Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Dhana nzima ya chanzo kuwa ni kitu cha lazima ni dhana potofu.Je nitakuwa sahihi nikisema wewe haupo duniani na sio hai kwa kuwa hajathitisha chanzo cha uhai wako?
Kwa hivyo, hoja yoyote inayoshikilia dhana ya chanzo kuwa ni kitu cha lazima imejengwa katika msingi potofu.
Nimeongelea "Quantum Causal Loops" na kuweka link awali kwenye thread hii.
Ni udogo wa mawazo na ukosefu wa elimu tu unaoweza kumfanya mtu aone chanzo kuwa ni hoja muhimu na ya lazima.
Dhana nzima ya chanzo si muhimu wala ya lazima.
Zaidi,
Tatizo lako si tu kwamba huwezi kuthibitisha Mungu yupo.
Tatizo lako ni kwamba jitihada zako za kuthibitisha Mungu yupo, pamoja na ulimwengu tunaouona, vyote vunam cintradict Mungu huyo.
Mimi, hata ukisema sipo kwa sababu siwezi kuthibitisha chanzo cha uhai wangu, hakuna kitu chochote katika ulimwengu huu kinacho contradict uwepo wangu. Hakuna maelezo ya uwepo wangu yasiyo na logical consistency kiasi cha kuonesha kwamba siwezi kuwapo.