Kukamia mechi moja sio jambo zuri kwa timu inayojitambua, unatakiwa uweke nguvu kwenye mechi zote 30 za ligi ili utoboe na sio kuchagua mechi na kutumia nguvu kubwa kupita kiasi ukasahau kwamba Kuna mchezo mwingine mbele yako Tena unaucheza ndani ya siku 3!
Azam walimwaga jasho lote kwenye mechi ya yanga, wakacheza Kama vile akuna kesho nyingine, matokeo yake wanaadhibiwa vikali na NAMUNGO!
Wachezaji wao Wana fatique kubwa sana yaani wako unga vibaya sana, unakamia mechi moja na unafungwa unapoteza point 3, mechi inayofata unapoteza Tena point 3 ambazo ungetumia akili ungezipata!
YANGA nao walikuwa na fatique lakini utimamu wao wa kimwili umewasaidia PAKUBWA ashukuriwe kocha wa viungo anafanya kazi yake ipasavyo ingekuwa timu nyingine kucheza mechi 2 ngumu ndani ya siku 4 isingetoboa!
Sasa Azam wameisoma namba na funzo wamelipata