Asingeweza kusimamia yeye Hizo pesa kwani Tayari zilishakuwa chini ya usimamizi wa BOT, kwenye mchakato wa kutoa hizo pesa ulihusika Mwanasheria mkuu, Hazina, TRA, Ikulu, TISS of-course na wizara yake, na kwenye Wizara yake muhongo sio mtendaji, mtendaji ni Katibu na ndiye aliyekuwa kwenye hayo mawasiliano
Kiukweli sijaona Mantiki ya Jina la Muhongo kuwemo kwenye hiyo report,
Huyu ni rais wa nchi.Ni muheshimiwa rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Hajiuzuru mtu hapa
Kweli mi huwaga nawashangaa waislam wana maisha duni sana, kumbe sisi ni mijizi ndo mana tuna afford kuishi maisha bora kuliko wenzetu!
Huku Mbezi na Mikocheni wagalatia tumepastawisha kumbe ni hela za wizi! Huu ni uonevu! Na aibu mno!
Ona Tiba ana shule nzuri eti ya Yatima huku anaifund na wizi wa fedha ya umma!
Kwa nini wakristo Rugemalila na cos wasingepeleka fedha hizo shule za Kata za Mbagala na Buguruni?
Ukimkuta na rozari kuubwa utadhani mnyororo wa kufungia Mbwa. Kumbe jizi tu!
Subiri, yote yanajibika na haondoki mtu.
Muhongo ametajwa kwa chuki za kisiasa zinazo chochewa na mkono na mengi kwa kukosa kitaru cha gesi.Hivi ni kweli huoni mantiki ya jina lake kutajwa?? Kweli we ni Kituko
Report ya PAC inasema wazi kuwa Waziri Mkuu Pinda alikuwa anajulishwa kila kitu kuanzia mwanzo hadi mwisho wa kuhamisha fedha za Escrow. Pia hela zilizohamishwa kutoka mkombozi zingine majina ya waliolipwa yamefichwa
"Mlitaka mpewe Umeme wa bure" Teh Teh hata wajukuu tunaona bibi Bomba ni kilaza wakutupwa
Nashangaa sana watu wanapenda vya bure pole yao."Mlitaka mpewe Umeme wa bure" Teh Teh hata wajukuu tunaona bibi Bomba ni kilaza wakutupwa
Na akome kiherehere chake ana dharau sana kwa Watanzania eti tunaweza kutengeneza juice tu alinikera Sana tena ajiuzulu uwaziri
Katibu anaweza akatoa go ahead bila idhini ya waziri,ukizingatia kwenye issue sensitive kama hiyo?cheo ni dhamana aondoke tu akafundishe,kwanza kwa mujibu wa sheria anatakiwa kustaafu,basi akajiajiri tu
Kwa watalamu kama muhongo amajibu yapo wazi kabisa.Naam, hakuna umeme wa bure.
Ile ripoti inajibika, wala sina shaka nayo.
Inawezekana hakutajwa lakini aliwajibika Kama msimamizi wa kazi za serikali. Na pinda nae awajibike.labda tujikumbushie report ya richmond ni wap lowasa alitajwa kaiba ........?
Nimesikia na kuona Majina mengi ya waliokula mlungula, lkn Sijaona Waziri Muhongo ameingiziwa ngapi ningependa kujua, kwa maana huyu ndio Ring leader mwenyewe akifwatiwa na Kikwete!
Genius yule. Embu ingia Facebook account yake uone aliandika nini tarehe 13 mwezi huu, ndio utajua huu mchongo kachonga nani. Lowassa hawezekaniki!
SOMA MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC INAYOSOMWA SASA BUNGENI. Zitto: Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe. Andrew Chenge (Mb) Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni 1.6. Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62 Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6. Zitto: Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4 Zitto: Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4. Zitto: Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga alipewa shilingi milioni 40.4 Zitto: Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7. Zitto: Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4 Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa shilingi milioni 40.4 Zitto: Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4 Zitto: Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8. Zitto: Viongozi wa Madhehebu ya Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63 Methodius Kilaini shilingi 80.9 Zitto: Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4. Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow Zitto: Bilioni 73.5 zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006 Zitto: Taarifa ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa. Zitto: Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha