kaka samahani naomba kama hutojali unielezee kwa kirefu kuhusiana na visa vya semiramis na nimrod
Nimrodi ni mjukuu wa Ham mtoto wa Nuhu.Alikuwa ni mtuhodari sana na muwindaji mahiri sana.Vyanzo vingine vinaeleza kwamba,kwasababu ya watu kuanza kuenea baada ya gharika na wanyama kuazaliana kuliibuka kitisho kwa binadamu wa eneo la Babeli la kudhuriwa na wanyama wakati na Nimrod alikuwa akipambana na wanyama vilivyo na kuwa mtu muhimu sana katika jamii iliyomzunguka...
Alianza kua mtawala wa Babel hadi Ninawi na maeneo mengine ya jirani.Alimuoa Semiramis ambaye vyanzo vingine vinasema kwamba alikuwa ni mama yake.Alianzisha dini ya kuabudu sayari ambayo ilikuwa maarufu sana maeneo mengi ya dunia baadaye.Imani hii aliipata baada ya kuwasiliana na viumbe wa roho ambao ni wale malaika walioasi.Dini hii ilikuwa maarufu sana katika Babeli....
Baada ya watu kuwa wengi aliamua kujenga mnara ambao kama itatokea tena gharika basi watu wasife.Alijenga mnara mkubwa sana ambao ulikuwa ni mnara mrefu zaidi duniani kwa wakati ule.Pia hakutaka watu wasambae duniani kote bali wabaki pale pale ili kujenga jamii moja na yenye nguvu ikiwa na dini moja.Maelekezo yote haya aliyapata kutoka kwa malaika waasi ambao alikuwa akiwasiliana nao kwa njia mbali mbali kama vile maono na ndoto....
Dhana hii ya kuunda jamii moja yenye nguvu inayozungumza lugha moja na yenye dini moja ndiyo ipo hadi leo na ndiyo maana hata jengo la umoja wa ulaya limejenga likionekana halijamaliziwa wakimaanisha kudhamiria kukamilisha alichoshindwa kukikamilisha Nimrod.Pia,kitendo kilichotokea sept 11 kule Marekani ni ishara ya kuondoa mamlaka mbili zilizokuwa zikishindana na kubakisha moja ya shetani na ndiyo maana likajengwa jengo moja tu na likaitwa One World Trade center...
Turudi kwa Nimrod..
Babu yake ambaye ni Ham hakufurahishwa na imani hii,aliamua kumuua mwanae huyu na kumkatakata vipande vipande na kuvisambaza katika maeneo yote aliyokuwa akitawala Nimrod na kutoa agizo kuwa yoyote atakayeendelea kufanya ibada alizokuwa anazifanya Nimrod basi atafanywa kama kiongozi wao alivyofanywa...
Suala hili liliwafanya wakazi wa Babel wakaogopa lakini kwa muda tu.Mkewe Nimrod ambaye ni Semiramis alikusanya vipande vya mwili wa mumewe na kuvizika lakini kiungo cha uzazi cha Nimrod hakikupatikana na Semiramis akasema kuwa Nimrod amepaa kwenda kuishi juu na alama yake ni jua [Sun] na tangia hapo alama ya Jua ikawa ni alama ya Nimrod na akaanza kuabudiwa kama mungu na ndipo ibada ya kuabudu jua ilivyoanza na ikaonekana kuwa kiungo cha uzazi ni kitakatifu hivyo wakakitengenezea alama ya kukiheshimu kama alama ya imani yao na ndipo ilipotengenezwa Obelsk..
Obelisk hizi zipo maeneo mengi sana duniani kama vile St. Peter's square kule Vatican,Washingnton DC,Paris,Ufaransa na maeneo mengi kuonesha ni imani gani waliyonayo...
Baada ya miaka kupita Semiramis alipata ujauzito kwa namna ambayo hadi leo haijulikani lakini yeye akasema kwamba alikuwa amekwenda kumtembelea Nimrod mawinguni na akampatia ujauzito kwa njia ya ajabu hivyo hata atakachokizaa kitakuwa ni kitakatifu.Baada ya muda alimzaa mwana aliyejulikana kama Tamuz....
Tamuz,kama alivyokuwa "baba yake" naye alikuwa muwindaji mahiri sana lakini alikuja kuuawa na nguruwe pori siku ya ijumaa na waumini wa dini ile wakaamua kila ikifika ijumaa hiyo kwenye mwaka walikuwa hawali nyama kabisa kuenzi kifo cha Tamuz.Tamuz alichukuliwa kama |mwana wa mungu" [son of god] kwasababu ya maelezo ya mama yake ambaye alisema kuwa alikwenda mawinguni na kupewa ujauzito na Nimrod hivyo naye wakawa wanamuabudu...
Semiramis alikuja kufa na waumini wake waliamini naye kama ilivyokuwa Nimrod alikuwa ameenda kuishi na mumewe mawinguni na kuanzia hapo alama yake ikawa ni mwezi,mwezi ukawa kama mke na jua likawa kama mume kwakuwa lilikuwa linawakilisha watu hao muhimu mawili katika imani ya Babeli na ndipo ilipozaliwa ibada ya kuabudu vitu hivyo na kuviweka kwenye majumba ya ibada.....
Walitengeneza utatu wao ambao ulikuwa ni wa Nimrod,Semiramis na Tamuz,semiramis akajulikana kama malkia wa mbingu [queen of heaven]
Baadaye ilipoanguka mamlaka ya Babeli imani hiyo ilisambaa duniani kote na watu hao watatu walikuwa wakiabudiwa kwa majina tofauti tofauti.Mfano kule Misri waliitwa Isis [Semiramis] Osiris [Nimrod] Horus [Tamuz]....
Ni hayo kwa ufupi sana mkuu...