran ya hakhi... Maneno yako ni kweli kabisa.
 
Kutoka Misri ya kale hadi Kabbalah

Wakati Musa angali hai, Waisraili walikwishaanza kutengeneza Masanamu kama yale yale waliyoayaona Misri na kuyaabudia. Baada ya Musa kutawafu (kufariki Duniya), hakukuwa tena na kikwazo cha kuwazuia Waisraili kuzama katika upotofu. Bila shaka haiwezi kusemwa kuwa ni Wayahudi wote waliokengeuka, lakini baadhi yao walifuata upagani wa Misri. Kwa kweli walishikilia mafundisho ya ukuhani wa Misri (mafundisho ya wachawi wa Firauni) ambayo yalijengwa kwa msingi wa imani ya jamii hiyo na wakaihujumu imani yao kwa kutumbukiza mafundisho haya ndani yake. Itikadi ambayo ilitumbukizwa katika Uyahudi kutoka Misri ya kale ilikuwa ni Kabbalah. Kama ulivyokuwa mfumo wa Makasisi wa Misri, Kabbalah nao ulikuwa mfumo wa siri na msingi wake ulikuwa utamaduni wa uchawi. Maelezo juu maumbile ambayo Kabbalah inayatoa ni tofauti kabisa na yale yaliyokutwa katika Taurati. Ni maelezo ya kilahidi yaliyoegamia dhana ya Misri ya kale juu ya uhai wa milele wa maada. Murat Ozgen, mwana Frimasonri wa Kituruki ana haya ya kusema juu ya suala hili:

Ni dhahiri kuwa Kabbalah iliundwa miaka mingi kabla ya kuja kwa Taurati. Sehemu muhimu ya Kabbalah ni ile nadharia juu ya muundo wa ulimwengu. Nadharia hii iko tofauti kabisa na maelezo juu ya maumbile yaliyopokewa na dini zinazoamini Mungu. Kwa mujibu wa Kabbalah, mwanzoni kabisa mwa hatua ya kuumbwa kwa ulimwengu, vitu vilivyoitwa Sefiroth vikiwa na maana ya miduara au mihimili yenye sifa za kiroho na kimaada iliibuka. Idadi ya jumla ya vitu hivi ilikuwa 32.

Ile kumi ya mwanzo ndiyo iliyoshikilia mfumo wa sayari na mingine iliyosalia imeshikilia makundi ya nyota angani. Imani hii ya ajabu ya Kabbalah inabainisha kuwa inahusiana kwa karibu na mifumo ya imani ya unajimu. Kwa hiyo Kabbalah inapinmgana kabisa na dini ya Uyahudi na inanasibiana kwa karibu na imani za zamani za siri za mashariki. Kwa kufuata mafundisho ya siri na ya kilahidi ya Misri ya zamani ambayo yalijengwa kwa msingi wa uchawi, Wayahudi wakapuuza mambo yaliyoharamishwa katika Taurati. Wakashikilia ibada za kichawi za Wapagani na hivyo Kabbalah ikawa itikadi ndani ya Uyahudi lakini yenyewe ikienda kinyume na Taurati. Katika kitabu chake kiitwacho Secret Societies and Subversive Movements, mwandishi wa kingereza Nesta H Webster anasema:

Uchawi kama tuujuavyo ulikuwa ukifanywa na Wakanani kabla ya kuvamiwa kwa Palestina na Waisraili. Misri, India na Ugiriki nazo zilikuwa na wachawi na waaguzi wao. Licha ya makemeo dhidi ya uchawi yaliyomo katika sheria ya Musa, Wayahudi walijiingiza katika uchawi na ule utamaduni mzuri waliourithi wakauchanganya na mawazo ya kichawi yaliyotoka katika jamii nyingine
 
Tamaduni za kipagani za uchawi wa zama za kale

Katika toleo lililopita tuliona kuwa Wayahudi walipuuza mambo yaliyohamishwa katika Taurati na hivyo kufuatia ibada za kipagani. Kwa ajili hii, Kaballa ikawa itikadi ndani ya dini ya uyahudi ingawaje ingawaje ilipingana na Taurati. Katika kitabu chake kiitwacho Secret Societies, and Subversive Movements, Mwandishi wa kiingereza Nesta Webster ameandika hivi:

Uchawi, kama tuujuavyo ulikuwa ukifanywa na Wakanani kabla Palestina haijavamiwa na Waisrail. Nazo nchi za Misri, India na Ugiriki vile vile zilikuwa ni za Wachawi na Waaguzi wao. Licha ya makatazo yaliyomo katika sheria ya Musa, Wayahudi wakauchanganya utamaduni wao mtukufu na mambo ya uchawi yaliyotoka katika jamii nyingine na mengine waliyoyatunga wenyewe. Hapa ndipo ilipo hoja ya Wapinzani wa Kabballa kuwa hii tunayoijua sisi hivi leo kama Kabbala, kimsingi haikutoka katika Uyahudi. Katika Qur’an, kuna aya inayozungumzia jambo hili. Mwenyezi Mungu anasema kuwa; wana wa Israili walijifunza tamaduni za kichawi za kishetani kutoka nje ya dini yao.

Wakafuata yale waliyofuata mashetani(wakadai kuwa yalikuwa katika Ufalme wa Suleiman na Suleiman hakukufuru, wakafundisha watu uchawi(waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani), na(uchawi) ulioteremshwa kwa Malaika wawili, Haruta na Maruta katika(mji wa) Babil. Wala(Malaika hao) hawakumfundisha yeyote ila mpaka wamambie, hakika sisi ni mtihani(wa kutazamwa kutii kwenu) basi usikufuru. Wakajifunza kwao mambo ambayo kwayo waliweza kumfarakanisha mtu na mkewe(na mengineyo) wala hawakuwa webye kumdhuru mtu yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza ambayo yatawadhuru wala hayatawafaa. Na kwa yakini wanajua kwamba aliyekhiari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika Akhera. Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia nafsi zao laiti wanagelijua
Q 2:102

Ayah Hii inabainisha kuwa japo, Wayahudi Fulani walijua kuwa watapata hasara katika maisha ya Akhera lakini bado walijifunza na kufuata tamaduni za kichawi.

Hivyo walikengeuka na toka katika sheria ambayo Mungu aliwashushia. Wakawa wamezitia hasarani nafsi zao kwa kutumbukia katika upagani(Itikadi za wachawi). Mambo yaliyoelezwa katika aya hii yanaweka bayana vinpengele vikuu vya mfarakano katika historia ya Wayahudi. Mapambano yalikuwa baina ya Mitume na wafuasi wai kwa upande mmoja na kwa upande wmingine Wayahudi waliopotoka na kuasi amri za Mungu na kuiga tamaduni za kipagani. Ni muhimu kukumbuka kuwa maovu ya Wayahudi wapotevu yamendikwa katika agano la kale. Ndani ya agano la kale kuna kitabu cha Nehemia ambamo Wayahudi wanaungama na kutubu. Waliokuwa wazawa wa Israili wakajitenga na wageni wote, wakasimama mahali pao, wakasoma katika kitabu cha Torati ya Bwana, Mungu wao, muda war obo ya siku, na siku nyingine, wakaungama, wamuabudu Bwana Mungu wao. Ndipo wakasimama madarajanai ya walawi, Yeshua na Bani, na Kadimieri na Shebania na Kenani, wakamlilia Bwana Mungu wao kwa sauti kuu.

(Wakasema) walakini(Baba zetu) hawakutii, wakaasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako walioshuhudia juu yao wapate kuwarejeza kwako; wakatenda machukizo makuu. Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua na wakati wa shida yao walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa katika mikono ya adui zao. Lakini walipokuwa wamekwishastarehe, walitenda mabaya tena mbele zako; kwa hiyo ukawaacha katika mikono ya adui zao, nao wakawatawala; hata hivyo waliporejea na kukulilia, uliwasikia toka mbinguni, ukawaokoa mara nyingi kwa rehema zako, ukawashuhudia ili uwarudishe tena katika sheria yako; lakini walitakabari wasisikilize amri zako,(ambazo mtu akizitenda ataisi katika hizo0 nao wakayaondoa, wakafanya shingo zao kuwa ngumu, wasitake kusikiliza. Ila kwa rehema zako nyingi hukuwakomesha kabisa wala kuwaacha; kwa maana wewe u Mungu Mwenye neema, Mwenye rehema. Basi sasa Ee Mungu, Mkuu Mwenye Uweza, Mungu wa kuogofya mwenye kushika maagano yote yaliyotupa sisi, wafalme wetu wakuu wetu wa makuhani wetu wa manabii wetu, na baba zetu na watu wako wote, tangu zamani za Wafalme wa Ashuru hata leo, na yasihesabiwe kuwa ni madogo. Lakini wewe u mwenye haki, katika hayo yote yaliyotupata; maana wewe umetenda yaliyotenda yaliyokeli lakini sisi tumetenda yaliyo mabaya na Wafalme wetu na wakuu wetu na wakuu wetu na makuhani wetu na Baba zetu hawakushika sheria yako wala hawakusikiliza amri zako na shuhuda zako ulizowashuhudia. Kwa kuwa hawakukutumikia wewe katika Ufalme wao na katika wema wako mkuu uliowapa na katika nchi ile kubwa yenye neema uliyowapa mbele yao wala hawakughairi na kuacha mabaya yao
.(Nehemia 9:2-4, 26-29, 31-35).

Kifungua hiki kinalezea tamaa ya kurejea katika imani ya Mungu mmoja ambayo Wayahudi wengi walikuwa nayo, isipokuwa katika kipindi Fulani cha historia kundi moja lilimeguka na kupta ushawishi kidogo kidogo, na baadae likaja kuwa tawala Wayahudi na baadae likaigeuza kabisa dini yenyewe. Kwa sababu hii, katika Taurati na katika vitabu vingine vya Agano la Kale kuna masalia yanayotoka katika mafundisho ya kipagani. Katika kitabu cha mwanzo inaelezwa kuwa Mungu aliumba Ulimwengu kwa siku sita wakati ambapo hapakuwa na chochote. Hii ni im’ani sahihi kabisa na inatokana na ufunuo sahihi. Lakini hapo hapo inasema kuwa Mungu alipumzika siku ya saba huu ni uzushi kabisa. Ni dhanna potofu iliyotoka katika upagani amabo unampa Mungu sifa za kibinaadamu:

Katika aya hii ya Qur’an Mwenyezi Mungu anasema:

Na tumeziumba mbingu na ardhi na vilivyomo katika yao katika nyakati sita wala hayakutugusa machovu
Q 50:38

Katika sura nyingine za Taurati kuna staili ya uandishi ambayo ni ya utovu wa heshima kwa Mwenyezi Mungu hasa zaidi katika zile sehemu ambazo sifa za kibinaadamu anapewa Mungu. Imani hizi potofu za kulinganisha udhaifu wa kibinaadamu ndizo imani ambazo wapagani walikuwa nazo kwa miungu yao bandia. Maneno mengine ya kufuru ni yale yanayodai kuwa Yakobo, Baba wa Waisrail alipigana mieleka na Mungu akashinda. Ni wazi kabisa hiki ni kisa cha kutungwa ili kuwatukuza Waisrail ni mwigo kutoka katika jamii za Wapagani. Katika agano la kale kuna mtindo wa kumuelezea Mungu kama Mungu wa Utaifa yaani Mungu wa Waisraili peke yao. Lakini Mungu kwa Ulimwengu na viumbe sote. Dhana hii ya dini ya Utaifa katika agano la kale inafanana na dhana za kipagani ambapo kila kabila linaabudia Mungu wake. Katika baadhi ya vitabu vya Agano la kale(mfano, Yeshua) amri zinazotolewa kufanya maovu dhidi ya watu wasiokuwa Wayahudi. Mauaji ya halaiki yanamrishwa bila kujali wanawake, watoto wala wazee. Mwenendo huu wa kinyama unakwenda kinyume kabisa na sheria ya haki ya Mungu, badala yake unarandana na ushenzi wa tamaduni za kipagani za kuabudu Mungu bandia wa vita.
 
Mafundisho ya kipagani yalivyoongezwa katika Taurati

Katika toleo lilipita tulimalizia kwa maelezo haya; kwamba katika baadhi ya vitabu vya Agano la kale(mfano Yeshua) zinatolewa amri za kufanya maovu dhidi ya watu wasiokuwa Wayahudi. Mauaji ya halaiki yannamrishwa bila kujali Wanawake, watoto wala wazee. Mwenendo huu wa kinyama unapingana kabisa na sheria ya haki ya Mungu, badala yake unarandana na ushenzi wa tamaduni za kipagani za kuabudia Miungu bandia wa vita. Mawazo haya ya kipagani ambayo yametumbukizwa katika Taurati yumkini yana chanzo chake. Lazima tu kulikuwa Matyahudi ambao walifuata mila isiyokuwemo katika Taurati.

Wakaishika na kuitukuza mila hiyo. Kisha, baadaye, Wakatumbukiza katika Taurati mawazo yaliyotokana na mila hii ambayo wao walikubaliana nayo. Chimbuko la Mila hii linaanzia nyuma kabisa kwa makuhani wa Misri(Wachawi katika utawala wa Firauni). Kwa kweli ilikuwa ni Kabbala iliyorithiwa na Wayahudi wengi. Kabbala ilikuwa na sura ambayo iliziwezesha itikadi nyigine za kipagani kujipenyeza katika dini ya Uyahudi na kustawi ndani yake. Wadau wa Kabbalah, bila shaka wanadai kuwa Kabbalah inafafanua tu kwa kina siri zilizofichikana katika Taurati, lakini kwa kweli, kama asemavyo mwanahistoria wa Kiyahudi kuwa Kabbalah si sumu isiyotambulia ambayo imeingia katika dini ya Uyahudi na kuiathiri kabisa. Hapo sasa inawezekana kukuta ndani ya Kabbalah yale masalia ya itikadi ya ulahidi ya Wamisri wa zama za kale.

Kabala-Itikadi inayopingana na itikadi ya kuumbwa kwa ulimwengu.

Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu anabainisha kuwa Taurati ni kitabu cha Mungu ambacho kilishushwa kama muongozo kwa Wanadamu.

Hakika tuliteremsha Taurati yenye uongozi na nuru ambayo kwayo Manabii waliojisalimisha waliwahukumu Mayahudi na Watawa na Maulamaa pia, kwa sababu walitakiwa kuhifadhi kitabu hicho cha Mwenyezi mungu, nao walikuwa mashahidi juu yake
Q 5:44

Kwa hiyo basi, Taurati, kama ilivyo Qur’an, ni kitabu chenye ilimu na maamrisho yanahusiana na Tauhidi inayobainisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na upweke wake, sifa zake, kuumbwa kwa Wanaadamu na viumbe vingine lengo la kuumbwa kwa binaadamu na kanuni za maadili za Mwenyezi mungu kwa Wanadamu. Hata hivyo, ile Taurati ya asili haipo tena hivi leo. Tuliyonayo hivi leo ni Taurati iliyoandikwa upya na kuhujumiwa na mikono ya binaadamu. Nukta muhimu ni kuwa ile Taurati ya asili na Qur’an zinashabihiana. Mote humo, Mwenyezi Mungu anatambuliwa kama Muumba. Anatambuliwa kama aliyetakasika na aliyeepukana na upungufu wowote ule na amekuwepo bila mwanzo. Chochote kile miinghairi yake ni kiumbe chake. Yeye ndiye aliyeumba ulimwengu wote, maumbile ya angani, maada isiyo na uhai, binaadamu na vyote hai. Mwenyezi mmoja tu.

Wakati ambapo huu ndio ukweli wa mambo, kuna malelezo tofauti kabisa yanyokutikana katika Kabbala, ambayo ni sumu iliyopenya katika mishipa ya uyahudi na kuathiri kabisa mafundisho yake juu ya Mungu; maelezo hayo yanapinga na kabisa na ule ukweli unaokutikana katika ile Taurati ya asili na katika Qur’an. Katika moja ya maandiko yake juu ya Kabbala, mtafiti mmoja wa Amerika, Lance S. Owens anatoa maoni yake juu ya vyanzo hasa vya itikadi hii. Itikadi ya Kabbalah imezaa dhana kadha wa kadha kuhusu Mungu. Nyingi kati ya hizo zimetoka nje kabisa ya mtazamo wa dini. Msingi mkuu wa imani ya WanaIsraili ulikuwa ni Kalima kwamba Mungu wetu ni mmoja. Lakini Kabbala ikdai kuwa wakati Mungu akiishi katika umbile la peke yake ambalo, katika Kabbalah linaitwa Ein Sof- asiye na udhaifu-upweke huu usiojulikana laima utakuwa umeanzia katika maumbile mengi ya kiungu.

Yaani kundi la Miungu. Miungu hii ambayo mwanakabbala aliita sefiroth yaani sura au nyuso za miungu. Jinsi ambavyo mungu alitokea katika umoja usioeleweka na kuingia katika wingi ilikuwa ni siri ambayo Wanakabbalah walihangaika kuitafuta.

Ni dhahiri kuwa hii sura ya Miungu inakubaliana na madai ya Washirikina siyo tu Mungu alikuwa katika wingi katika itikadi ya Kabbala bali hata upweke usiojulikana kulichukuwa sura mbili; ya kiume na ya kike, Baba na Mama, Hokhmah na Binah. Hizi ndizo sura za mwanzo za Mungu. Wafuasi wa Kabbala walikuwa wakitumia tamathali za kijinsia kuelezea jinsi maingiliano ya kimaumbile kati ya Hokhma na Binah yalivyozaa maumbile mengine. Jambo jingine la kuchekesha katika theolojia hii ya kishirikina ni kuwa, binaadamu hawakumbwa bali kwa kiasi Fulani na wao Wanaasili ya Kiungu. Bwana Owens, mtafiti wa Kiamerika anaielezea hivi dhana hii.

Picha ya ajabu ya Mungu iliyobuniwa na Kabbalah ina sura ya Upweke na wingi. Kwa mujibu wa dhanna hii ya Kabbalh, Mungu alikuwa Adamu Kadnoni. Mtu alikuwa sawa na Mungu nkatika ile sifa ya asili ya kutoumbwa na katika lile umbile lisilofahamika. Dhana hii ya ajabu inayomuelezea Adamu kana Mungu ilishadidiwa na mafundisho ya Kabbala; thamani ya tarakimu ya majina Adamu na Yehova na Adamu walikuwa sawa, hivyo Adamu alikuwa Mungu. Kwa dai hili binaadamu wote wanapofikia daraja la juu kabisa huwa sawa na Mungu. Theolojia hii inayojumuisha dhanna ya upagani ndiyo iliyojenga msingi uliopotosha chini ya Uyahudi. Wanakabbalah wa kiyahudi wakakiuka mipaka ya kawaida ya binadaamu kiasi kwamba wakafika mahala pa kuthubutu kufanya binaadamu miunga. Mbali na ishara hivyo, kwa mujibu wa theolojia hii, sio tu binaadamu walikuwa miungu bali miungu wenyewe ni wayahudi peke yao; watu wa jamii nyingine walihesbiwa kama binaadamu tu wa kawaida. Matokeo yake ndani ya ndani ya dini ya Uyahudi ambayo, kimsingi, ilianzishwa kwa ajili ya kumtii na kumtumikia Mungu, itikadi hii potofu ilianza kumea lengo likiwa kutimiza ujinga wa Wayahudi.

Licha ya kupinga kwake na Tautrati, Kabbal ikaingizwa katika Uyahudi na hatimaye ikaanza kuihujumu Taurati. Jambo jingine la kuzingatia kuhusiana na mafundisho potofu ya Kabbala ni ule uwiano wa fikra baina yake na upagani wa Misri ya zamani.

Kama tulivyosema awali, wamisri wa zamani waliamini kuwa maada na uhai; kwa maneno mengine walikanusha kuwa maada iliumbwa pasipo chochote. Kabbalah nayo inadai vivyo hiovyo kuhusiana na binaadamu. Inadai kuwa binaadamu hawa kuumbwa na kwamba Wanajiendeashea wenyewe maisha yao.

Kulizungumzia hili kwa maneno ya sasa ni kuwa Wamisri wa kale walikuwa walahidi na kimsingi itikadi ya Kabbala yaweza kuitwa secular Humanism. Ni muhimu kukumbuka dhanna hizi mbili; ulahidi na Secular Humanism ndizo zilizozaa itikadi ambayo imetawala Duniyani kwa zaidi ya karne mbili zilizopita.

Yafaa kuuliza iwapo kuna watu ambao wameziendeleza itikadi za Misri ya kale na Kabbalh tokea katikati ya kipindi cha nyuma cha historia hadi leo hii.
 
Wale waliokuwa Matempla ndio hao wakawa Mafrimansori

Wakati tulipowazungumzia Matempla huko nyuma, tulisema kuwa kundi hili mahususi la Makruseda liliathiriwa na “siri” waliyoikuta Jerusalem.

Katika kitabu Foucaut’s Pendulum Mwanafasihi mashuhiri wa Italia umberto Eco, naye anauelezea ukweli huu. Katika riwaya yake yote anasimulia kupitia vinywa vya wahusika wakuu wa riwaya yake kuwa Matempal waliathiriwa na Kabbala na kwamba wale Makabbala walikuwa na siri ambayo chanzo chake chaweza kuwa ni Mafirauni wa Misri ya kale.

Kwa mujibu wa Eco, baadhi ya Wayahudi mashuhuri walijifunza siri Fulani kutoka kwa wamisri wa zamani na baadae wakazi tumbukiza katika vitabu vitano vya kwanza Agano la kale.

Lakini siri hii ambayo ilisambazwa chinichini, ilikuwa ikijulikana kwa Wanakabbala peke yao. Baada ya kuelezea kuwa Wanakabbala waliisoma siri hii ya Misri ya kale katika Hekalu la selemani, Eco pia anaandika kuwa Matempla nao wakaisoma siri hii kutoka kwa walimu wa Kabbala mjini Jerusalem.

Siri hii ilikuwa ikijulikana kwa kikundi kidogo sana cha Waalimu wa Kiyahudi waliobakia Palestina. Matempla wakaisoma kutoka kwa Waalimunhao. Pale Matempla walipofuata itikadi mseto ya Misri ya Kabbal ndipo walipofarakana na dhehebu la Kikristo lililokuwa likiwatawala Ulaya.

Ulikuwa ni mfarakano ambapo wao walishirikiana na nguvu nyingine kubwa ya Wayahudi. Baada ya Matempla kutiwa mbaroni kwa amri ya pamoja ya Mfalme wa Ufaransa na Papa mnamo mwaka 1307, kundi hili likatokomea chini chini lakini athari zake zikabakia. Tena zikawa mbaya zaidi na zilizokuwa na uelekeo madhubuti.

Kama tulivyosema awali, idadi ndogo ya Matempla walinusurika katika kamata kamata na kukimbilia kwa Mfalme wa Scotland, utawala pekee wa Kifalme barani Ulaya ambao hakuyatambua mamlaka ya Papa.

Kule Scotland, Matempla wakajipenyeza katika jumuiya ya Well Builders na wakaitawaa. Jumuiya zikafuata ule utamaduni wa Matempla na hapo ndipo ilipopandwa mbegu ya Masoni.Kama ilivyofafanuliwa kwa kina katika kitabu kiitwacho The New Masonic order, kuanzia karne ya kumi na nane ndipo yanapoonekana masalia ya Matempla na Mayahudi kadhaa walioshirikiana nao katika vipindi mbali mbali vya historia ya Ulaya.

Bila kutoa maelezo mengi, zifuatazo ni nukta muhimu za utafiti. Katika mji wa Province nchini Ufaransa kulikuwa na kambi ya Matempla waliokimbilia nchini humo na kujificha wakati wa ile kamatakamta.

Kielezeo kingine ni kuwa huko ndiko kulikokuwa na kituo mashuhuri cha Ukabbal. Province ndipo mahali ambapo fasihi simulizi ya kabbala iliandikwa katika kitabu. Kwa mujibu wa wanahistoria, uasi wa wakulima nchini Uingereza mwka 1381 ulichochewa na jumuiya Fulani ya siri.

Watafiti wa historia ya Frmasonri wamekubaliana kuwa jumiya hii ya siri ilikuwa ya Matempla. Ule uasi haukuwa tu wa kizalendo bali pia ulilenga kulishambulia kanisa katoliki.

Nusu karne baada ya uasi huu, Kasisi mmoja wa Bohenia John Hus akaanzisha vurugu kulipinga Kanisa Katoliki. Kama kawaida, nyuma ya uasi huu walikuwepo Matempla.

Isitoshe Huss mwenyewe alikuwa akiipenda sana Kabbal. Yeye alikuwa akimpenda sana Avigdor Ben Isaac Kara. Mtu huyu alikuwa Mwalimu mashuhuri wa kiyahudi mjini Prague na pia alikuwa Mwanakabbala.

Vielezeo hivi vinaonesha kuwa ushirikiano baina ya Matempla na Wanakabbala ilileng kubadilisha mfumo wa jamii ya Ulaya. Mabadiliko haya yalijumuisha misingi ya utamaduni wa Kikristo ambao ndio utamaduni mama wa ulaya na badala ya utamaduni huu uwekwe utamaduni uliojengwa kwa misingi ya kipagani kama vile kabbal. Kisha yafuate mabadiliko ya kisiasa. Mfano ni mapinduzi ya Ufaransa na Italia.

Huko mbele tutaona vipindi vya mabadiliko ya Historia ya Ulaya. Katika kila kipindi tutakutana na ukweli kuwa kulikuwa na nguvu iliyotaka kuitenganisha Ulaya mbali kabisa na mafundisho ya Kanisa na badala yake iweke itikadi ya kisekula na hivyo izisambaratishe taasisi zote za dini.

Nguvu hii ilijaribu kuichaguzi Ulaya kuikubali itkadi iliyorithiwa kutoka Misri ya kale kupitia Kabbala. Tulikwishabainisha huko nyuma kuwa misingi ya Usekula ni dhana za Humanism na Matearialism au utu mtu na ulahidi.
 
Itikadi ya utu- ‘Humanism'

Yasadikiwa na wengi kuwa Humanism ndiyo itikadi madhubuti ambayo inampandikiza mtu hisia za upendo, utulivu, na udugu. Lakini kifalsafa dhana hii ina maana kubwa zaidi. Humanism ni utaratibu wa fikra ambao unaichukulia dhana ya utu kuwa ndio msingi wa lengo lake kuu.

Kwa maneno mengine unawataka watu wajitenge mbali na Mungu Muumba, kisha washughulike tu na maisha yao na utu wao. Kamusi ya kiingereza iitwayo Common Dictionary inaliainisha neno Humanism kama ni mfumo wa itikadi uliojengwa juu ya msingi wa maadili, sifa, na tabia, ambazo zinaaminika kuwa bora zaidi kwa vigezo vya binaadamu wenyewe bila kutegemea mwongozo wowote wa kiungu.

Ainisho la wazi zaidi la humanism limetolewa na wale wanaunga mkono dhana hii. Mmoja kati ya wapiga debe wakuu wa itikadi ya humanism ni bwana Carloss Lamont. Katika kitabu chake, the philosophy of humanism, mwandishi huyu ameandika; " kwa ujumla Humanism inaamini kuwa maumbile yanatokana na mkusanyiko wa vitu halisi ambavyo msingi wake na nguvu ya maada".

Kitabu hiki kinazidi kueleza kuwa maada ndio msingi wa Ulimwengu, na kwamba nguvu za kiungu hazipo.

Dhana ya nguvu za Kiungu kwa upeo wa Binaadam haina ushahidi. Kwamba watu hawana roho za kudumu milele yaani zisizokufa, na ulimwengu kwa ujumla hauna Mungu aliyeuumba wala Mungu wa milele.

Kama tunavyojionea wenyewe katika nukuu hizo, Itikadi ya humanism inafanana kabisa na itikadi ya Atheism, na ukweli huu unakubaliwa bila ubishi na Wahumanisti wenyewe.

Zilikuwepo ilani mbili muhimu zilizochapishwa na Wahumanisti katika karne iliyopita. Ilani ya kwanza ilichapishwa mwaka 1933 na ikapitishwa na watu wao muhimu wa wakati huo.

Miaka arobaini baadaye (yaani mwaka 1973), ilani ya pili ya Wahumanisti ikachapishwa. Ilani hii ilithibitisha ile ya awali, lakini ilitiwa nyongeza kufuatia hatua Fulani za maendeleo ambazo zilipigwa wakati huo. Maelfu ya wanafikra, waandishi wa vitabu, na wanahabari, walisaini ilani hii ya pili, ambayo inaungwa mkono na chama cha harakati za wahumanisti wa Amerika. Tukiziangalia ilani hizi tunagundua kuwa, katika kila ilani kuna msingi mmoja mkuu ambao ni dhana ya Atheism.

Dhana hiyo inasema kwamba Ulimwengu haukuumbwa, na Wanaadamu pia hawakuumbwa.. Kwa msingi huo wanaadam wanaishi kwa kujiendesha wenyewe na kwamba hawawajibiki kwa mamlaka yeyote isipokuwa kwa wao wenyewe.. Na kwamba imani juu ya Mungu inadumaza maendeleo ya watu na jamii. Kwa mfano vipengele sita vya kwanza vya ilani ya Wahumanisti ni hivi vifuatavyo;

Mosi, Wahumanisti wanaitakidi kuwa Ulimwengu unajiendesha wenyewe na haukuumbwa.

Pili, dhana ya humanism inaitakidi kwamba mtu ni sehemu ya maumbile, na kwamba ameibuka kutokana na mfumo unaojiendesha wenyewe.

Tatu, wakishikilia mtazamo wa maisha ya kiagoniki, wahumanisti wanaona kuwadhana ya pande mbili za nafsi na mwili lazima ipingwe kabisa.

Nne, itikadi ya humanism inatambua kuwa utamaduni wa kidini wa mtu na ustaarabu wake kama ulivyoelezwa na historia ni zao la hatua za polepole za maendeleo zitokanazo na mahusiano baina yake na mazingira na mazingira yake. Mtu anayezaliwa katika utamduni Fulani, kwa kiasi kikubwa, anajengeka kwa utamaduni huo. Tano, dhana ya humanism inatangaza kuwa maumbile ya ulimwengu yaliyoelezwa na sayansi ya leo yanatupilia mbali nguvu yeyote ya mbinguni kuhusiana na maadili ya binadamu. Sita, tunaamini kuwa dhana ya theism, deism, modernism na aina kadhaa za itikadi mpya zimepitwa na wakati.

Katika vipengele hivyo, tunaiona waziwazi nafasi ya falsafa ya common ambayo inajidhihirisha yenyewe kwa majina ya Materialism, Darwinism atheism na agnosticism. Katika kipengele cha kwanza dhana ya ulahidi ya uhai wa milele wa ulimwengu umeelezwa wazi. Kipengele cha pili kinasema kuwa binadamu hawakuumbwa. Hivi ndivyo isemavyo nadharia ya evolusheni. Kipengele cha tatu kinakanusha mamlaka ya Mwenyezi Mungu juu ya ulimwengu na walimwengu na kipengele cha sita kinaikataa imani juu ya Mungu. Ikumbukwe kuwa madai haya ndiyo yale yale ya zile duru zenye chuki na dini sahihi. Sababu ni kuwa dhana ya humanism ndio msingi mkuu wa hisia zote zinazopinga dini.

Hii ni kwasababu dhana hii inasema kuwa mtu ataachwa hivyo hivyo bila kuhesabiwa. Katika historia yote huu ndio umekuwa msingi wa madai ya kumkanusha Mungu. Katika aya hii ya Qur'an Mwenyezi Mungu anasema; Je anafikiri binadamu kuwa ataachwa bure? Je hakuwa tone la manii lililotonwa? Kisha akawa kidonge cha damu, kisha akamfanya namna mbili, mwanaume na mwanamke. Je! Hakuwa huyo ni muweza wa kuhuisha wafu?

Hapa Mwenyezi Mungu anasema kuwa watu hawakuachwa tu hivi hivi na anawakumbusha kuwa wao ni viumbe wake. Hii ni kuwa pale mtu anapotanabahi kuwa yeye ni kiumbe wa Mungu, basi aelewe kuwa haishi bila ya kuangaliwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom