Kwa akili yako hicho ndicho kikosi tegemeo cha simba?
Una uhakika kwamba simba ingekuwa mechi ya ushindani wangecheza na hicho kikosi?
Panga sasa Kikosi Kwa Hali Ya Sasa Nani Angecheza Mechi ya Ushindani usiwe unaongea tuuuu.
Mimi ni Mwana Simba Kijana nilie na Card Ya Uanachama Nakwambia kitu nacho Kifahamu. Hao ndio wachezaji tulio kuwa tunaelekea nao na Tunaenda Nao Kimataifa. Watafanyiwa Sub either kuanza au kuingia Baadae. Kikosi Kipana kiko wapi.
Usiwe Shabiki wa Simba Kuwa Mpenzi wa Simba Ili unielewe ninacho kwambia kuwa Simba Hatupo Tayari Kimataifa Kama Hatutafanya Vitu vya haraka na msingi katika Benchi.
Manula ndio yule ambaye anafungwa magoli yale Yale, Kanoute Mechi Ngumu huwa Anakuwa Mzigo tunabaki kumtegemea Mkude ambaye Leo ndio Hovyo. Okrah wa Mikimbia Majeruhi yamemuandama kwa sababu hatuna Fitness kama Ya Yule Kocha wa Viungo Tulie Muacha Na Da Rossa, Una Phiri Majeruhi, Una Bocco, Una Baleke hana fitness una mtegemea nani Ku score? Una Saido Ambaye Mechi Kadhaa Zimeonesha Akiwa na Mechi ngumu Anakuwaje? Usiseme kama Shabiki wa Mpira sema Kama Mpenzi wa Mpira
Simba Tunahitaji Reformation Kubwa ya Kikosi na Benchi la Ufundi hata tuwe na Makocha 100 hiki sio Kikosi cha Kupambana na Lile Kundi Letu na Kusema Kwa Mkapa hatoki Mtu.
Unahisi Wachezaji ni Hussein, Kapombe na Chama? Umeangalia Ratiba Yetu ilivyo Ngumu? Chama Akikutana na Kiungo wa Shoka Anampoteza pale Kati na Hatuna Mwingine wa Kubadirisha Mpira. Hii mechi inatuonesha Ni kiasi gani hatuko tayari na CAFCL