FT: Tanzania 0 - 3 Morocco | AFCON 2024 | San Pedro, Ivory Coast | 17.01.2024
Isitoshe ni aibu kwa Morocco kuwa 1-0 up hadi sasa tuna bahati sana.

Half-Time analysis

Taifa Stars wapo disjointed na hawana viungo imara wenye kusaidia mashambulizi hivyo tutaendelea kucheza mchezo uleule wa kipindi cha kwanza.

Morocco wana timu yenye wachezaji wenye kuunganisha mashambulizi, kutafuta vyumba na akina Ziyech kuwa na nafasi za kufunga au kusababisha magoli.

Lakini Morocco wana dharau sana wamekodi hoteli yao peke yao mbali na kambi nzima ya timu zote za kwenye kundi.

Morocco ni timu iliyopo kwenye nafasi ya 22 kwenye world ranking, Tanzania ni ya 131!

Kwenye bara la Afrika CAF ranking Morocco ni ya 2 na Tanzania ni ya 36.

Tungojee kipindi cha pili chaja.
Hapa kwangu mimi tatizo linakuja kwamba timu haina straika

Sisi kama watanzania tunakosa watu wabunifu pale mbele

Angalia pacome,chama,aziz ki, yule jamaa anachomekeaga yule wote ni 10 esque players wanaovuma nchini

Watu hatuna 9 mwenye nguvu
Hatuna namba 10 wenye ubunifu
Timu imejaa wakata umeme na mabeki kibao ambao hawatumii akili kubwa
Mwisho wa siku tunajitahidi kulinda ila kushambulia hamna kitu

Na bila magoli hamna ushindi
 
Sasa mtu mnalaumu kocha

Timu nzima mchezaji ni samaatta na Novatus dismas

Wengine woote hamna kitu

Morocco wana mtu anaanza PSG, wana mtuu anaanza Sevilla, wana mtu anakuwa kwenye rotation man united
Wana mtu anaanza bayer munich

Mnataka nini watanzania

Kwangu mimi wakifungwa chini ya 2 goals wamejitahidi

Mnataka mchange history na nan? Haji mnoga?[emoji23][emoji23][emoji23] acheni utani waheshimuni morocco
Wewe ni mpumbavu Sana misri alinusurika chupuchupu licha ya kucheza na msumbiji ambae Nina uhakika hujui hata mchezaji wake mmoja.


Mapumbavu kama wewe ndio mzigo Kwa taifa hili
 
Morocco apige cha pili watu tumalizane na mhindi. Kimasiala tu unashangaa yanatokea mambo ya algeria na egypt.
 
niilivyooona list nkasema mbele kunamabomu ya machozi hakuna jipya
Mmh yajayoo yanafurahisha
 
Jinsi TANESCO walivyokata umeme na Jinsi Taifa Stars inavyotembezewa kipigo nafarijika sana. Tanesco kamatieni hapo hapo hadi game iishe
 
Back
Top Bottom