FT: Wydad Casablanca 1-0 (Penati 4-3) Simba S.C | CAF Champions League | Simba yaondolewa kwa mikwaju ya penati

FT: Wydad Casablanca 1-0 (Penati 4-3) Simba S.C | CAF Champions League | Simba yaondolewa kwa mikwaju ya penati

Wanathiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiimbaaaaaaa[emoji350][emoji350]
Hayawi hayawi Sasa yamekuwa, Ile siku iliyosubiliwa Kwa hamu na waarabu wote hatimaye imefika..
Ni siku ya hukumu kwa mnyama Simba
Ni siku ambayo taifa la Tanzania linaenda kupata aibu kwa kipigo kizito watakachoenda kushushiwa Simba na waarabu wa Morocco.

Mwana kulitafuta mwana kulipewa, mtoto akililia wembe mwache umkate,
wameingia cha kike eeh waaah!!!

Kuwa nami mwarabu feki upate kile kitakachojiri pale katika Dimba la Mohamed V (machinjioni) Jijini Casablanca...

Mechi hii ya kukata na shoka itaanza majira ya saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika mashariki na itarushwa na Azam Sports kupitia Channel ya ZBC2

Kaa nami mwanzo Mwisho......

Rest in peace Simba[emoji3545]
Timu zote tayari zimeshaingia uwanjani kupasha misuli tayari Kwa mpambano huu wa Leo [emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]

00" Mpira umeanza hapa katika uwanja wa Mohamed V Wydad ndio wamekuwa wa kwanza kugusa Mpira ule

03" Wydad wameanza kusaka bao la mapema

06" Simba wanapata kona ya kwanza ya mchezo ila haikuzaa bao

13" Milango bado migumu kwa pande zote mbili

20" mashambulizi yanaongezeka kuelekea lango la Simba, ila golikipa Ally Salum anakaa vema na kuondoa hatari ile

24" Goooooooo Wydad wanapata goli la kwanza

30" Simba inapataa faulo eneo zuri lakini mpira unaokolewa na kuwa ni wa kurusha kuelekea lango la Simba

45"+1 Imeongezwa Dak 1 ya nyongeza hapa
Mpira ni mapumziko Wydad wanaongoza Kwa goli moja

Kipindi cha pili kimeanza

46" wanaanzisha mashambulizi kupeleka lango la wydad

49" Wydad wanafanya shambukizi Kali lakini mpira unaenda nje

60" mashambulizi ni makali sana langoni mwa Simba ila Bado wameshikilia bomba

View attachment 2602892View attachment 2602894
Dalili zote zinaonesha Simba anamchomoa bingwa mtetezi kwa matutq. Hawa Wydad wameishakubali.
 
😂😂
Jirani yangu hapa kuna mtu kanywa vitu vyake huko, kila saa anamuulizia Manula, anaambiwa goalkeeper leo siyo Manula, anasahau tena..!

anarudi 'unajua leo kama ni matuta Manula hawezi', anaambiwa tena, Manula ni majeruhi hayupo, anaelewa kwa muda, kisha anauliza tena, kwani Manula ana shida gani..??😂😂

Niko hapa nasikia kulia kwa uchungu..!😂
Yan kwa ujumla leo simba wamevurugwa ukichanganya na wewe😆😆😆
Sio jirani yako, wala wewe, wala ndugu zake onyango
Sipati picha wangekua na hata kagoal kamoja hiko kiherehere chao😆😆😆
Pole sana dada angu
 
Kilichobakia Hawa Waarabii Wanafanya Kila Kitu Yaani.
 
Hawa waarab pamoja na kudominate mpira ila hawatengenezi nafasi kabisa.Sasa hivi wancheza na refa.

Vp leo mmejiandaa kwa matuta.......?
Duuuh hapo kwenye matuta sasa ndo penye shida,mlango ungefunguka tupate goli ingekua njema sana.
 
Saidoo anatakiwa apumzike hizi dakika za mwisho aingie Phiri au Shako.

Baadae Chama atoke (hana impact yoyote leo) aingie Nyoni, hii game ilipofikia Nyoni anacheza vizuri tu kuliko kumtegemea Chama ambae hana lolote leo.
Atasaidia Sana kwenye penati Kama matokeo yakibaki hivi.

Maana hatuna wapigaji penati kabisa
 
Saidoo anatakiwa apumzike hizi dakika za mwisho aingie Phiri au Shako.

Baadae Chama atoke (hana impact yoyote leo) aingie Nyoni, hii game ilipofikia Nyoni anacheza vizuri tu kuliko kumtegemea Chama ambae hana lolote leo.
Unakumbuka alichofanya Sakho kwenye first leg?

Phiri ni risk, hana game fitness

Nyoni naye ni mchezaji wa msimu, huwenda akiingia atacheza vizuri lakini pia akavuruga kabisa mchezo wenyewe kwa poor performance

Ni kweli Chama amekuwa akicheza chini ya ubora wake tuliozoea ila hiyo ni kutokana na kadi ambayo anayo.

Hofu ya kupigwa kadi nyekundu ndio inamfanya ashindwe kukaba vyema
 
Saidoo anatakiwa apumzike hizi dakika za mwisho aingie Phiri au Shako.

Baadae Chama atoke (hana impact yoyote leo) aingie Nyoni, hii game ilipofikia Nyoni anacheza vizuri tu kuliko kumtegemea Chama ambae hana lolote leo.
Wanategemewa kwenye matuta hao
 
Back
Top Bottom