west african wametuharibia sana. Waafrica hatuaminiki kwa sababu ya tabia zao za kishenziUnachokisema ni kweli. Lakini bafo inawezekana .. ni wewe tu na jinsi gani unchat na muhusika wako , kuna wayu akili hazijakuwa anachata na mchuchu anamuomba hela sasa utaachaje kuonekana tapeli hahahahaha
Sikumbuki mkuu....uzi unaukumbuka unaitwaje?
Mkuu, Vibali gani inahitajika kuwa na vyo ili uweze ku export bidhaa nje?Wakuu, njia ingine nzuri zaidi ya kutoka nje na kujitayarisha kuwa mfanyabiashara wa bidhaa.
Ila lazima uwe mfanyabiashara smart unaelewa biashara na masoko, sheria mbalimbali na viwango vya nchi husika na kadhalika.
Bidhaa nyingi Ulaya sasa hivi zimekuwa haba kutokana na masuala kama ugonjwa wa UVIKo-19 ambao umesababisha biashara nyingi ndogo kufa.
Kwa mfano waweza kuamua kuwa wasafirisha nje, bidhaa ambazo ni "hot cake" katika maduka ya huko kama maparachichi, na sasa hivi kama kule UK wanahitaji sana Viazi kwa ajili ya chips.
Suala ambalo wazungu siku zote wanataka ni viwango, kuanzia kuvuna hadi kupakia bidhaa kwa viwango vinavyoridhisha.
Kwa mfano ukipaki parachichi wengine wataki upaki nne katika kifurushi na uweke alama zote muhimu kwenye kifurushi chako.
Maparachichi yanahitajika sana lakini ukumbuke washindana na wazalishaji wa nchi zingine hivyo uwe smart.
Bidhaa kama Viazi ni haba kwa sasa khasa Uingereza ambapo jamaa zangu waliko pale wasema viazi vimeadimika.
Hivyo ukiwa Tanzania watakiwa kuwa na storage, na packaging yako iwe katika viwango na uweze kuwa wahifadhi viazi vya kuweka kwenye ubaridi frozen chips ambapo vyaweza kuingia moja kwa moja kwenye kikaangio.
Hizi biashara zipo maana wahindi, wachina na raia kutoka nchi zingine za Afrika kama Ghana na Nigeria hupeleka kule bidhaa kama mihogo, mchicha na mbogamboga zingine.
Ila kama ambavyo nimekuwa nikisema humu siku zote, hizi shughuli zatakiwa kuanzia kwanza nyumbani Tanzania kisha wajijenga na kuanza kusafirisha bidhaa hizo ndani ya nchi kisha waweka "base" ya wateja na baadae kuendelea nje ya nchi.
Lakini masuala kama kuvuna, kupakia, kufanya "labelling", kuwashirikisha shirika la viwango, na mamlaka zingine ni jambo la muhimu kabla hujasafirisha bidhaa nje.
Ila kwa sasa suala la ugonjwa wa UVIKO-19 limewapa sababu nchi nyingi za Ulaya na Marekani kutumia nafasi hiyo kuzinyanyasa nchi maskini nyingi zikiwa za Afrika kwa kuziweka katika orodha jhyekundu au RED LIST.
Hiyo yaleta taabu kwa kiasi kikubwa kwani ni wale wenye fedha na matajiri ndo watoweza kujitenga mahotelini kwa gharama za kwao.
Uko sawa kabisa mkuu! Canada wanacaluclate marks ukikidhi hivi vigezo unakuwa kwenye nafasi nzuri zaidiKuna vigezo vingi wanaangalia hiyo ya experience ni kigezo kimoja wapo kisha wanacalculate credits.
Baadhi ya vigezo ni;
Education level
Experience
Age
Language profficiency(English/French)
Yes ni jambo zuri sana maana kampuni nyinine za nje hziz cv zetu format yake hawazielewi kabisa ..oi ma bro naombeni mnisaidie kutengeneza cv
Yeah ukiwa na 3.6millions Dubai unaenda kabisa mkuu. Huko ni kupambana tu hakuna kuchagua kazi kabisa mkuupamoja sana OllaChuga Oc
unaweza nisaidia ni mambo gani ya kufanya kabla ya kukanyaga uarabuni?
kuanzia ubalozini kwao, napaswa kuwa na kiasi gani cha fedha.
do and don't za huko diaspora.
vp kuhusu ubalozini wanatoa visa ya muda gani?Yeah ukiwa na 3.6millions Dubai unaenda kabisa mkuu. Huko ni kupambana tu hakuna kuchagua kazi kabisa mkuu
mtamba bView attachment 1892671
View attachment 1892672
Royal Caribbean cruise ship..
Meli za kitalii zinazosafiri nchi mbali mbali port of entry..
Unaweza kuapply kama unapenda kusafiri majini.. kutoka nchi m9ja kwenda nchi nyingine!
Zina hotels, malls- maduka, restaurants, n.k
Hii hapa chini ni website yao ya nafasi za kazi waazotoa unawe,a kuapply..
Kuwa makanini na websites nyingine zinazofanana na hiyo juu, usije tapeliwa, interview zao wanafanya kwa skype na hautaombwa pesa yoyote kutoka kwao
Angalia Department unayofit , then tengeneza C.V/ RESUMe pamoja na cover letter nzuri...
Hahahaha Achana na cv zetu za kibongo izi za kuandika marital status na primary school!!
Kikwazo ni IELTS mkuu ni gharama sana.Hongera Mkuu kwa kuanzisha huu uzi.
Nitajitahidi kudondosha ninazokutana nazo. Kwa mfano, kwenye huu ukurasa unakupa link za fursa za masomo na tafiti katika nchi za Umoja wa Ulaya:
Hizi ni fursa zinazotolewa na Australia:
Scholarships to study in Australia
Kuna fursa nyingi sana, na inasikitisha sana jinsi watanzania wachache sana hutumia hizi fursa ukilinganisha na mataifa mengine.
Ni kweli Mkuu. Ila kuna mitihani ya umahiri wa lugha ya kiingereza (English Proficiency Tests) inayotolewa na UDSM ambayo gharama zake ni chini zaidi. Ila lazima pia uangalie kama mitihani na cheti utakachopata vinatambuliwa na chuo au fursa utakazotuma maombi.Kikwazo ni IELTS mkuu ni gharama sana.
Inategemea unataka CV ya aina gani na kwa matumizi gani:oi ma bro naombeni mnisaidie kutengeneza cv
Cc: Myahudi Jr IIAsante kwa tag, naomba mwenye taarifa ya namna ya kuingia Canada au mchongo wa wazi anijuze l...nasema wa wazi mfano kupitia scholarship etc. maana siku hizi kupigwa kwingi
Ni kweli kwasasa baadhi ya byuo wanaangalia kama ulisoma bachelor na lugha iliyotumika kufundishia ni kiingereza basi unakuwa unakidhi vigezoNi kweli Mkuu. Ila kuna mitihani ya umahiri wa lugha ya kiingereza (English Proficiency Tests) inayotolewa na UDSM ambayo gharama zake ni chini zaidi. Ila lazima pia uangalie kama mitihani na cheti utakachopata vinatambuliwa na chuo au fursa utakazotuma maombi.
Vilevile, kipindi hiki cha janga la UVIKO, kuna baadhi ya nchi na vyuo vimeondoa uthibitisho wa umahiri wa lugha kama shahada ya kwanza ulisomea kwa lugha ya kiingereza.
Usikate tamaa mkuu.
Canada: Scholarships for Non-CanadiansAsante kwa tag, naomba mwenye taarifa ya namna ya kuingia Canada au mchongo wa wazi anijuze l...nasema wa wazi mfano kupitia scholarship etc. maana siku hizi kupigwa kwingi
Binafsi, mimi sijakuelewa mkuu... andika tena pole poleMm natamani nipate permit ya resident na work permit huko canada
Yaani nipate ili nikiona nikiomba iwe rahis kupata kwasababu nina kibali cha makaz na cha kufanya kazi
Hii inawekana wakuu?