Full Time: Yanga SC 1 - 3 Tabora United | NBC Premier League | Azam Complex | November 7,024

Full Time: Yanga SC 1 - 3 Tabora United | NBC Premier League | Azam Complex | November 7,024

Alianza Adam
Akafuatia Samson
Kisha ....
IMG-20241107-WA0096.jpg
 
Tatizo Yanga wanataka wakafunge ndani ya 18 siku ile Pacome alifunga nje ya 18 ndio wanatakiwa wafunge magoli ya vile haya magoli ya pasi pasi mpaka ndani ya 18 ni kupoteza muda tu nje ya 18 pale achia dongoooooo usilembeeeee
Na ndio ufungaji utakaolipa mambo ya wanaopaki bus
Na kila timu saizi lazima ikamie
 
Yao Yao Kwasi majeruhi
Bocca majeruhi
Baka ana nyekundu

Mabeki hao wote wameenda bench sasa Yanga imebakia haina mabeki kule nyuma amebakia Mwamnyeto tu

Kingine Yanga hawatulii uwanjani sijui kuna tatizo Diara magoli yanaingia hata haruki lile goli la kwanza limeingia hajaruka kaacha tu liingie angeruka hata angepangua lingekua sio goli na goli la pili pia hivyo hivyo na goli la tatu hakua anafuata mpira karibu magoli yote kwa hio Diarra bila mabeki hakuna kitu Yanga itaishia kufungwa tu Aucho amejitahidi sana kumsaidia Mwamnyeto pale ila haikuwezekana sababu Tabora walikua wanarudi wote nyuma kuziba goli ila Yanga wanawaachia Aucho na Mwamnyeto huku nyuma wengine hawarudi nyuma kwa hio Tabora wanakuja wengi wanajifungia tu

Kingine Pacome Aziz Ki Mudathir Mzize Chama Maxi Nzengeli Dube wakifika karibu na goli nje ya 18 wajaribu kutia mashuti walenge goli km alivyokua anafanya Sureboy alilenga mara 2 ila alikua anatoa nje hayakua yanalenga goli yale mashuti kwani nani aliewafundisha wakafungie ndani ya goli ndani ya 18 nani anawaambi wapasiane mpaka ndani ya 18 yaan wakafungie mbele ya kipa ndani ya 18 Gamond ndio anawalazimisha wafanye hivyo?

Mimi sikuelewa yaan wanakazana wakafungie ndani ya 18 kwanini wasifunge nje ya 18 wangepiga mashuti mengi nje ya 18 Tabora ingefungwa Yanga walikua na nafasi nyingi za kufunga ila mbinu waliyoitumia ndio imewafelisha Mwalimu kwanini anawalazimisha wakafungie ndani ya 18? Kwanini wasitie mashuti nje ya 18 pale kufunga kupo tu

Kingine Yanga wachezaji wakifika karibu na goli hawatulii kabisa yaan sijui niseme hawajiamini au namna gani ila hawatulii wakifika golini kufunga km wanashikwa na kitete sio Aziz Ki sio Pacome sio Dube sio Maxi yaan almost wote wakifika golini kufunga wanakua km wanakosa kujiamini hivi sasa sielewi hawa wachezaji wa Yanga wana matatizo gani?

Kidogo niliemuona Kibabage alikua anajituma sana na confidence za kutosha na Sureboy, Chama na Mzize nae kwa mbali walikua wametulia tatizo lilikua ni wakifika goli la Tabora Tabora wote wanajaa golini wote wanaziba goli wote ila kwa Yanga mpira ukifika golini kwa Yanga anaekuepo kuzuia ni Mwamnyeto na Aucho tu wengine wote hawarudi golini kuzuia wasifungwe hapo lazima mfungwe na Tabora walipoona hilo wakawa wanatumia mwanya huo huo kwenda kufunga na wanaenda wengi kule goli la Yanga yupo Aucho na Mwamnyeto tu ndio wanalinda goli kwanini msifungwe wakati mpo out numbered?

Wachezaji wa Yanga hawapo sawa kabisa kocha inabidi abadiri kikosi Aziz Ki Pacome Maxi hawa wasianze dakika 45 za kwanza inabidi watokee bench Chama Mzize na Dube inabidi waanze dakika 45 za kwanza Aziz Andambwile sijamuona jana Baleke aingizwe dakika za mwishoni zimebaki 20, 10 au 15 ndio aingizwe Nickson Kibabage Khalid Aucho ni bunduki za Yanga

Watu kwenye bandaumiza walikua wanasema Yanga pale nyuma haina beki mpaka nikasogelea TV nimtafute Mwamnyeto ndio nikamuona Bakari Nondo nikajiuliza hamna beki au hamna Mabeki?
Ukute jana wenzio walikuwa wanaona wanafukuzwa na nyuki
Ohooo 🤣🤣🤣
 
Na ndio ufungaji utakaolipa mambo ya wanaopaki bus
Na kila timu saizi lazima ikamie
Ndio dawa ni hio inabidi wakifika nje ya box waachie mikuki pale wasisubiri mpaka waingie ndani ya 18 yaan nimeshangaa Aziz Ki alikua na hio kawaida naona Gamond kampiga marufuku kwa hio sasa hivi analazimika akafungie ndani ya 18 wakati mnaocheza nao wanawakamia fika nje ya 18 achia fataki moja lenga goli lazima goli liingie tu, Yanga kuna tatizo sio bure kuna tatizo wachezaji kuna kitu wanalazimishwa wafanye kwanini hawachezi kwa uhuru kwanini mpaka ndani ya 18? Kwanini sio nje ya 18? Yaan pale jana nafasi kibao nje ya 18 wangeachia mashuti lazima kuna mashuti hata matatu yangeingia wavuni
 
Ndio dawa ni hio inabidi wakifika nje ya box waachie mikuki pale wasisubiri mpaka waingie ndani ya 18 yaan nimeshangaa Aziz Ki alikua na hio kawaida naona Gamond kampiga marufuku kwa hio sasa hivi analazimika akafungie ndani ya 18 wakati mnaocheza nao wanawakamia fika nje ya 18 achia fataki moja lenga goli lazima goli liingie tu, Yanga kuna tatizo sio bure kuna tatizo wachezaji kuna kitu wanalazimishwa wafanye kwanini hawachezi kwa uhuru kwanini mpaka ndani ya 18? Kwanini sio nje ya 18? Yaan pale jana nafasi kibao nje ya 18 wangeachia mashuti lazima kuna mashuti hata matatu yangeingia wavuni
kushuti nje ya 18 nakufunga goli inahitaji enegy kubwa sana jambo ambalo wachezaji wa nyumamwiko hawana kwa sasa
 
kushuti nje ya 18 nakufunga goli inahitaji enegy kubwa sana jambo ambalo wachezaji wa nyumamwiko hawana kwa sasa
Sureboy mboni alikua anatia mashuti pale ila tatizo ni kushindwa kulenga goli tu hivi vitimu vinavyokamia kamia dawa yao ndio hio tu fungia mbali tia mashuti ya mbali mpaka kipa afie uwanjani tia mashuti ya mbali mpaka kipa akidaka aletewe machela akapumzike nje

Tatizo sio kwamba Yanga hawafungi kwa kupiga mashuti ya mbali ila naona kocha kabadiri mfumo anataka wafungie ndani ya 18 sasa kufungia ndani ya 18 kwa wakamiaji sio jambo la kawaida fungia mbali tia mashuti ya mbali mpira lazima utaingia tu, Gamond awaachie wale wachezaji wafunge magoli ya mbali sio anawalazimisha wakafungie ndani ya 18 kwa timu zinazokamia lazima abadiri mfumo mashabiki tunachotaka ni magoli sio mbwembwe sisi goli liiingie tu sio kingine hayo masuala ya mfumo mfumo baki nao huko huko sisi tunataka magoli tu
 
Nawambiaje. Kuna namna hizi timu mbili wanamtumia haji manara katika kupata ushindi. Naona toka yanga waanze kuwa na mzozo na manara mambo yamekuwa magumu sana kwao.
Simba Haji alitumika kama msemaji na mhamasishaji tu. Kwa Yanga anatumika kama mratibu wa waganga, sina hakika kama kuna mabadiliko
 
Mmemuona Azizi Ki saizi yupo ndani na hakuna kitu anafanya.

Then akitoka nje anageuka kuwa kocha msaidizi kuanza kuwa lecture wenzake.

Anaona ni rahisi kuwaambia wenzake cha kufanya wakati yeye akiwa humo ndani anashindwa kutekeleza
Ndio mpira ulivo mkuu
Haya waangaliaji pia wakatj mwengine hugeuka tukawa makocha 🤣🤣🤣
 
Mechi: Yanga SC VS Tabora United
Ligi: NBC Premier League
Uwanja: Azam Complex
Tarehe: November 7,024
Muda: 🕖 6:00PM
View attachment 3145701


Dakika, 11 Si Yanga wala Tabora hakuna timu iliyopata goli hadi sasa.

Dakika, 15 Mchezo umendelea kuwa mzuri timu zote zinacheza kwa utulivu sana.

Dakika, 19 Tabora wanapata goli kupitia Chikola.

Dakika, 30 Yanga wanaendelea kufanya mashambulizi hadi sasa bado awajapata kusawazisha goli.

Dakika, 34 Mlinda mlango wa Tabora amekuwa bora kudaka mipira hatari kutoka kwa Yanga.

Dakika, 44 Bado ngoma ngumu kwa Yanga hadi sasa. Tabora wakiwa bado wapo mbele.

Dakika 4 zimeongezwa kutamatika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Dakika, 47 Yanga wanapata penati.

Dakika, 48 Tabora wanapata goli la pili kutoka kwa Chikola.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika.

Dakika 45 za kipindi cha pili kimeanza Je Yanga atafanya maajabu ya soka kusawazisha magoli mawili.

Dakika, 54 Hussen Masalanga anatoka baada ya kupata maumivu.

Dakika, 59 Yanga wanaendelea kulisakama goli la Tabora lakini mambo ni magumu
Hawa, pamoja na kwamba kiafya nyuki watatu wakikudunga ni TIBA, wakumbuke kilichoipata timu ya IHEFU. Baada ya kutambua kuifunga Yanga kila msimu hatimai haipo katika Ulimwengu wa soka.
 
Sasa tukipunguza mdomo tutakula na kuzungumza kwa kutumia nini bila kuwa na mdomo? <do,o mi kitu cha muhimu sana katika maisha ya kila kiumbe; hata wewe una mdomo na huwezi kuupunguza.
Unajua mzee...

Hapa duniani, hakuna watu huaibika kama wajuaji...

Ukijifanya wajua kila jambo, waja watakusubiri siku ya aibu yako wakunyooshe vizuri...
 
Simba Haji alitumika kama msemaji na mhamasishaji tu. Kwa Yanga anatumika kama mratibu wa waganga, sina hakika kama kuna mabadiliko
Wamemvuruga ndio maana mambo hayaendi kwao vizuri siku ukiona picha za haji akianza kuisifia yanga ujue mamb yatakuwa mazuri upande wao
 
Back
Top Bottom