FT: Tanzania 0 - 0 DR congo | AFCON 2024 | Amadou Gon Coulibaly | 24 .01 .2024

Haya matokeo yanaonyesha tabia ya watanzania wengi. Yaani hata hivyo tumejitahidi. Hili neno linatuathili sana.

Tunatakiwa kukomaa sio kujitahidi.
 
Tanzania hatuna kabisa uwezo wa kutengeneza winga na washambuliaji, hili ni tatizo kubwa, na ni kwasababu washambuliaji wengi na mawinga kwenye ligi yetu ni wageni.... Ila kwenye viungo na mabeki tupo vizuri, tatizo linaanzia hapa...
Tatizo kubwa naloliona kwa timu yetu ya Taifa ni wachezaji kujisahau

Hili jambo nimekuwa nikiliona linafanyika sana Simba lakini nimekuja kugundua kuwa ni nature ya watanzania

Timu ikishapata goli basi hapo ndip mwanzo wa show game, husling zinapungua ma masihara yanashika hatamu.

Kingine ni kutojiamini.

Haiwezekani katikati ya uwanja unashusha back pass ndefu hadi kwa kipa, hiyo ndio inayotufanya tuone tunamiliki mpira kwa asilimia kubwa kuliko mpinzani, wakati umiliki wenyewe tunaufanya tukiwa kwenye eneo letu.
 
Yaani unakuta kabisa huu mpira ni wa kwenda mbele, mtu anarudisha nyuma, shida hii ya kujua kucheza mpira ukubwani.. ukigeuka umegeuka ukirudi umepiga kiatu na mpira unao ww na unasababisha mpira wa adhabu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kuna mtu hii pesa atailipiaa, atake asitakee.
Pesa yangu huwa haipotei buree, na uzuri Ali bett yeye, mie pesa nlimpa, ko atairudisha km ilivyo.
Naomba tu azime simu mbona ghetto litakuwa chungu
 
Next time Tanzania tupeleke Wanajeshi wa JWTZ wenye Uchungu tukuka na Uzalendo ili waipiganie na waipambanie nchi.
 
Mechi ya Zambia ndiyo ilikuwa inatubeba tukashindwa kulinda wala kuongeza goli.

Uchezaji na matokeo ya leo yangekuwa na tija kama kikosi kingekuwa serious mechi ya Zambia.
Kwani hii ya DRC tumefaulu Kwa lipi? Nimegundua kitu Kimoja Waswahili wakisikia watu wanacheza Ulaya au kuona ngozi nyeupe mavi yanaginga chupi wanaahindwa kujiamini.

Hiyo Zambia mliyoikomalia ni Kwa vile wachezaji wao wengi wanacheza timu za Afrika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…