FT: Tanzania 1-1 Zambia | AFCON 2024| Laurent Pokou Stadium | 21.01.2024

Hivi hizi threads za michezo kuanzisha usiku wa manane ndio nini?

Nimemiss kipindi threads zinaanzishwa karibia na muda wa mechi, homa iko juu tunachangia kwa mihemuko & mchecheto.

Hizi za mapema hadi kufika muda wa mechi tumeshachoka!
Wanashindana wawe kwanza kuanzisha uzi.
 
Labda Zambia wasawazishe au wafunge 2 ndiyo atatolewa .
Makocha wetu wanafundisha kimazoea sio kimbinu.
Game ishakuwa ngumu sana kwa Zambia
 
Kama mchezaji wa Zambia kapewa red kwa ile faulo, halafu kwenye VAR wanasema touch ya mwisho aligusa Kibu na wameshindwa kuipa Tanzania foul kick wala kona, ile kadi inakuwaje?
Kadi nyekundu alistahili

Kwa sisi ambao tunatazama huu mpira kupitia beIN sports tumesikia kishindo cha kile kipepsi kilivyotua kwenye kifua cha Samatta

Ilikuwa ni fair kabisa hata hivyo Samatta nadhani alijikaza tu ile ningepigwa mimi nisingesubiri filimbi ningeibuka na jiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…