FT: Tanzania 0 - 3 Morocco | AFCON 2024 | San Pedro, Ivory Coast | 17.01.2024
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] huyu lazima niruke nae, huenda ndo ikawa ticket ya kutokaa bongo, unashangaa ananibebaaa mambelee
Uduguu fursaa kuifataaa, haijiletiiiiii mweeeeh
Kwahiyo daladala za gomz unatuachia wenyewe 🤣🤣
 
Sasa kama ni kweli.
Na ujue bongo kwa watu kama samata, msuva namba ni uhakika
Sasa namba uhakika hilo sii jukumu lake kocha kuona kuwa huyu hanifai. Its all down to selection...kama anapangiwa nani aje kikosi cha timu ya taifa basi hamna haya ya kuwa nae bora tuwe na mzawa tuu
 
Kama jina Taifa Stars halitishi wapinzani walau basi tuwe na wachezaji wanaoweza kuwatisha wapinzani.

Bahati mbaya hatuna vyote bora tuende na jina la Kichwa Cha Mwendawazimu.
 

Mpira ni maandalizi ya muda mrefu, kuandaa wachezaji kimwili na kiakili. Hamasa ni baada ya maandalizi mazuri.

Ligi yetu inabebwa kwa asilimia 90 na wachezaji wa nje. Morocco ni timu bora sana kwetu, lakini wachezaji wetu bado sana.
 
Hiki ni kilio chetu..!

Tunawaomba Sana, Mechi Ijayo Kama inawezekana mtubadilishie Wale Mabeki...!
Ushabiki wetu Wa Yanga na Simba ubakie huku huku NBC...!
 
Nilifikiri ungetoa hoja, kumbe unakimbilia jinsia, poleee wee
Mpira ni mchezo wa wazi na haujifichii, punguza mahaba.

Wachezaji wa ndani leo hakuna kitu, hasa mabekii.
Kwahiyo tatizo ni mabeki ndio waliochangia usipigwe mpira wowote uliolenga lango?
 
Yaani Taifa stars ishinde dhidi ya Timu ambayo ilicheza robo fainali kombe la Dunia na ikaibuka kidedea mbele ya Portugal yenye wachezaji mahiri kama Cr7,Jota,Bruno Fernandes na wenzie wengi ambao wametoka vilabu vya uingereza!

Hivi watz huwa mnawaza kupitia akili za wapi?
Mpira siyo janjajanja..
Tz tunachoweza ni kupiga mdomo tu,mpira bado hatuuwezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli moroco ni timu bora lakini tumeona timu nyingine bora kwenye maahindano haya zikiambulia sare au kufungwa . Kila timu imejiandaa vyema
 
Back
Top Bottom