FT: Yanga 2-1 Simba | Yanga yatwaa Ngao ya Jamii

FT: Yanga 2-1 Simba | Yanga yatwaa Ngao ya Jamii

Ushauri wangu kwa watu wa Simba mjifunze kupunguza kelele, mnaboa sana.

Game ya leo sikutaka kuangalia nyumbani nikajichanganya mtaani kuangalia game, kwakweli watu wa Simba hawana ustaarabu halafu wanajiamini kwa timu ambayo tukiweka ushabiki pembeni haina quality kama Yanga.

Pili mpira ni mpaka refa amalize mechi, watu wa Simba wengi hawalijuhi hili.

Niliokuwa naangalia nao mechi niliwaambia ogopa Yanga akitangulia kukufunga hurudishi, Ila Yanga ukiwapiga wanarudisha na wataongeza, leo naonekana kama mnajimu wakati sina unajimu wowote fact ziko wazi.

Leo mji upo kimya wapiga kelele wanalala na viatu, watu wa Simba badilikeni.
Hawawezi kukuelewa mkuu wengi ni muhemko na hawapendi kufungua akili zao, ndiyo maana wanaanza kutatufa mchawi na very bad lucky viongozi wa simba wameingia kwenye huo mtego
 
Inaelekea unajiliwaza toka saa 3 usiku hadi saa hizi,,, 7 hours loh.Umeandika TANGA kapumzike kwanza.
 
Ngoja na Mimi nitoe maoni yangu.

Jana ilikuwa mechi ya mbinu zaidi kuliko uwezo wa wachezaji, maana yake ni kwamba uwezo wa wachezaji ulikuwa unacompliment mbinu za walimu. Hii inathibitishwa na vikosi ambapo walimu wote waliamua kuanza na wachezaji wengi waliokuwepo msimu uliopita na wapya wachache ili kuendelea momentum na uelewano ambao tayari umeshajengwa.

Sasa kama ambavyo imekuwa inasemwa hizi timu zote zina madhaifu kwenye kiungo Cha chini (Diffensive midfield) ambao wanaweza kusaidia mabeki wakati wanashambuliwa. Ndio maana hata goli la kwanza la Simba alilifunga Sakho lilitokana na kuchelewa Kwa safu ya kiungo kuzuia penetration ya mpira na mtu na kufanya Sakho apite katikati ya center backs wa Yanga ambao walikuwa flat wakati huo na kufunga goli zuri sana. Makosa haya waliendelea kuyafanya mara kadhaa ila tu Simba hawakuwa na mtu sahihi mbele ya goli la Yanga.

Kipindi Cha pili kocha wa Yanga Nabi alifanya mambo mawili kwanza alibadili wachezaji kadhaa halafu akafanya switch of play formation. Mwanzo alicheza na 4-3-3 lakini kipindi Cha pili akaja na 4-2-3-1. Mabadiliko haya yalilenga mambo 3.
  • Kutanua uwanja Kwa kuwatumia wide players
  • Hao wide players kwasababu ya Kasi kuwazuia full backs wa Simba wasipande, ndio maana ukaona sasa katikati wachezaji wa Simba wamepungua maana mwanzoni walikuwa wanakuwa wengi kwasababu Mohamed Hussein na Israel walikuwa wanasogea pale wanapaoverload kwahiyo wanawaoutnumber viungo wa Yanga.
  • kufungua eneo la kiungo la Simba ili kuruhusu mpira kutembea.

Nimeona watu wanalalamika Chama na Kanoute kutolewa, yes it was an avoidable changes kwanini? Chama anakuwa mchezaji mzuri timu ikiwa inacontrol midfield ili kumpa nafasi ya kufanya interchanges ya pass na wenzie. Lakini timu bila mpira Chama ni useless. Pili Kanoute alikuwa na yellow card tayari na style of pressing ya Kanoute na namna Yanga walivyoingia second half ilikuwa rahisi yeye kucommit foul ambayo ingeweza kuigharimu timu Kwa kupewa second yellow na hivyo kuwa nyekundu so ilikuwa lazima atoke.

Sasa walichofanya Yanga sasa ilikuwa kumrudisha Feisal kwenye base ya midfield na Aucho kama double pivot halafu Aziz Ki akawa play maker nyuma ya Mayele. Lakini kwenye transition wakiwa na mpira Yanga wakawa wanafanya kitu tofauti kidogo yaani wakichukua mpira kutoka Kwa Simba wanacheza Kwa Fei na Aucho ambao badala ya kupeleka Kwa Aziz Ki mbele yao wanapelwka Kwa Moloko au Morrison pembeni ili kuwafanya Simba watanuke. Defense ya Simba ikitanuka Moloko na Djuma wanapasiana halafu wanapitisha mpira Kwa Aziz Ki ambaye anakuwa na space katikati ambaye sasa analink na Mayele huku Moloko na Morrison nao wakiingia kuoverload eneo la defense ya Simba.

Sasa Aziz Ki anaoperate vizuri sana akicheza kama no 10 na ana passing accuracy ya Hali ya juu ndio maana utaona pass iliyozaa goli la kusawazisha ilivunja mistari 2 ya kiungo defense ya Simba imamkuta Mayele ambaye pia alikuwa na composure ya Hali ya juu akafunga.

Sasa baada ya hapo Simba wakawa kama wamekosa majibu ya namna ya kudeal na mbonu ya Yanga kwasababu mara kadhaa Yanga walitumia mbinu hizo hizo kufika langoni mwa Simba kama nafasi ya Mayele na Morrison zilivuotokea. Kwakuwa Bado sasa Simba katikati kulipwaya ndio maana sasa mpaka Job Kuna wakati akawa ana uwezo wa kudrive timu kutoka kwenye backline mpaka katikati na ndipo goli la 2 lilipopatikana. Job alicheza one two na midfield wake akapanda huku Fei akirudi kucover nafasi yake akapiga Ile penetration Kwa Mayele ambapo Mayele akatumia udhaifu wa defense ya Simba iliyokuwa flat na kufunga goli la pili.

My note: Simba na Yanga wote wanastfiggle na kuwa na typical number 6 hasa baada ya Yanga kumrudisha Bangala nyuma. Kanoute sio mchezaji wa kumtegemea Kwa dakika 90 maana aina yake ya uchezaji inamfanya kuwa kwenye Uzi mwembamba sana wa kupata kadi.

Simba hawana namba 5, central defenders wa Simba wote wanacheza kama namba 4. Yaani hakuna wa kumtuma mwenzie na yule wa kusawazisha makosa ya mwenzie.

Nadhani Nabi ni master ya kusoma mchezo na kuinflict mbinu zake against timu pinzani maana hata mechi ya jana ameshinda Kwa mbinu
 
Haya majamaa ni mambumbumbu kama Rage alivosema. Kuna watu humu baada ya mechi na wahabeshi waliandika madhaifu ya timu lao ila walitukanwa nakebehi juu. Ila sasa yanaongea yaleyale yaliyoambiwa yakaanza kutukana. Nini shida nyie mbumbumbu?
Nyie wenye akili timu nzima au yanga nzima wawili leo naona meno yote njeee
 
Alipomtoa chama ndipo mayele akasema yes mbabe wa dimba katoka, ngoja nikiwasheee.
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, kipindi cha pili kilipoanza ni Nabi pekee ndiye alitefanya mabadiliko ya kumtoa sureboy na Farid Musa na kumuingiza Morrison na Moloko. Kocha wa Simba alifanya Sub baada ya Yanga kusawazisha. Point yangu ni kwamba Mayele alianza kufunga kipindi Chama yupo.
 
Mimi kuongea sana kwa hiyo ndio nishakua shoga sasa sindio?

Kuna sababu nyingine nje na hapa ambayo mimi nilishawahi kukukosea au ni huu huu mpira tu?

Haya wacha nikuache na furaha yako uliyoipata baada ya ushindi japo lugha unayotumia kufurahia ushindi huo sio nzuri kwangu na hata kwa Yanga wenzako walio staarabika

Upo wewe na kuna huyu Matola nawe niliona ile post yako ya matusi nikaiacha tu

Ila mngekuwa mnajiuliza licha ya mimi kutotoa matusi kwanini hamnioni kutumia majina machafu kuwaita (kinyesi) kama ambavyo wengine wanawaita mngejifunza namna ya ku filter maneno.
Umejibu ki utu uzima, hongera kwa hili. Aidha, nikupe pole kwa kipigo cha jana.
 
Back
Top Bottom