FT: Mamelodi Sundowns 0-0 Yanga SC | CAF CL Quarter Final | Leg 2 | Loftus Versfeld Stadium | 05/04/2024 (Penat 3-2)

Mtani eeh, Semi final ilikua yenu na mliipambania kwa halali, ila wenye maamuzi wameamua kuwakata.

Tujipange mwakani.
Nawaza tu Mamelody Sundowns ndiyo mbeleko kiasi hiki, je Al Ahaly SC vs Simba SC itakuwaje sasa (wenye kombe lao)?
 
Nawaza tu Mamelody Sundowns ndiyo mbeleko kiasi hiki, je Al Ahaly SC vs Simba SC itakuwaje sasa (wenye kombe lao)?
Kwa Al Ahyl inaweza kuwa nafuu kwa sababu anachotafuta Al Ahly ni Ubingwa tu CL ambao keshauchukua sana lakini Mamelodi wanachotafuta ni zaidi ya Ubingwa wa CL bali nafasi ya kucheza Kombe la Dunia la Vilabu.
 
ngapi ngap uko Cairo 😂
 
Nilitaka kuona Yanga inafungwa kwa fair play sio hizi drama za kitoto ambazo tunaziona hapa.
Unakuwaga objective sana mkuu, binafsi nakukubali sana unavokomentiga
 
Unazungumzia shirikisho ya mwaka gani?
Ina maana umeshasahau au umeamua tu kujizima data? Sikumbuki mwaka lakini nakumbuka uzembe ambao tuliufanya na Gwaneng Galax ambae tulimpiga 2-0 kwao halafu kwa Mkapa akatupiga 3-1, kwahiyo tukaaga Champions tukenda Confederation ambayo tulitolewa Robo kwa matuta nadhani na Kaizer Chiefs au Orlando Pirates. Ni juzikati tu hapa, kama sio 2021/2022 basi 2022/2023
 
Wewe huko buza huko ndo umeona goal.ila walioko uwanjani hawajaona goal ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…