FT: US Monastir 2-0 Yanga SC || CAFCC || Rades, Tunis || 12-02-2023

FT: US Monastir 2-0 Yanga SC || CAFCC || Rades, Tunis || 12-02-2023

Utopolo wanajitahidi kuvuka lakini ukweli hawatoboi
JamiiForums757910739.jpg
 

[emoji460]️ US Monastir[emoji739]Young Africans SC
[emoji1001] 12 February 2023
[emoji935] 11:00 Jioni TUN | 01:00 Usiku TZ
[emoji909] Uwanja wa Rades, Tunis
[emoji471] CAFCC

Kikosi cha Yanga

Usiku wa deni haukawii. Hatuondoki hapa mpaka usiku mnene tukifurahi ushindi

Timu zinaingia uwanjani
Mchezo umeanza
2' Yanga wameanza kwa kasi, Kisinda anapata nafasi ya kukimbia na mpira
10' GOOOOOOOOOOOOOO Yanga wanafungwa goli la kwanza
Mohamed Saghraoui anawatanguliza wenyeji kwa bao la mapema
16' GOOOOOOOOOOOOOOO, Yanga wameruhusu magoli mawili ndani ya dakika 16
Boubacar Traore anafunga goli la pili kwa kichwa
30' Yanga wanaonesha utulivu na kumiliki mpira
35' Wenyeji ni hatari wanapokaribia lango, wanafanya mashambulizi makali
43' Yanga wanapata faulo karibu na lango la wapinzani, shuti linapigwa linapaa juu

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza
47’ Mayele anapiga shuti kali kipa anapangua kwa mguu
50’ Yanga wameanza vizuri, wanamiliki mpira na kupiga pasi nyingi
57’ Moloko anachezea faulo karibu na lango la US Monastir
58’ Shuti la Azizi Ki linambabatiza kipa na kurejea uwanjani
62’ Yanga wanaendelea kujipanga wakitengeneza nafasi kadhaa
62’ Lomalisa anaingia, ametoka Kibwana
75' Yanga wanafanya mabadiliko
Anatoka Moloko anaingia Frid Mussa, anatoka Aucho anaingia Mudathiri Yahaya
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mlianza kupenda timu kabla ya kupenda mpira kwanza ndio shida ya wengi wenu.

Football ni mchezo wa makosa, ulifanya makosa unaadhibiwa, hapo hakuna John Bocco wakisema ufanye makosa na bado anashindwa kufunga, hao Waarabu wamewekeza kwenye mpira, sisi ndio tunaanza.

Hakuna mafanikio ya haraka, hata Simba amekula sana hamsa hamsa mpaka zikampa uzoefu wa hii michuano.

Vipers siyo timu mbovu iliyokalishwa na Raja, Mwarabu ukianza mechi kwake hafanyi makosa.

Tell them....
Viva dar young Africa
 
Back
Top Bottom