FT: CR Belouizdad 3-0 Yanga SC | CAF Champions league | Stade du 5 Juillet | 24.11.2023

FT: CR Belouizdad 3-0 Yanga SC | CAF Champions league | Stade du 5 Juillet | 24.11.2023

Leo ndo leo majira ya saa 4 usiku Yanga sc watakuwa wanacheza mechi yao ya kwanza katika ligi ya mabingwa Afrika Mungu ibariki Yanga SC.
YANGA YAANZA VIBAYA MAKUNDI CAF, YAPIGWA 3-0 UGENINI

Ikicheza kwenye Uwanja wa Stade du 5 Juillet Nchini Algeria, Yanga imeshindwa kutamba baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-0 dhidi ya CRBelouizdad katika mchezo wa Kundi D kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF)

Magoli yamewekwa wavuni na Abdelraouf Benguit (10), Abderrahmane Meziane (45) na Lamin Jallow (90)

Mchezo ujao, Yanga itaikaribisha AlAhly ya Misri kwenye Uwanja wa Mkapa, Desemba 2, 2023
Kama Yanga mnapigwa na kibonde magoli 3 kwa nunge, mechi na Al Ahly tutegemee elnino ya magoli. Kweli Yanga ni sawa na kibatari kinachowaka kikiwa ndani ya nyumba lakini ukikitoa nje kinazimika. Pole sana Utopolo!
 
IMG_0895.jpg

Msimamo wetu, tuliweka kabla ya mechi na tutaendelea kila baada ya mechi.

Msimamo ni uleule wa 1998[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Unachezwa uwanjani; umeona jinsi ambavyo Yanga ilivyomiliki mpira ila ilifungwa kutokana na weakness katika positions muhimu kadhaa ambazo mastaa wa Yanga walikuwa wamechoka kutokana na mashindano ya FIFA na wengine hawakuweza kucheza kabisa kutoka na hiyo ratiba ngumu ya FIFA. Mchezo ujao wataikuta Yanga imekamilika na tutarudi hapa kuhabarishana matokeo.

Wao CRB hawakuwa na hizo ratiba za FIFA? Ila utopolo bana [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hiyi ndiyo ukisikia mpemba anasema "kufungwa twafungwa lakini chenga twawala".

Mmenichekesha sana vyura, poleni, ndiyo ukubwa huo.

Nilikuwa nashangaa naambiwa yanga anapiga mpira hatari. Nikasema ohhhh sasa hawa chura wanatupa kero mjini.

Lakini jamaa wao wanafunga tu. Leo marudio saa ngapi tuangalie[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom