Gucci gang
JF-Expert Member
- Jan 7, 2018
- 2,682
- 5,277
Hapa kwangu mimi tatizo linakuja kwamba timu haina straikaIsitoshe ni aibu kwa Morocco kuwa 1-0 up hadi sasa tuna bahati sana.
Half-Time analysis
Taifa Stars wapo disjointed na hawana viungo imara wenye kusaidia mashambulizi hivyo tutaendelea kucheza mchezo uleule wa kipindi cha kwanza.
Morocco wana timu yenye wachezaji wenye kuunganisha mashambulizi, kutafuta vyumba na akina Ziyech kuwa na nafasi za kufunga au kusababisha magoli.
Lakini Morocco wana dharau sana wamekodi hoteli yao peke yao mbali na kambi nzima ya timu zote za kwenye kundi.
Morocco ni timu iliyopo kwenye nafasi ya 22 kwenye world ranking, Tanzania ni ya 131!
Kwenye bara la Afrika CAF ranking Morocco ni ya 2 na Tanzania ni ya 36.
Tungojee kipindi cha pili chaja.
Sisi kama watanzania tunakosa watu wabunifu pale mbele
Angalia pacome,chama,aziz ki, yule jamaa anachomekeaga yule wote ni 10 esque players wanaovuma nchini
Watu hatuna 9 mwenye nguvu
Hatuna namba 10 wenye ubunifu
Timu imejaa wakata umeme na mabeki kibao ambao hawatumii akili kubwa
Mwisho wa siku tunajitahidi kulinda ila kushambulia hamna kitu
Na bila magoli hamna ushindi