Hayawi hayawi sasa yamekuwa, zilikuwa ni wiki zikawa siku hatimae ule muda wa kusubiri umeisha na leo ndio ile siku ya kuhitimisha michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya kwa msimu wa 2024/25.
Mtanange wa leo utakuwa baina ya mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG): na washindi wa nafasi ya pili kutoka ligi kuu soka nchini Itali Inter Milan, mtanange ambao utaanza mishale ya saa 4 kamili kwa saa za Afrika ya mashatiki katika dimba la Allianz arena mjini Munich nchini Ujerumani.
Ikumbukwe ya kuwa hii itakuwa fainali ya pili kwa timu ya PSG ikiwa mara ya kwanza ilivheza fainali mwaka 2020 dhidi ya Bayern Munich na kupoteza kwa goli moja bila. PSG wamefika hayua hii baada ya kuwaondosha vigogo wa soka nchini uingereza Arsenal kwa jumla ya mabao matatu kwa moja.
Kwa upande mwingine timu ya Inter milan itashika dimbani usiku wa leo kutafta taji lake la nne la ligi ya mabingwa barani ulaya huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa mwisho wa fainali dhidi ya wababe toka Uingereza timu ya Manchester city kwa bao moja bila majibu.
Wao wametinga fainali baada ya kuwaondoa watemi kutoka nchini hispania Barcelona kwa jumla ya magoli saba kwa sita.
Je ni Osmane Dembele au ni Lautaro Maryinez kuibuka kidedea usiku wa leo?.
Mimi na wewe hatuna manibu, majibu yatapatikana kuanzia mishale ya saa nne za usiku pale Allianz stadium.