FT: Mamelodi Sundowns 0-0 Yanga SC | CAF CL Quarter Final | Leg 2 | Loftus Versfeld Stadium | 05/04/2024 (Penat 3-2)

FT: Mamelodi Sundowns 0-0 Yanga SC | CAF CL Quarter Final | Leg 2 | Loftus Versfeld Stadium | 05/04/2024 (Penat 3-2)

1000045110.jpg
 
Kulikuwa na maana gani aucho, pacome kwenda South Africa? Na mnawapost kabisa wakiwa mazoezini...mwisho wa siku mnaleta kikosi cha kina gwede gwede
 
Hiii ni master piece,gamond ni bonge la kocha...huyu mu Argentina anatoa Radha zote yaani musonda atatutanguliza wananchi,guede atafanya mabeki wasipande then goli la pili max nzegeli anatupia tunafungua hesabu
 
Kocha Garmond anatuhujumu hivi hivi! Mchezaji wake Guede mpaka sasa haendani kabisa na mfumo wa uchezaji wa Yanga!! Yaani hana tofauti na mtangulizi wake Hafiz Konkoni!

Kitendo cha kumuanzisha kwenye hii mechi kitasababisha timu kuelemewa wakati wote! Maana siyo mkabaji! Hana kasi ya uchezaji awapo uwanjani! Muda mwingi anasubiri aletewe mpira!!

Bora hata angeanza Mzize anayekosa magoli ya wazi, huku akijituma na kuwasumbua mabeki! Dah!! Hii ni kamari ya hatari sana kocha ameamua kuicheza.


Naahidi kumuomba huyu Guede msamaha hapa jukwaani baadaye, iwapo ataonesha maajabu kwenye hii mechi. Ila kiukweli ataisababisha timu kucheza pungufu kwa muda mwingi kutokana na aina yake ya uchezaji.
Bado sijaona kama anastahili lawama. Ngoja tuone
 
Gamond leo sijamuelewa ina maana Aucho na Pacome hawajapona sasa mazoezi walikuwa wanafanya ya nini...🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Kulikuwa na maana gani aucho, pacome kwenda South Africa? Na mnawapost kabisa wakiwa mazoezini
Acha alinde vipaji vyao. Report ya Daktari ndiyo inapelekea kocha kuwapumzisha.
Tukienda nusu fainali mtamshukuru kocha.
 
Huwa nikiangalia mechi ya yanga huwa nafuata burudani na vipaji. Sasa hiki kikosi butu mshkj wangu Pacome hayumo ni naangalia mtu anayejitetea huku akipigwa.

Ngoja nisubiri Simba yangu, labda itafanya kakitu.
 
Back
Top Bottom