FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

Kikosi cha Wydad leo
20230422_155309.jpg
 
Kuna huyu DJ wa radio Fm 98.9MHz anapiga wimbo Daz Nundaz kamanda,na unaimba dakika chache kabla ya mechi hahahaa.
 
Leo nitakuwa makini kumuangalia huyo golikipa namba 3, ili nijiridhishe kama kweli ni hodari mlangoni, au kwenye mechi na Yanga mchezo tu ndiyo ulimkubali.
Kumuangalia huyo mtoto kwa waarabu utakuwa unamuonea, utopolo na waarabu ni sawa na mbingu na ardhi.
 
Duh Formation yao si ya kudefence.
 
Naaam mpira umeanza mabibi na mabwana kuleni chuma hicho
 
Najua ni kazi ta kocha ila mimi binafsi huwa sioni kabisa mchango wa Ntibazonkiza, kama Phiri yuko poa nadhani ingependeza akaanza kisha Ntibazonkiza akaingia kipindi cha pili kama ambavyo ilikuwa kwa Morisson enzi zile.

Ntiba huwa anapoteza sana mipiria na akili yake huwa inawaza kufunga yeye mwenyewe badala ya kusaidia washambuliaji ambao muda mwingi hukaa kwenye nafasi za kufunga wakati ambao yeye amekalia kupiga chenga zisizokuwa na mwisho mzuri (kunyang'anywa mpira).
 
Mpaka kufika saa kumi na mbili jioni makolo fc watakuwa wameshajua mbivu na mbichi . Kikubwa uzalendo muhimu japo haitasaidia kuepuka mvua ya goli tano
Huyo dogo kwenye Avatar yako akimaliza konyagi lazima afe😂😂😂🤣🤣

Naitakia Kila la kheli Kwa timu yangu ya Simba ushindi mnono.....
SIMBA GUVU MOYA 🦁🦁🦁🦁
 
Back
Top Bottom