Ndio nimemaliza, mpangilio huu wa ulimwengu lazima una mwanzo, au mbunifu aliyefanya hiyo kazi, bila shaka ni Mungu hakuna anayeweza kufanya aliyofanya
Hoja yako ya kwamba mpangilio huu lazima una mwanzo, na bila shaka mwanzo huo ni Mungu ina mapungufu mengi.
Kwanza umelazimisha kwa kuweka "bila shaka" bila kuelezea kwa nini iwe "bila shaka".
Una hakika gani chanzo cha ulimwengu huu ni Mungu?
Ulimwengu kulazimika kuwa na chanzo haina maana kwamba chanzo ni lazima kiwe Mungu.
Yani ni hivi, wewe muafrika kulazimika kuwa na baba, kwamba haiwezekani uwepo bila kuwa na baba mzazi, haimaanishi automatically baba yako ni Donald Trump aliyekuwa rais wa Marekani, mzungu.
Hoja uliyoitoa hapo ni sawa na kusema kwamba wewe muafrika, baba yako mzazi ni Donald Trump, mzungu. Kwa sababu wewe ni lazima uwe na baba.
Hata kama ni lazima uwe na baba, hilo halithibitishi baba yako ni Donald Trump. Thibitisha baba yako ni Donald Trump.
Hata kama ulimwengu ni lazima uwe na mwanzo, hilo halimaanishi mwanzo wake ni lazima uwe Mungu. Thibitisha mwanzo wake ni Mungu, usilazimishe hili kwa nguvu tu.
Hili la kwanza.
La pili,
Ukisema kitu chochote chenye mpangilio/complexity ni lazima kiwe na muumbaji, kimsingi unajiwekea mtego wa kuulizwa na Mungu naye ni complex, hivyo naye lazima atakuwa na muumbaji, na muumbaji wake naye ana muumbaji, na muumbaji wake ana muumbaji, ad infinitum, ad nauseam.
Yani ukishasema kila kilicho na mpangilio na complexity kinahitaji muumba, umeshakubali hakuna Mungu. Kwa sababu kila Mungu utakayemuweka atahitaji kuwa ameumbwa na Mungu/ kitu kingine, na akishaumbwa na Mungu au kitu kingine tu, anakuwa si Mungu.
Kwa hivyo, hii hoja ya kusema kwamba mpangilio wa dunia unathibitisha kuna Mungu, ni hoja ambayo inaweza kuonekana ya maana kwa mtu asiyefikiri kwa kina tu.
Kwa mtu anayefikiri kwa kina hii si hoja ya kutetea uwepo wa Mungu.
Kwa mtu anayefikiri kwa kina, hii hoja inaonesha Mungu muumba vyote hawezi kuwapo.