Full Time: Simba 0-2 Yanga Taifa 26/9/2015

Full Time: Simba 0-2 Yanga Taifa 26/9/2015

Jukwaa limebaki na washindi tu mikia haoooo wamesepa kidizaini.

Mkuu, subiri wapigwe mechi mbili zinazofuata wamtimue kocha na biashara zao za ukawa ziendelee.
Sasa hivi watashikana uchawi hadi Aveva atimuliwe.
 
Lzm wale kona mikia humu,wale wa taifa tu walisepa dk ya 70

Mikia ni sawa na nyani (Simba) aliyezoea kuvuna mahindi (ushindi) shambani kwa mtu mwingine (Yanga); kila siku anaamini mahindi yapo tu kumbe mwenyewe kagundua huo wizi na kuweka ulinzi mkali. Nyani anapofika hapo lazima apate rungu kila akitoka anajiuliza nimepigwa na kitu gani? Hao ndio Simba waliozoea kuifunga Yanga, hawaamini kilichotokea uwanjani.
 
Nilitabiri hili tokea mapema...raha sana kuwa shabiki wa Yanga,muda wote unajiamini.

Umetisha. Kumbe ukiangalia kwa makini unagundua kumbe sio Simba ni paka mgonjwa.
 

Ndiyo Yeye Aliyefukiwa Baharini Bagamoyo Na Sasa Wamemfukua Baada Ya Ushindi Wenu Wa Kusaidiwa Na Referee POPOMA Israel Nkongo.

Una mkosi kiongozi...wewe ni CCM alafu Simba pote unaelekea kukalishwa!!!!! kuna goli la penati au la makono?
 

Ndiyo Yeye Aliyefukiwa Baharini Bagamoyo Na Sasa Wamemfukua Baada Ya Ushindi Wenu Wa Kusaidiwa Na Referee POPOMA Israel Nkongo.

Mbaazi ikikosa maua husingizia jua!

Kuna bao mlifunga na refa akakataa? Nimeangalia highlights na kuona kuwa dakika 7 ziliongezwa lakini refa alichezesha zaidi ya hizo dakika 7 mfano kipindi Twite anapewa red card ilikuwa dakika ya 98, yote hayo yalifanywa na refa ili angalau mpate hata goli moja kumbe watu wenyewe hambebeki!
 
Back
Top Bottom