FT: Gaborone United 1-1 Young Africans SC | CAFCL-1st Leg | Botswana National Stadium | 05-09-2026

Ligi yetu bado sana kuvisaidia hivi vilabu vya Simba na Yanga kuwa competitive kimataifa, zinazifanya kuwa timu kubwa na za kutisha zikiwa zinacheza ligi za ndani ila huko international ndiyo tunaona panapovuja

Anyway hongera kwa kupata sare ugenini
Timu inayocheza mbinu ya low block kuifunga inatakiwa ufanye kazi ya ziada haswa. Timu nyingi pamoja na ubora wao huwa zina angaika kuzifunga timu inayocheza low block. Binafsi bado najipa muda, ila ukuta wa Bacca na Mwamnyeto naona wana makosa binafsi mengi sana.
 
Yaani! Niwe mkweli Mtani lile pira la Timu ya Wananchi jana hata sijalielewa.

Mmekumiss.
We ndo shabiki wa kweli. Nimekukosa (nimekumiss) pia.
Bila Ticha Jana mlikuwa mnalala na ndala.
 
Duuh kazi ipo Mwamnyeto sio wa kumwamini sana ndie anaemaliza harafu Bacca akipanda mtihani akirudi kukaba kwa kasi anasababisha faulo maeneo ya hatari.
 
Hakika. Na wale majamaa sio wepesi hata wakija hapa Tanzania si ajabu wakatusumbua pia.

Mie nipo.
Wa kawaida mno. Nadhani mabadiliko ya hali ya hewa yaliwaathiri wachezaji. Wakija Dar ndio tutajua ubora wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…