FT: Far Rabat 1-0 Yanga SC | CAF Champions League | Olympique de Rabat | Februari 7, 2026

FT: Far Rabat 1-0 Yanga SC | CAF Champions League | Olympique de Rabat | Februari 7, 2026

Hapo kocha amezingua sana! Yani wachezaji wote walikua na morali ya juu labda Okello hakua na mechi nzuri! Ila mbinu ya mwalimu imemfelisha pakubwa! Sio lazima afunguke sana ila kupaki Semi kwenye mechi ya maamuzi haikua mbinu bora! Angecheza Low block kipindi cha kwanza cha pili angepandisha mashambulizi viungo wa kutosha mana Defence ilikua sawa kuna namna angewakata tu pale kati sasa ilikua hata Foward akipewa ndefu tayari ana defender wa3 wako mwilini ... atafanya nn
Huyo Pacome akichekesha tayari kwanzia viungo wao wa kati mpk Ddefenders washamvaa akiwatoka akipiga mbele hamna mtu! Jamani nmekwazika basi tu! Pedro sio mbaya sana ila kuwa kocha ni kuchagua mbinu pia
Amenisikitisha sana, mimi nilishajiandaa kisaikolojia yanga kufungwa lakini sio kwa mpira ule. Nilijua tutaenda kupishana nao uwanjani.

Sasa tuombee al ahly ashinde tu, yule mwarabu mwingine inabidi tumpige kama ngoma maana hatuna cha kupoteza
 
Boka na dube cku ntakutana nao ntawachapa ngumi za kila rangi. Ila tena tusisahau kauli zetu wenyewe za yanga kupangwa kundi gumu ndo tulianza nazo makundi yalivotoka
 
Amenisikitisha sana, mimi nilishajiandaa kisaikolojia yanga kufungwa lakini sio kwa mpira ule. Nilijua tutaenda kupishana nao uwanjani.

Sasa tuombee al ahly ashinde tu, yule mwarabu mwingine inabidi tumpige kama ngoma maana hatuna cha kupoteza
Ili Yanga ifuzu inatakiwa hesabu hizi:
Al Ahly ashinde hata 1:0
Kisha Yanga ashinde 2:0

Jambo lililo gumu ni kuombea mwenzako ndiye akubebe wakati anahitaji sare tu kuongoza kundi
 
Ili Yanga ifuzu inatakiwa hesabu hizi:
Al Ahly ashinde hata 1:0
Kisha Yanga ashinde 2:0

Jambo lililo gumu ni kuombea mwenzako ndiye akubebe wakati anahitaji sare tu kuongoza kundi
Goal different tuna -2, wakati far rabat wana 1. Kama al ahly akishinda 1-0, kwa far rabat itabaki 0 maana hiyo yanga atatakiwa aondoe zile -2 halafu aongeze goli/magoli mengine ili yeye awe na advantage maana yake atapaswa kushinda sio chini ya goli 3-0 ili afuzu moja kwa moja.

Suala la kuchungulia chungulia uko kwa wemgine na kumwombea ubaya adui hatuna budi kufanya hivyo maana tushayatimba. Al ahly akifungwa anashuka nafasi ya pili kwahiyo hawezi kuichukulia game kirahisi rahisi tu
 
Maombi yote kwa Al Ahyl
1000303313.jpg
 
Hapana ni hivi, Yanga ina -2 huku AS FAR ana 1 hivyo AS FAR akifungwa na Al Ahly goli 1:0 itamfanya AS FAR wawe na 0 na Yanga akishinda goli 2:0 maanake Yanga nayo itakuwa na 0
Kwahiyo itakuwa Yanga amefungana na As Far katika H2H na pia watakuwa wamefungana katika goal differences kwasababu wote watakuwa na 0.

Kipi kitachoifanya Yanga ifuzu endapo matokeo yatakuwa hivyo? Ni magoli ya kufunga atakuwa kamzidi AS FAR kwa kufikisha magoli 4 huku AS FAR akiwa na magoli 3

Yanga kufuzu hesabu inatakiwa Yanga ishinde 2:0 huku upande wa Al Ahly iishe kwa ushindi kwa Al Ahly 1:0
 
Mama akitoa 2bn kwa kila goli yanga atatimba robo fainali kama amekaa.
Kolo pelekeni hili ombi kwa Rais kupitia kwa Makonda fasta
 
Hapana ni hivi, Yanga ina -2 huku AS FAR ana 1 hivyo AS FAR akifungwa na Al Ahly goli 1:0 itamfanya AS FAR wawe na 0 na Yanga akishinda goli 2:0 maanake Yanga nayo itakuwa na 0
Kwahiyo itakuwa Yanga amefungana na As Far katika H2H na pia watakuwa wamefungana katika goal differences kwasababu wote watakuwa na 0.

Kipi kitachoifanya Yanga ifuzu endapo matokeo yatakuwa hivyo? Ni magoli ya kufunga atakuwa kamzidi AS FAR kwa kufikisha magoli 4 huku AS FAR akiwa na magoli 3

Yanga kufuzu hesabu inatakiwa Yanga ishinde 2:0 huku upande wa Al Ahly iishe kwa ushindi kwa Al Ahly 1:0
Basi al ahly wasituangushe. Sisi na wao ni ndugu
 
28000 zinapotea kuangalia watu wamepaki ma SGR ujinga mtupu! Watu wanacheza low block 90min!! Mpaka Pacome kwa defender! Hata wakisema wafanye counter mbele kuna Mtu mmoja tu akitoa cros hamna mtu! Wachezaji wanapress - wa dk 90 hata angekua nani hawezi kupata utulivu wa kupass pass zenye macho lazima uvurugwe! Niliacha kuangalia dk ya 60 tu nikaona upuuzi! Watu wanacheza langoni kwenu saa zote utafikiri mmepaki Sgr labda Dodoma Jiji inacheza na Al Ahly
Mbinu ya kizamani sana. Chezea mpira na shambulia kama ukifungwa basi utakuwa umezidiwa uwezo na mbinu. Huu ujinga wa kulinda goli sifuri ni ujinga tupu. Huyu kocha sioni future yake ndani ya YANGA hana mbinu za kisasa. Hata uchezaji sasa hivi imekuwa wa vipasi vifupi vifupi ambavyo vinapoteza tu muda.
 
Ila mimi naona mbinu haikuwa mbaya hasa unapocheza away, hata Al Ahly pamoja na ubora wake wote ila away anakuacha ucheze mpira kisha yeye anacheza na moments tu. Binafsi natofautiana na wengi ambao wanamlaumu kocha, kocha alikuwa sahihi kimbinu ila kilichomuangusha ni wachezaji wakuweza kutelekeleza mpango kazi wake wamefeli. Jana wachezaji wakipata mipira wanakosa utulivu na umakini na uharaka wa kufanya counter attack mwisho mipira inapotea kirahisi. Mechi dhidi ya Al Ahly kule Misri Yanga ndio timu iliyotengeneza nafasi nyingi zaidi kwenye kipindi cha kwanza na wamepiga on target nyingi huku Al Ahly hawakupata nafasi ya kupiga hata on target moja lakini mwisho wa siku wanapata on target moja na goli wakati sisi tumepoteza minafasi kibao, goli lenyewe ni la kizembe kabisa kwenye ukabaji

Kocha anafanya mabadiliko ili asawazishe, Mudathir anachomesha, Maxi na Dube wanapoteza nafasi ya dhahabu kuipatia goli. Mechi ya marudiano ni makosa ya Boka na makosa ya wachezaji kushindwa kupata goli goli la ushindi. Maxi anapiga free header anashindwa kulenga goli, jana Dube nafasi kama zile anashindwa kufunga unategemea uingie robo kwa wachezaji wa namna hiyo wanaoshindwa kutumia nafasi?

Kocha angethubitu kufunguka ni kweli angepata goli ila Yanga ingeoga magoli ya kutosha kwenye counter attacks.
Uoga tu na kutojiamini. Kwa kupaki kule gari unategemea hzo counter zingepstikanaje? Unapokwenda kipambana huku umejaa uoga lazima kisaikoljia uteseke tu na mwisho wa siku utafungwa.

Kupaki Baci 90 minutes kwa kulinda 0 goal kwa mpira kama ule ni matumizi mabaya ya nguvu za wachezaji. Hiyo energy na morali waliyoitumia kudefendi hewa wangeitumia kupambana kwa kucheza na kushambuli pengine mambo yangekuwa tofauti. I believe in playing and attacking siyo kujikunyata kama vile mbwa kamuona chatu. HUO NI UOGA NA UOGA HUSABABISHA MATOKEO MABAYA!
 
Leo timu inacheza kama vile hatuitaki robo..Mabeki plus Pakome wamejitahidi sana hichi kipindi cha kwanza.Kipindi cha pili inabidi tukaze zaidi kama tunataka kupata matokeo.
Wametoka kuifunga mashujaa 6-0 wakaenda kufungwa 2-0 na Al Ahly. Wameshagawa utamu tena kwa Far rabat sasa angalia siku wakija kucheza Mtibwa. Yanga 6-Mtibwa 1

Hii ndiyo timu wanayoisifia wanayanga? huyo mashujaa alijifunza nini?
 
Kocha Concalves hatoshi. Sijui yanga walimuokota wapi. Hana tofauti na yule mfaransa waliyemfukuza.
 
Back
Top Bottom