Furaha kutoka Gerezani, huzuni kufika Nyumbani

Furaha kutoka Gerezani, huzuni kufika Nyumbani

Ali Nassor Px

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2022
Posts
2,384
Reaction score
3,926
Baada ya kuiona habari hii nikaona acha nivae uhusika. Ya watuhumiwa wa ugaidi kuachiwa huru baada ya miaka tisa ( 2014-2023).

IMG_7637.jpeg

Katika hali ya kawaida tu mtu anapotoka kwenye matatizo basi roho yake na nafsi yake usawajika.

Tokea 2014- 2023 ni miaka 9 imekatika wale walioingia gerezani kwa tuhuma ya kesi za ugaidi sasa wameachiwa huru kabisa.

Nashukuru kwanza kwa jamaa kuachiwa ila bado nabaki na maswali maana kesi au matatizo yanamkuta mtu yoyote yule.

Wapo ambao sio watumia bangi lakini washawahi kukamatwa na kukutwa na kesi za bangi. Maswali ninayojiuliza mda huu;
1. Huyu mtu aliyefungwa miaka 9 akifika nyumbani kwake anaanza vipi kutengeneza uhusiana wake na mtoto wake (Kwa sababu malezi yanahitaji wazazi wawili). Mtoto anamtafsiri vipi baba yake ?

2. Huyu mtu kabla ya tuhuma labda alikuwa na biashara zake atajisikia vipi akifika nyumbani akikuta hakuna kitu kabisa (kuanza mmoja)?

3. Vipi mkewe kipenzi aliyemuacha miaka 9 nyuma bado anamsubiri yeye tu arudi maisha yaendelee au kashaolewa na mwanaume mwengine?

4. Serikali unamuacha acha vipi huyu mtu ambaye ana hatia wanamuachia kwa kauli yupo huru tu au kuna chochote kitu anapewa kimsogeze kimaisha?

Tujadilini kwa pamoja.
 
Kuna wengine wake zao waliamua kujiua, wengine wake zao walishaolewa, familia zingine zilishasambaratika, lakini wahusika wamejengeka kiimani zaidi,

maana kuna wakati unapata mitihani mikubwa kutokana na sababu ya imani yako ukajikuta uko kalibu na Muumba wako kuliko mtu mwingine yeyote yule, ukabaki kujioni mshindi siyo mshindwa, naamini huko gerezani walikuwa wanaswali mda wote na wataendelea kuswali

Haya maaisha ya duniani ni upuuzi mtu, usitumie madaraka yako kumtesa mtu, wako wapi waheshimiwa wa kidunia waliotukuzwa?Wamelala wameoza wamebaki mifupa mitupu
 
Kuna wengine wake zao waliamua kujiua, wengine wake zao walishaolewa, familia zingine zilishasambaratika, lakini wahusika wamejengeka kiimani zaidi,

maana kuna wakati unapata mitihani mikubwa kutokana na sababu ya imani yako ukajikuta uko kalibu na Muumba wako kuliko mtu yeyote yule ukabaki kujioni mshindi siyo mshindwa, naamini huko gerezani walikuwa wanaswali mda wote na wataendelea kuswali

Haya maaisha ya duniani ni upuuzi mtu, usitumie madaraka yako kumtesa mtu, kwa waheshimiwa wa kidunia waliotukuzwa wako wapi? Wamelala wameoza wamebaki mifupa mitupu
Sipingani na wewe kuwa wanaishi kiimani sana lakini dakika ya mwisho na wao ni binadamu kama binadamu wengine.

Hawa watu wasipowezeshwa na kuwekwa sawa kisaikolojia wanaweza kupiga tukio la kweli kama la mwanzo lilikuwa ni tuhuma hewa tu
 
Hakuna kitu kizuri kama uhuru ndugu nenda kamulize Sabaya atakuambia

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Nakubaliana na wewe kuwa uhuru ni jambo jema sana ila na wewe jaribu kujiuliza ayo maswali niliyojiuliza mimi alafu vaa uhusika utagundua kuwa.

Furaha inaweza ikaja pale inapotoka kauli ya upo huru lakini ukifka kwako unaanza kuwa na stress
 
Hiyo sheria ya ugaidi ni miongoni mwa sheria ovu.. ililenga kuua uislamu...
Mauaji aliyofanya Mackenzie pale Kenya angekuwa amefanya shekh yqngetambuliwa na Dunia nzima km ugaidi.
Nadhani kuna aja ya serikali sasa kulekebisha sheria ya ualifu sana sana kwenye mda wa kufatilia kesi
 
Baada ya kuiona habari hii nikaona acha nivae uhusika. Ya watuhumiwa wa ugaidi kuachiwa huru baada ya miaka tisa ( 2014-2023).

View attachment 2660266

Katika hali ya kawaida tu mtu anapotoka kwenye matatizo basi roho yake na nafsi yake usawajika.

Tokea 2014- 2023 ni miaka 9 imekatika wale walioingia gerezani kwa tuhuma ya kesi za ugaidi sasa wameachiwa huru kabisa.

Nashukuru kwanza kwa jamaa kuachiwa ila bado nabaki na maswali maana kesi au matatizo yanamkuta mtu yoyote yule.

Wapo ambao sio watumia bangi lakini washawahi kukamatwa na kukutwa na kesi za bangi. Maswali ninayojiuliza mda huu;
1. Huyu mtu aliyefungwa miaka 9 akifika nyumbani kwake anaanza vipi kutengeneza uhusiana wake na mtoto wake (Kwa sababu malezi yanahitaji wazazi wawili). Mtoto anamtafsiri vipi baba yake ?

2. Huyu mtu kabla ya tuhuma labda alikuwa na biashara zake atajisikia vipi akifika nyumbani akikuta hakuna kitu kabisa (kuanza mmoja)?

3. Vipi mkewe kipenzi aliyemuacha miaka 9 nyuma bado anamsubiri yeye tu arudi maisha yaendelee au kashaolewa na mwanaume mwengine?

4. Serikali unamuacha acha vipi huyu mtu ambaye ana hatia wanamuachia kwa kauli yupo huru tu au kuna chochote kitu anapewa kimsogeze kimaisha?

Tujadilini kwa pamoja.
walifungwa na muislamu mwenzao wakaachwa na muislamu mwenzao.
 
mwaka 2012-14 ilikua ni miongoni mwa miaka mibaya sana Arusha, vijana wengi walikamatwa kwa kuhisiwa ni magaidi na mmoja ninae mfahamu aliuwawa kwa kupigwa risasi wakisema alijaribu kutoroka akiwa anatoka mahakamani kurudishwa mahabusu gerezani

jamaa alikua mtu poa sana alikua ni brother kitaa nafikiri kupenda kwake mazoezi ilimfanya watu waende kutoa taarifa za uongo /za hisia ya ugaidi
 
Back
Top Bottom