Full Time: Tanzania 1 - 0 Guinea | 2025 AFCON Qualifier | Estadio Benjamin Mkapa | 19.11.2024

Full Time: Tanzania 1 - 0 Guinea | 2025 AFCON Qualifier | Estadio Benjamin Mkapa | 19.11.2024

Huitaji Kuwa mchambuzi kuweza kujuwa Stars haina kocha ina wasimamizi wa mazoezi tu.

Hatujachelewa sasa serikali hasa huyo mama ajitolee sasa kumlipa mshahara kocha wa viwango aje kufundisha stars.

Huyo Morocco amepata rekodi ya kuboost cv yake lakini tumwambie asante sana timu inahitaji kocha sasa, tumefuzu kimagumashi tu
Unamaana gani unaposema tumefuzu kimagumashi!!!
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Timu imefuzu kwa kushinda mechi 3 kufungwa 2 na kudroo moja.Mvimba macho anaita imeshinda kimagumashi.Ni chuki tu za kitofautiana kisiasa.
Yani kanishangaza sana hizo mechi tatu tumeshinda kihalali na tumefungwa kihalali pia.

Kuna mechi tulizicheza vizuri na kuna mechi tuliyumba kidogo na ndio football ilivyo watu wamevuja jasho sana wanastahiki kupongezwa. Walimu waliyumba wakaambiwa wakarekebisha baadhi ya maeneo.
 
Zinapocheza Simba na Yanga kwenye mashindano ya kimataifa utakuta wavimba macho wanazishangilia licha ya timu hizo kuonyesha wazi misimamo yao kisiasa. Linapokuja swala la timu ya Taifa ndio unakuta vinajitokeza kuiponda eti kwa sababu zinauungwa mkono na upande wasioupenda.Logic ya kijinga mno.
 
Wasaliti wote kwa Taifa lao, waliokuwa wanaombea Taifa Stars ifungwe, wakati timu ya Guinea inaondoka nchini waondoke nayo. Utaratibu ni kwamba unakwenda kula ugali kule ulipopeleka mboga.
Mawazo yenye kiwango cha chini Sana cha kufikiri. Usaliti ndiyo unapimwa hivyo?

Hivi mafisadi waliokuwa wanashadadia stars ishinde na wachapakazi waliokuwa hawaishangilii staz nani msaliti?
 
Screenshot_20241119-213130 (1).jpg

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwapa zawadi ya Tsh. milioni 700 Taifa Stars baada ya Tanzania kufuzu AFCON 2025 ambayo michezo yake itachezwa Morocco.

Akiongea na Wachezaji wa Stars Jijini Dar es aalaam leo November 19,2024, Waziri Ndumbaro amesema “Rais Samia alikuwa kwenye mkutano Brazil lakini kila baada ya dakika Wasaidizi wake walikuwa wanampenyezea karatasi kumuonesha matokeo yakoje, karatasi ya kwanza ilisema Msuva amekosa goli, ya pili Feitoto kapaisha, ya tatu Mzize anawatapisha Mabeki, ya nne wakamwambia Msuva aliyekosa magoli kafunga bao, Mh. Rais anawapongeza sana, pili ameelekeza Bunge la February mualikwe Bungeni, tatu amesema leo amedondosha kwenu zawadi za pongezi Tsh. milioni 700 na Mama hana mbambamba”

Itakumbukwa Rais Samia pia alilipia tiketi zote za mchezo wa leo na kuruhusu Wananchi kuangalia mchezo huo bure na pia alitoa ndege ya kupeleka timu ya Taifa CONGO DRC ambako Taifa Stars ilicheza na Ethiopia na kushinda mchezo huo.
 
Machawa wamejikita kusifia mtu ambaye hakutoa jasho leo.
Wamejikita kumsifu Shibiki mwenzetu, mzalendo mwenzetu.
Mimi naelekeza sifa zote kwa wavuja jasho wetu waliokuwa wakisimamiwa na wataalamu
Hemed Morocco
Juma Mgunda
Jamhuri Julio Kiwelu
Na Nahodha wa jahazi akiwa Mbwana Samata.
Mmefanya kazi kubwa sana kuliheshimisha Taifa letu.
Hatuna kikubwa cha kuwalipa kwa furaha hii mliyoitengeneza kwa Taifa letu. Hongereni sana.
Dua zetu zitakuwa nanyi daima.
IMG-20241119-WA0052.jpg
 
Upotezaji wa hela tu hata kumi na sita bora hatufiki
 
Wasaliti wote kwa Taifa lao, waliokuwa wanaombea Taifa Stars ifungwe, wakati timu ya Guinea inaondoka nchini waondoke nayo. Utaratibu ni kwamba unakwenda kula ugali kule ulipopeleka mboga.
NMewaandalia bites waende nazo tumewachoka wanafiki
 
Back
Top Bottom