Fursa za Nje ya Nchi: Scholarship (kusoma), Ajira/kujiajirina Biashara/kuwekeza

Fursa za Nje ya Nchi: Scholarship (kusoma), Ajira/kujiajirina Biashara/kuwekeza

Unachokisema ni kweli. Lakini bafo inawezekana .. ni wewe tu na jinsi gani unchat na muhusika wako , kuna wayu akili hazijakuwa anachata na mchuchu anamuomba hela sasa utaachaje kuonekana tapeli hahahahaha
west african wametuharibia sana. Waafrica hatuaminiki kwa sababu ya tabia zao za kishenzi
 
Wakuu, njia ingine nzuri zaidi ya kutoka nje na kujitayarisha kuwa mfanyabiashara wa bidhaa.

Ila lazima uwe mfanyabiashara smart unaelewa biashara na masoko, sheria mbalimbali na viwango vya nchi husika na kadhalika.

Bidhaa nyingi Ulaya sasa hivi zimekuwa haba kutokana na masuala kama ugonjwa wa UVIKo-19 ambao umesababisha biashara nyingi ndogo kufa.

Kwa mfano waweza kuamua kuwa wasafirisha nje, bidhaa ambazo ni "hot cake" katika maduka ya huko kama maparachichi, na sasa hivi kama kule UK wanahitaji sana Viazi kwa ajili ya chips.

Suala ambalo wazungu siku zote wanataka ni viwango, kuanzia kuvuna hadi kupakia bidhaa kwa viwango vinavyoridhisha.

Kwa mfano ukipaki parachichi wengine wataki upaki nne katika kifurushi na uweke alama zote muhimu kwenye kifurushi chako.

Maparachichi yanahitajika sana lakini ukumbuke washindana na wazalishaji wa nchi zingine hivyo uwe smart.

Bidhaa kama Viazi ni haba kwa sasa khasa Uingereza ambapo jamaa zangu waliko pale wasema viazi vimeadimika.

Hivyo ukiwa Tanzania watakiwa kuwa na storage, na packaging yako iwe katika viwango na uweze kuwa wahifadhi viazi vya kuweka kwenye ubaridi frozen chips ambapo vyaweza kuingia moja kwa moja kwenye kikaangio.

Hizi biashara zipo maana wahindi, wachina na raia kutoka nchi zingine za Afrika kama Ghana na Nigeria hupeleka kule bidhaa kama mihogo, mchicha na mbogamboga zingine.

Ila kama ambavyo nimekuwa nikisema humu siku zote, hizi shughuli zatakiwa kuanzia kwanza nyumbani Tanzania kisha wajijenga na kuanza kusafirisha bidhaa hizo ndani ya nchi kisha waweka "base" ya wateja na baadae kuendelea nje ya nchi.

Lakini masuala kama kuvuna, kupakia, kufanya "labelling", kuwashirikisha shirika la viwango, na mamlaka zingine ni jambo la muhimu kabla hujasafirisha bidhaa nje.

Ila kwa sasa suala la ugonjwa wa UVIKO-19 limewapa sababu nchi nyingi za Ulaya na Marekani kutumia nafasi hiyo kuzinyanyasa nchi maskini nyingi zikiwa za Afrika kwa kuziweka katika orodha jhyekundu au RED LIST.

Hiyo yaleta taabu kwa kiasi kikubwa kwani ni wale wenye fedha na matajiri ndo watoweza kujitenga mahotelini kwa gharama za kwao.
Mkuu, Vibali gani inahitajika kuwa na vyo ili uweze ku export bidhaa nje?

Namna gani unaweza kupata masoko/wateja nchi za nje?
 
Kuna vigezo vingi wanaangalia hiyo ya experience ni kigezo kimoja wapo kisha wanacalculate credits.
Baadhi ya vigezo ni;
Education level
Experience
Age
Language profficiency(English/French)
Uko sawa kabisa mkuu! Canada wanacaluclate marks ukikidhi hivi vigezo unakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi
 
oi ma bro naombeni mnisaidie kutengeneza cv
Yes ni jambo zuri sana maana kampuni nyinine za nje hziz cv zetu format yake hawazielewi kabisa ..
Mtu anaorodhesjha hadi primary school wakati ana level nyingj kubwa tu za elimu na skills..

Marital status , dini..

Kiufupi zjnakuwa n information nyingi ambazo haya makampuni hayaiziitaji kabla hawajakupatia kazi
 
Asante kwa tag, naomba mwenye taarifa ya namna ya kuingia Canada au mchongo wa wazi anijuze l...nasema wa wazi mfano kupitia scholarship etc. maana siku hizi kupigwa kwingi
 
Asante kwa tag, naomba mwenye taarifa ya namna ya kuingia Canada au mchongo wa wazi anijuze l...nasema wa wazi mfano kupitia scholarship etc. maana siku hizi kupigwa kwingi
Level ya Masters/phd ?
 
View attachment 1892671

View attachment 1892672

Royal Caribbean cruise ship..
Meli za kitalii zinazosafiri nchi mbali mbali port of entry..
Unaweza kuapply kama unapenda kusafiri majini.. kutoka nchi m9ja kwenda nchi nyingine!

Zina hotels, malls- maduka, restaurants, n.k

Hii hapa chini ni website yao ya nafasi za kazi waazotoa unawe,a kuapply..


Kuwa makanini na websites nyingine zinazofanana na hiyo juu, usije tapeliwa, interview zao wanafanya kwa skype na hautaombwa pesa yoyote kutoka kwao

Angalia Department unayofit , then tengeneza C.V/ RESUMe pamoja na cover letter nzuri...

Hahahaha Achana na cv zetu za kibongo izi za kuandika marital status na primary school!!
mtamba b
 
Hongera Mkuu kwa kuanzisha huu uzi.

Nitajitahidi kudondosha ninazokutana nazo. Kwa mfano, kwenye huu ukurasa unakupa link za fursa za masomo na tafiti katika nchi za Umoja wa Ulaya:

Hizi ni fursa zinazotolewa na Australia:
Scholarships to study in Australia

Kuna fursa nyingi sana, na inasikitisha sana jinsi watanzania wachache sana hutumia hizi fursa ukilinganisha na mataifa mengine.
Kikwazo ni IELTS mkuu ni gharama sana.
 
Kikwazo ni IELTS mkuu ni gharama sana.
Ni kweli Mkuu. Ila kuna mitihani ya umahiri wa lugha ya kiingereza (English Proficiency Tests) inayotolewa na UDSM ambayo gharama zake ni chini zaidi. Ila lazima pia uangalie kama mitihani na cheti utakachopata vinatambuliwa na chuo au fursa utakazotuma maombi.

Vilevile, kipindi hiki cha janga la UVIKO, kuna baadhi ya nchi na vyuo vimeondoa uthibitisho wa umahiri wa lugha kama shahada ya kwanza ulisomea kwa lugha ya kiingereza.

Usikate tamaa mkuu.
 
oi ma bro naombeni mnisaidie kutengeneza cv
Inategemea unataka CV ya aina gani na kwa matumizi gani:

1. Kama ni ya kawaida tumia Microsoft Word au hata LinkedIn zinakupa muongozo wa kinachohitajika kuandaa CV. Ukimaliza inakutengenezea hapo hapo.
Kama unataka CV zenye madoido na nakshi za kileo: Hizi ni programu mahiri za kuandaa:
Best CV builders in 2021
  • Resume.com.
  • ResumUP.
  • CakeResume.
  • Reed.co.uk.
  • Novoresume.
  • ResumeHelp.
  • CVmaker.
  • VisualCV.

2. CV zozote unaandaa kutokana na matumizi. Kama unaomba kazi hakikisha unaweka taarifa itakayohitajika na ofisi au kazi unayoiombea. Usitumie CV moja kuomba kila aina ya kazi.

3. Hakikisha CV yako ni rahisi kuelewa bila kuweka vifupi au maneno magumu, isipokuwa kama unauhakika atakayeisoma ataelewa. CV zenye taarifa nyingi zinashauriwa kwa watu wanaowasilisha kwaajili ya consultancy. Kama ni maombi ya kazi, usiweke CV ndefu sana, kurasa mbili zinatosha kabisa.
 
Ni kweli Mkuu. Ila kuna mitihani ya umahiri wa lugha ya kiingereza (English Proficiency Tests) inayotolewa na UDSM ambayo gharama zake ni chini zaidi. Ila lazima pia uangalie kama mitihani na cheti utakachopata vinatambuliwa na chuo au fursa utakazotuma maombi.

Vilevile, kipindi hiki cha janga la UVIKO, kuna baadhi ya nchi na vyuo vimeondoa uthibitisho wa umahiri wa lugha kama shahada ya kwanza ulisomea kwa lugha ya kiingereza.

Usikate tamaa mkuu.
Ni kweli kwasasa baadhi ya byuo wanaangalia kama ulisoma bachelor na lugha iliyotumika kufundishia ni kiingereza basi unakuwa unakidhi vigezo
 
Asante kwa tag, naomba mwenye taarifa ya namna ya kuingia Canada au mchongo wa wazi anijuze l...nasema wa wazi mfano kupitia scholarship etc. maana siku hizi kupigwa kwingi
Canada: Scholarships for Non-Canadians

Ni rahisi kuhakiki taarifa yoyote kuhusu fursa katika nchi nyingine kupitia balozi zao. Siku zote kama una mashaka na fursa tuma email kwa ubalozi wao nchini au ubalozi wenye uwakilishi wa hiyo nchi na watakuhakikia. Ni moja ya jukumu lao pia.
 
Mm natamani nipate permit ya resident na work permit huko canada
Yaani nipate ili nikiona nikiomba iwe rahis kupata kwasababu nina kibali cha makaz na cha kufanya kazi
Hii inawekana wakuu?
 
Mm natamani nipate permit ya resident na work permit huko canada
Yaani nipate ili nikiona nikiomba iwe rahis kupata kwasababu nina kibali cha makaz na cha kufanya kazi
Hii inawekana wakuu?
Binafsi, mimi sijakuelewa mkuu... andika tena pole pole
 
Back
Top Bottom