MY RESEVERD COMMENTS:
1. Nimesoma hiyo taarifa iliyoandikwa kwa kiingereza, nimeridhika pasipo shaka yoyote kuwa hiyo ni hati ya Tundu Lissu mwenyewe..
2. Hicho ni Kiingereza chake kwa 100%. Amepataje simu au kifaa cha kumwezesha kutuma ujumbe huu? It's a million dollar question to be answered in another day. Lakini kinachoonekana hapa ni kama vile, yeye katoa ujumbe wa mdomo na mtu mwingine anayesimamia Akaunti zake za mitandao ya kijamii akauandika na kuposti. Hilo ni zuri, maana hii ndio njia Moja ya njia za wanaharakati wa ukombozi na wapigania uhuru wote walio ktk kifungo hutumia kuwasiliana na watu walio nje..
3. Na napenda kuamini kwa 100% kuwa, ndani ya serikali, Jeshi la Polisi, Magereza na TISS bado Kuna watu wema na wanaompenda Tundu Lissu na wanaoamini kwa dhati kabisa kile anachosimamia na kukipigania kuwa ndio ukombozi wao pia kutoka katika nira na vifungo vya utumwa wa kimwili na kifikra uliotengenezwa na mfumo wa ki CCM kwa takribani miaka 65 sasa tangu uhuru 1961 ambao sasa ni lazima uangushwe na kupotelea mbali...
4. Sasa mliokuwa hamuamini, bila shaka mtageuza fikra zenu zifikiri kivingine na muanze kuelewa kuwa, hii sio kesi ya kawaida ambayo mahakama ktk mifumo yake ya kawaida ya utoaji haki inaweza kuamua..
5. Hii ni kesi ya akina Jakaya Kikwete na genge lake wakimtumia Samia Suluhu Hassan kama egemeo lao ili ammalize huyu Bwana Tundu Lissu ambaye wanamdhania ni adui yao, kikwazo cha malengo yao ya kisiasa na kiuchumi.
6. Ingekuwa ni kesi ya kisheria, ingeshaishia kule chini kwenye mahakama ya ukabidhi ya Kisutu kwa kuwa haina miguu ya kisheria kuweza kusimama mahakamani..
7. Lakini kwa kuwa, waovu na wahuni hawa wameshindwa kumpata kwa njia zingine ikiwemo kumuua kwa risasi, wamedhania na wanaendelea kudhani kuwa kwa kuitumia mahakama wanaweza kutimiza mpango na malengo yao, KUKIONDOA WANACHODHANI KIKWAZO, uhai wa Tundu Lissu...!
8. Tunawaapia kwa Jina la Mungu Yehova aliyehai katika Yesu Kristo kuwa, mpango wao hautafanikiwa. Tundu Lissu hatakufa kwa mapenzi na utashi wao. Kabla hajafa yeye, wataanza kufa wao kwanza mmoja baada ya mwingine..!
9. Kila anayemjua na kumwamini Mungu Yehova ktk Yesu Kristo, endelea kumuombea Tundu Lissu. Shetani Ibilisi ndani ya Samia na genge lake wapoteane na waanze kuchinjana wao kwa wao. Sema hivyo hivyo...
10. Tumia Neno la Mungu (Upanga wa Roho) unapoomba. Mistari hii ni bunduki ya kuwamaliza watesi wetu wote. Itumie kikamilifu ktk maombi yako:
Ayubu 5:12-15 SUV
".....Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao. Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka. Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vilevile kama usiku. Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari...."
Isaya 54:17 SUV
"......Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA...."
Maombolezo 3:31-33 SUV
".....Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha...."
Mungu Yehova ktk Yesu Kristo akubariki sana. Amina🙏🙏🙏🙏