FULL TIME || TotalEnergiesCAFCC || Stellenbosch 0-0 Simba SC || Aggreggate 0-1 || 27.04.2025 || 16:00 EAT || Moses Mabhida Stadium

FULL TIME || TotalEnergiesCAFCC || Stellenbosch 0-0 Simba SC || Aggreggate 0-1 || 27.04.2025 || 16:00 EAT || Moses Mabhida Stadium

Aibuuu kwa Kibu eti anajirusha baada ya mkono 🤣
 
View attachment 3316905

Mechi ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika mkondo wa pili kupigwa leo Jumapili.

Mnyama Simba SC atakuwa dimba la Moses Mabhida akicheza na Stellenbosch.

Mnyama anaingia katika mchezo huu akiwa na mtaji wa goli 1 - 0 alilopata kwenye mchezo wa kwanza pale Zanzibar.

Mechi hii itapigwa kuanzia saa 10:00 jioni.

Karibu kwa live updates

Kikosi cha Simba SC kinachoanza dakika 45 za kwanza
View attachment 3317523

Kikosi cha Stellenbosch kinachoanza dakika 45 za kwanza
View attachment 3317537

Hili ni vibe la Stellenbosch wakiingia uwanjani
View attachment 3317539

Simba SC wakiingia uwanjani wakiwa watulivu wa akili na mwili bila mbwembwe

View attachment 3317544View attachment 3317545View attachment 3317546View attachment 3317547

KIPINDI CHA KWANZA
  • Mwamuzi anapuliza kipyenga kuashiria kuanza kwa Mchezo
  • Mchezo unaanza kwa kasi timu zote zikiwa na hamu ya kupata goli la kuongoza
  • Dakika ya 03 Mousa Camara anapangua mpira moja matata na kulicha lango lake likiwa salama
  • Dakika ya 06 Stellenbosch wanakaba kama nyuki
  • Dakika ya 11 Kibu Denis anachezewa madhambi pale ndani ya Box, Refa anafunika mkwaju wa Penati
VAR CHECK - Refa anenda kujiridhisha kupitia VAR
  • Dakika ya 15 VAR CHECK - Hakuna Penati
  • Dakika ya 20 Mukwala anapoteza mpira Stellenbosch wanapiga counter attack Mwamba Camara anaokoa
  • Dakika ya 22 lango la Simba SC ilnakoswakoswa pale wanapoteza nafasi ya kufunga goli Stellenbosch
  • Dakika 25 Stellenbosch wanapata mpira wa kurusha hapa
  • Mpira Mrefu wa kurusha Simba wanaponea chupuchupu hapa
Asante kwa Updates
 
Back
Top Bottom