FT: Yanga 0-1 Azam | VPL | Benjamin Mkapa | April 25, 2021

FT: Yanga 0-1 Azam | VPL | Benjamin Mkapa | April 25, 2021

Dah! Timu yangu leo imekufa kabisa kwenye eneo la kiungo! Haka Katoto ka Angola kanacheza kibishoo bishoo tu! Hakawezi hata kukaba! Kanategemea kuchukua ujiko kwenye mipira ya adhabu na kona tu.

Kiufupi hatuna kiungo namba 8! Fei Toto sijui yuko wapi! Bora hata wangemuingiza mkongwe Niyonzima. Tukishinda mechi hii basi itakua ni bahati nasibu tu. Hapa kuna sare au kufungwa kagoli kamoja!
Utabiri umetimia! Ubingwa ni wa Simba, kwa mwaka wa nne mfululizo. Wanastahili. Yanga ina matatizo. Kuanzia wachezaji, benchi la ufundi na viongozi.

Ni wakati sasa kwa Viongozi kuharakisha mchakato wa kuibadili timu kutoka kwenye mfumo huu wa sasa. Wachezaji wengi walio sajiliwa ni wa kiwango cha kawaida sana ukilinganisha na usajili wa Simba.
 
Back
Top Bottom