FT: Madeama 1-1 Yanga | CAFCL | Baba Yara Sport Stadium | 08.12.2023

FT: Madeama 1-1 Yanga | CAFCL | Baba Yara Sport Stadium | 08.12.2023

Nikiwa kama mpenda mpira na sio shabiki maandazi wa mpira, Huwa napenda kuwa realistic na Huwa siweki chuki Wala mahaba.

Yanga mpaka sasa hivi amecheza mechi 3 amekusanya points 2, kabakiza mechi 2 za nyumbani na moja ya ugenini.

Kumbuka huko ugenini anaenda kucheza na National Al Ahly timu Bora ya Karne, hapa nyumbani anacheza na CRB ambayo tayari kila mtu kaona kiuwezo ni Bora kuliko Yanga na game nyingine ambayo angalau Kuna uwezakano mkubwa wa ushindi ni ya hawa washamba wa aliyocheza nao Leo.

Sasa kimahesabu tu hapo na uhalisia, hapo Yanga atapata points 3 nyumbani dhidi ya hawa Maema sijui madeama.. game dhidi ya CRB uwezakano mkubwa ni droo tu pale game ya Ahly hata kupata droo tu utakuwa ni mtihani mzito.

Hivyo Kuna possibility kubwa ya kukusanya points zisizozidi 6 ambazo kismingi hazitatosha kumpeleka hatua inayofuata. Sio chuki Wala Nini Bali ni maoni yangu binafsi
Unaongea huku roho inakuuma kwasababu unajua kabisa hao CRB wanafungika vizuri tu.
 
Ila Yanga Ipunguze Mbwembwe wakiwa kwenye Box.
Wakiangalia marudio ya hii mechi wanaweza kujifunza kitu.

Kibabage ni mdhaifu sana kwenye kufanya maamuzi.
 
Hatimaye hesabu za uto kucheza robo fainali cafcl zimetiki.

Mkakati uliopo sasa ni kumfunga Al ahly nyumbani mchezo unaofuata, ili tuongoze kundi.

Tukijumlisha na pointi sita za nyumbani za crb na madeama, tayari tumeingia robo fainali.

Tabu ipo kwa watani zetu, kolowizadi. Maana kesho kwa wydad ac wanapigwa mkono, wakija kwa gàlaxy na asec na wydad tena wanakufa. Wana kazi
 
Back
Top Bottom