Kuna timu siyo za kuziwekea dhamana mfano mmojawapo ni Ghana na Tanzania. Ghana juzi alikuwa anaongoza lakini sikutaka hata kucheki mpira wao nilijua watazingua tu, nikasema niwaangalie Misri maana ni watu wanaojitambua. Sikujutia uamuzi wangu, wote mliona kwa mafarao haiishi mpaka iishe.
Hivi wachezaji wa Tanzania wanajisikiaje wakiangalia wenzao wanavyopambania nchi zao? Kuzidiwa uzoefu au kipaji siyo inshu, onyesha kweli unautaka ushindi tutakuelewa hata ukibamizwa za kutosha. Kwenye mpira juhudi ni jambo la wazi halifichiki.