Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Ndugu yangu, Tanzania ni shamba la bibi. Kila mtu anajiokotea na kuondoka zake. Huyo Mechamar anaweza kuja kudai na tukamlipa bila matatizo. Ni wao tu kuamua kuandaa mchoro mwingine na kuwahakikishia wakuu mgao wao basi. Hizi zilizokwisha toka ndio imetoka hivyo. Hairudi hata senti ng'o; hata ashuke malaika kuja kututetea.
 
spika makinda alisema wengine hapa mnapiga kelele nikiwaamsha hata hamjui cha kusema hili ni fumbo la imani kuna IPTL,PAP,MECHMAC, VIP,PIPELINE,SIMBA TRUST zote hizo ni wakala wa shetani

FUMBO la imani hahahahahaaaaa Nimeipenda sana
 
spika makinda alisema wengine hapa mnapiga kelele nikiwaamsha hata hamjui cha kusema hili ni fumbo la imani kuna IPTL,PAP,MECHMAC, VIP,PIPELINE,SIMBA TRUST zote hizo ni wakala wa shetani
Hapo kwenye Mechmac na Piperlink unamkuta na SCBHK, hili kweli ni fumbo la imani.
 
Ndugu yangu, Tanzania ni shamba la bibi. Kila mtu anajiokotea na kuondoka zake. Huyo Mechamar anaweza kuja kudai na tukamlipa bila matatizo. Ni wao tu kuamua kuandaa mchoro mwingine na kuwahakikishia wakuu mgao wao basi. Hizi zilizokwisha toka ndio imetoka hivyo. Hairudi hata senti ng'o; hata ashuke malaika kuja kututetea.

huu ni ukweli mchungu mchungu sana! unless Wahisani watusaidie lakini hapa tuko hatarini sana!
 
Mmiliki wa 70% ni Standard Chartered Bank Hong kong, na Tanzania lazima itakuja kumlipa.

huu nao ni ukweli mwingine mchungu sana! hizi pesa mafukara lazima tubebeshwe malipo yake! ndio maana naona wakoloni pekee ndio wanaweza kutusaidia bila hivyo tumezama!
 
ndip maana nashawishika kuamini kuwa huyu PIPER Link ndio huyu PAP aliyeingia kiwizi akijifanya kununua hisa za mwenzake VIP na ambaye anaweza kurudi tena kama PIPER link kukana kuuza mali yake na fedha zake akadai pia.
 
Naomba kuelimishwa vema. Je ile pesa ya escow, kama ingelipiwa kodi za aina yote yaani vat na income tax. Itaendelea kuwa ni pesa ya umma? Naomba kuelimishwa.

Je jinsi ilivyogawiwa na Lugemalila, kulikuwa na invoice? Fee Note? Au document yenye hadhi ya kimkataba kutoka kwa wale wote walionufaika nazo?

Je kwa pesa ilolipwa maaskofu . sadaka huwa na invoice au receipt?
 
Uliahidi kwenye kamati ya PAC kuwa utakamilisha uchunguzu kuhusu tuhuma za ufisadi mnamo tare 8, tunakukumbusha ahadi yako DR watanzania hatutaki tena siasa kwenye mambo ya msingi
 
Tulisikiliza Bunge maarufu.Bunge liliovuta hisia.Ukubwa wa Issue uliwameza sana watu na kujisahau kuwa walikuwa akitumika hapohapo na watu wasio aminika,watu wasio lala wakifikiri namna ya kufikia ktk matamanio,matamanio yanayowafanya waone wengine hawakustahili kuwa sehemu fulani ila wao tuu ndio waalistahili.Ktk hii njia hila nyingi sana zilitembea pale bungeni,na waaminifu walichezewa sana na wapuuzi.Kwa ujumla ilikuwa rahisi sana kuona jinsi TZ haina viongozi wengi sana,hata wakipimwa kwa parameter moja,na zikiongezeka hata 3 CCM hawatakuwa na candidate. 1.CCM walijaribu sana kujifanya wapo upande wa watenda,lengo ni kuteka hisia za watu na baadae kuteka Credits zote za walio upande wa mashujaa. 2.Makinda alikuwa akizunguka zuka akikataa PHRASE za watu ,akijifanya kutaka ushirikiano wa wapinzani.ILa alikuwa anazuga tuu ili pawe kuzuga watu hadi CHENGE ASIMAME na kusema kitu ambacho kingewapa CCM platform ya KULAZIMISHA kuwa UCHUNGUZI UfANYE TENA...Zitto haraka akapigilia msumari.Thanx GOD team Mbowe ikaamka haraka na kugeuza Manowari. 3.Mtoto wa Mgimwa alionyesha ujinga mwingine,akidhani kuwa anaonyesha kuumia sana rohoni,na kuamini kuwa ubunge aliopewa ni huruma ya CCM.Na wapinzani kuotaka uchunguzi wa Waziri anayewajibika kwa Taifa ni kutokuwa na UTU.HUyu mtoto hisia zimezidi akili yake.Sijui angezaliwa kwa Saddam angesemaje..wakati baba anaadhibiwa?Bahati mbaya sana siku anaamka na kufikiri uchunguzi unahitajika atakuwa kachelewa sana,hata wahusika wengine wanaweza wasiwepo.Poor Boy..kwanini hakupiga kimya km watoto wa Nyerere ili kuachia mlango wa possibilities? 4.Zitto nae alionyesha kutofikiri sana, akajiliza akaleta drama.As if wengine nao hawakuwahi ambiwa kuwa wauaji.Ktk chadema wengi wameambiwa kuwa walimuua Wangwe, na wengine.Ila kwa vile Zitto hupenda weka mambo mabaya ktk kila jema atendalo.Akaamua tuyesha haweza kuwa kiongozi wa juu kabisa halafu taifa liwe nyuma yake.Kwake Zitto yeye ndie Victim pekee na wengine wamlilie yeye.Upuuzi mtupu hajui mama yake alikuwa ktk chama na kiongozi aliyestahili wajibika kwa umma wake? 5.Maccm Wengi walikosa uaminifu Hata Pinda aliyepata huruma ya wapinzani alishaanza chafua hali ya hewa ktk hotuba ya mwisho.Wasira nae akaanza weka CCM ktk hotuba ambayo aliyewapa huruma hakuweka chama chake,wala hata jina UKAWA.Ilikuwa nia njema.Maccm kila koda wanayopata wanataka wachukue sifa zote km wanavyoiba hela zote. 6.Compliments za Mzee wa matusi kwa Zitto na kumlinganisha na Mbowe ilikuwa ni attempt chafu ya kumshambulia Mbowe,ni ishara ya udogo wa akili wa Maccm nahofu yao dhidi ya Mbowe.Cha kushngaza ni kwamba,CCM mara nyingi sana wameponea ktk Busara za Mbowe.Ila baada ya hapo huanza mchafua,sijui km wangafanikiwa mchafua sana,kipindi kigumu wamesimama na nani wakati wananchi wakiwa na hasira? 7BUnge lilijaa watu wenye bifano na maelezo marefu ili kujijengea uhalali wa kusikilizwa ila siku zote walikuwa akimalizia kwa kutetea ule ule uovu ambao ktk kuupinga ndio wanasikilizwa.Haswa wabunge wa CCM ambao wengi walijaa wivu kwa kukosa hiyo haramu,wengine walipambana kuwatetea wenza wao ktk makundi,wengine walikuwa akiwamaliza wapinzani wao ktk makundi.
 
kalisha makalio ,washa ubongo .Sasa unazima ubongo ndio usome?mengine ni kwamba natumia browser isiyokubali paragraphy,new line etc.

Mkuu uwe unatulia unapoandika mada maana hii haiko ktk mtiririko mzuri na wala mawazo na matini hayako sawa kiasi cha kutozalisha dhana na maudhui kamili ya ujumbe wako....

Ondoa chuki na mihemko ili kuleta utulivu Wa fikra na kukufanya ueleweke vizuri.
 
Mmiliki wa 70% ni Standard Chartered Bank Hong kong, na Tanzania lazima itakuja kumlipa.

Ujinga mwengine huo...hao standard walinunua lini? Wao wamenunua madeni ya melchar malaysia lakini sio hisa za Iptl.
Wao wana interest na madeni yao.
Wao hawajawahi kuwa na board member ndani ya Iptl.
Iptl inaendesha shughuli zake bila ya Standard bank.
Hawaja wahi kudai kuwa wao ndio wamiliki hivyo kupinga transfer za melchar to Std bank.
Sakata hili ni mchezo mchafu na watu kulitumia bunge kukashif watu na kupinda sheria kwa vile kuna immunity
 
Wakati watanzania wameaminishwa kuwa hela ya Tegeta Escrow Account ni za serikali,wajanja wachache wachota mabilioni ya shilingi za kitanzania kiulaini.


Taarifa zilizovuja kutoka vyanzo vya uhakika vinaelezea kuwa uhusiano wa Singh na washirika wa Lowassa ulianza wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa nchi wa nchi jirani ambayo ni mwanachama wa EAC.


Baada ya uchaguzi huo kumalizika na kundi hilo kushindwa walihamia Tanzania ambapo mpango mahususi wa wizi wa hela halali za Benki moja iliyopo Far East Asia ulifanywa.


Mchezo huu ulichezwa kwa umakini wa hali ya juu sana ambapo nyaraka za kughushi ziliandaliwa na kundi hili ili kuhalalisha wizi huu uliowapa faida ya mabilioni ya shilingi za kitanzania.


Benki moja nchini ilitumika kupitisha hela hizo,Meneja wa benki hiyo na baadhi ya wafanyakazi wengine wenye uhusiano wa karibu sana na Lowassa wameshafukuzwa kazi.Meneja wa Benki hii ni raia wa nchi jirani mwanachama wa EAC na yupo katika timu ya kampeni ya Lowassa.Meneja huyu ndio aliruhusu hela zitolewe taslimu na kwa kiasi kikubwa sana.


Baada ya kuona wao wameshachafuka,Lowassa na mshirika wake mkubwa katika biashara mwenye asili ya kiasia,walimkabidhi mfanyabiashara mmoja wa kiasia kazi ya kuwa na mtuhumiwa huyo.


Kazi kubwa waliyoifanya ni pamoja na kuwaaminisha watanzania kupitia vyombo vya habari wanavyovimiliki kuwa fedha zile ni mali ya umma na hivyo kuondoa nafasi ya wananchi kuwasogeza karibu na wizi huu.


Walitengeneza mazingira ya kila hila kuonesha kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikalini wameshiriki kuiba na kula fedha hizo.


Hoja iliyowasilishwa bungeni ilikuwa ni wizi wa fedha za umma,lakini mwisho wa mjadala huo ambao ulipamba moto sana,uliishia kutoa adhabu kwa watendaji wa serikali kuwa walikuwa wazembe na waziri mmoja kushitakiwa kwa kusema uongo bungeni jambo ambalo ni tofauti kabisa na hoja ya msingi ilipowasilishwa.
 
tutasikia mengi sana kipindi hiki. kila kitu kitakuwa wazi. just wait and see
 
Back
Top Bottom