Uchaguzi 2020 Funzo nililolipata baada ya kupata 0 kwenye kura za maoni za udiwani CCM

.
Wasikupe pole bali hongera kwa kujaribu. I like your attitude.. Utafika mbali mzee
 
.
Wasikupe pole bali hongera kwa kujaribu. I like your attitude.. Utafika mbali mzee
Nashukuru Sana mkuu kwa kunitia moyo.
Mkuu ukiona umepata hiyo kura ujue kwanza siasa unailazimisha , pili hata ukishinda uko kwa personal interest zaid, na hautakuwa pale to serve wapigakura wako
Kwanini umeniona nipo kwa pesrsonal interests mkuu? Funguka nijirekebishe maana maana sipendi nionwe hivyo wakati Sina uchu huo wa madaraka zaidi ya dhamira yangu ya dhati ya kuwatumikia wananchi na ndiyo maana utaona nimeipokea hiyo sifuri kwa mikono miwili kuliko ningepata hata kura moja.
 
Ndugu wajumbe mwaka huu mmelaaniwa sana yan
 
Hahaaaaa,na wewe imekukuta?


Mimi na wasomi wenzangu tuliunda kundi la vijana na tukasajili Halmashauri.

Tukagombea nafasi mbalimbali ikiwemo kujaza nafasi za kamati ya siasa ya tawi, Halmashauri Kuu ya Tawi, EMAU na n.k.

Yale majina yalipelekwa kata.

Kata wakafanya udadisi wakagundua kuwa Katibu wa Tawi ni kijana na yupo upande wetu.

Wakamtumbua Katibu.

Kwa hasira uongozi mzima kuanzia mwenyekiti wa Tawi na jumuia zake wakajiuzulu.

Akaja kaimu Katibu akafuta mchakato wa uchaguzi ule tukachukua fomu tena ila tukafyekelewa mbali.

Nikagundua tatizo pale.

Kundi letu likagawiwa hela ila pesa ile milion 5 ikaingizwa kwenye kundi katika mtaa ule linasadikika ni la 'wajumbe'.

Kimsingi ukitaka kujua siasa za CCM wewe shiriki shughuli za chama ngazi ndogo tu ya Tawi utajua kila kitu.

Nilichoka sana.

Kumbe jamaa walihisi ujio wa wasomi ni hatari maana maamuzi tungefanya sisi na ushawishi pia.

Kimsingi Kama ulikuwa hujui ujumbe unarithishwa Kama ufalme.

Baba akifa anamwachia mtoto au mke katika baadhi ya maeneo.

Kuna jamaa zangu waligombea mwaka huu hawataki hata kunijibu imekuwaje.

Wajumbe ni wazuri kwa hulka na maongezi ya bashasha ila sasa kinyume chake ndiyo hivyo yaani Ni Wana usalama fulani na Wana Siri hatari.
 
Mkuu mpaka unapata 0 hukukumbuka hata kujipigia wewe mwenyewe?
 
Na hii ni kwa Tanzania nzima yaani inachekesha Sana baada ya kuhuzunisha.

Fikiri Mimi kaka yangu aliyeniachia ziwa ndiyo mwenyekiti wa kijiji chetu Sasa lakini hakunipa kura,Kuna shemeji yangu mmoja kaoa dada yangu aliyemuachia ziwa huyu kaka yangu mwenyekiti lakini hakunipa kura,Kuna mjumbe mmoja alikuwa kwenye foleni akinipa tabasamu na Mimi nikawa nafurahia kuwa kura yangu hii maana tulizungumza mengi Sana kabla ya mchakato kumbe ndo anaenda kunichinjilia huko.

Mgombea mwenzangu mmoja naye mwajiriwa mjumbe mmoja ni mpwa wake kabisa,wawili ni wakwe zake hivyo akawa anahesabia kuwa ni kura zake ajabu alipata kura moja aliyojipigia yeye mwenyewe maana alikuwa ni mjumbe.

Sasa msikilize Steve Nyere ndo unacheka balaa alichofanyiwa.
 
Wajumbe , hawasikilizi hotuba yako ya kujinadi.

Kweli umejilipia kujifunza siasa, sasa yule atakayeteuliwa wewe jipendekeze kuwa mshirika wake.

Piga kampeni za nguvu kumnadi hiyo ndiyo njia ya kujitambulisha kwa wananchi.
 
Wajumbe , hawasikilizi hotuba yako ya kujinadi.

Kweli umejilipia kujifunza siasa, sasa yule atakayeteuliwa wewe jipendekeze kuwa mshirika wake.

Piga kampeni za nguvu kumnadi hiyo ndiyo njia ya kujitambulisha kwa wananchi.
Na nimeahidi kufanya hivyo bila kinyongo.
 
Hapo
Na nimeahidi kufanya hivyo bila kinyongo.
Hapo sasa ndo unajiwekea hazina uchaguzi ujao.

Usisahau takrima mdogomdogo, madaftari kwa wanafunzi, penseli ,ufutio gawa mwenyewe kwa wanafunzi hao ni watoto wa wajumbe salamu zinafika.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] wajumbe mwaka huu sio walirogwa na Nani wamekula hela za wengi na wakawatosa nadhani mpaka warogwe
 
Kali kuliko you're majibu ya wajumbe was ccm kwa wagombea ,wakiulizwa mtanipa kura kura? Wanajibu tuko pamoja kuja kuhesabu kura unaambulia 0.
 
Mkuu acha ujivuni,kwani kuwa diwani lazima uwe msomi,na je hizo ndio sifa zinazotakiwa kuwa diwani,kumbuka hao hao wa darasa la nne ndio wapiga kura,wanawajua nyie wasomi kwa kuleta mbwembwe za kijinga, kuna mheshimiwa mmoja ni waziri kaporomka,alipokuwa kwenye kijiji kimoja akawa anajinasibu kwa mengi ya kitoto oh mara mimi ni tajiri,mimi nina pesa ,nina magorofa huko Dar,sasa kikaja kipindi cha maswali akaulizwa mh tulikusikia ukijinasibu kuwa wewe ni tajiri na maneno mengi je utajirika wako sisi unatusaidia nini?na kama tajiri huku unafuata nini?akaishia kufoka na kudai wewe wa darasa la pili unataka uniambie nini, matokeo akaangukia pua.
 
KUMBESOL JNAIJUÀ MSITUMALIZIE.MB ZETU
KAJIPANGE
1) 2025 UWE NA FEDHA ZA RUSHWA A KUTOSHA
2))JIFUNZE UNAFIKI...HILI SIKUTARAJIA LIMEKUSHINDA

MAANA MA.MC WENGI WANASIFIKA KWA UNAFIKI ILI KAZI ZAO ZIENDELEE HAPO TAFUTA MKONGWE AKUSAIDIE UNAFIKI GAN UNATAKIWA

3))HILII NDILOO LINAWAMALIZA WENGI SIASA N LAZIMA UCHAGUE.MAWILI KUWA NA MUNGU MPAKA.MWISHO AMA.KUWA NA SHETAN😁😁😁

UWEZI KUSALI NA KUTOA RUSHWA UKATEGEMEA UTASHINDA

WENZENU WANASHINDA WAMEJIKITA.MAZIMA.UPANDE WAPILI

UKIWA VUGUVUGU UNAISHA MAZIMA KWENYE SIASA HILI USILISAHAU 2025
KILA.LA KHERI MPWAAA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…