FT: Vipers S.C 0-1 Simba S.C | CAF Champions League | St. Mary's Stadium | 25.02.2023

FT: Vipers S.C 0-1 Simba S.C | CAF Champions League | St. Mary's Stadium | 25.02.2023

Nakazia... hii ndiyo Vipers iliioifunga Utopolo na TP Mazembe.
JamiiForums229484241.jpg
 
#Uchambuzi wangu baada ya match ya simba na vipers#

Simba imeshinda ila mpira haukuwa mzuri kabisa bado kuna simtofahamu baina ya wachezaji ni kama hawataki kucheza mfumo mpya wa coach Alberto.

Pili aina ya mpira waliocheza vipers ndio mpira naona simba inajaribu kucheza maana yake ni kuwa kocha Alberto anatuletea mpira wa vipers ndio uwe aina ya mpira wa simba tukumbuke vipers imefundishwa na Alberto kwa zaidi ya match 58 kifupi ni kuwa aina ya mchezo wanaocheza vipers ni matokeo ya kocha Alberto sasa kwa simba iliyokuwa na aina nzuri ya mpira kuanza tena kubadili mfumo tena mfumo wenyewe ni kama wa vipers mimi binafsi sioni feature ya Simba kama itaendelea na aina hii ya mpira hata wachezaji ni km hawataki aina hii ya mfumo wa huyu kocha.

Ushauri wangu.
Makosa yameshafanyika kwa kumleta kocha ambaye haendani na falsafa ya mpira wa simba kabisa..

Uongozi ufanye maamuzi ya haraka kuokoa jahazi au la basi tusubili msimu uishe kocha afanyiwe usajili wa wachezaji wapya ambao itakuwa rahisi kuiga mfumo wake.

Ila cha kujiuliza ilikuwaje screening ya simba kumselect kocha ambaye historia yake ya mpira sio kubwa kama simba yaani tumeenda kuchukua kocha wa vipers ambayo ndio mara ya kwanza kuingia kwenye makundi klabu bigwa huku sisi tukiwa ni wazoefu wa hadi robo fainali kwa zaidi ya mara mbili.
#Simba nguvu moja#
 
Back
Top Bottom