Wananchi tumejitafuta na tumejipata, leo kazi inaanza, kocha Ramo ameona shida yetu ni fitness na stamina ya wachezaji wetu kushindwa kucheza dkk 90, basi baada ya kumaliza gym tu mbio za beach za masaa mawili kwa siku mwezi mzima ziwahusu wachezaji wote hata wasio first eleven!!
Kukosa fitness na stamina pia ni tatizo la wachezaji wa taifa stars, maana huwa tunafungwa na DRC kuanzia dkk ya 60 onwards. Huo ni muda ambao fitness, umakini, kukaba, kukimbia, stamina morali na nishati ya wachezaji wa taifa stars vinakuwa vimekwisha kabisa, timu inakuwa mdebwedo, tia maji tia maji mashabiki tunaomba mpira uishe, roho mkononi, kocha Morocco fundi sana ushauri wangu, wiki mbili nzima kabla ya ya Afcon peleka Coco beach vijana wako wakakimbie kwenye mchanga masaa matatu daily maana boli wanajua tatizo lao ni pumzi ya chips mayai na shisha!
All the best wananchi leo