Fuvu na Mifupa(Skull and Bones) Jamii ya Siri ya Kishetani inayoongoza Matukio ya Duniani

Me Eiyer namkubali sana, tatizo lake anajua vitu vingi lakini apendi kuvitoa.
 
Me Eiyer namkubali sana, tatizo lake anajua vitu vingi lakini apendi kuvitoa.
Mkuu unajua kama hujui haya mambo unaweza kudhani ni rahisi tu kuyasema.Hapa sizungumzii labda hofu bali namna mambo yenyewe yalivyo,ili uweze kuandika kwa mtiririko mzuri na unaoweza kueleweka ni jambo litakalokufanya utumie muda mrefu sana labda uwe unaelezea vijikundi kama huyu mtoa mada kitu ambacho kwangu mimi naona siyo sahihi kwasababu tunakuwa tunaangukia kwenye mtego wa hawa watu maana wameandaa vijikundi hivi ili ku mislead watu wanaotaka kujua watu hao ni akina nani maana vijikundi hivi havitakufikisha popote ukiamua kuvifuatilia,nafahamu ninachokisema...

Labda pa kuanzia ni kuanza namna binadamu alivyoanza maisha kule Eden na kile kilichotokea kuanzia hapo huenda inaweza kuwa point ya maana kuliko kuanza na KKK au Theosophical society au Rosicrucian maana tutakuwa tunaanza kusafisha matairi ya gari wakati tulipaswa tuanze ndani kwenye viti kisha tule nje kwenye bodi kisha ndiyo tumalizie matairi...

Ndiyo maana post yangu ya kwanza tu katika mada hii imeonekana kama ni hasi au nimedharau alichokifanya Guru wakati sikuwa na maana hiyo.Pia,naona Guru amejiunga JF mwaka huu na inawezekana hafahamu mengi ambayo yameshajadiliwa hapa lakini kimsingi haya mambo tulishayajadili sana,tafuta uzi upo hapahapa Intelligence unahusu familia mbili kubwa na tajiri duniani,Rockerfeller [Rock Feller] na Rothschild [Rock shield] utaona mengi sana na usione uvivu kusoma maana ni mada ndefu sana nadhani ni ya mwaka 2012 hivi....

Nainatumai utaelewa mengi sana mule maana wapo watu waliojitokeza na kusema mengi sana ambayo ni muhimu hasa mkuu mmoja anaitwa Juve2012...
 
Asante mkuu kwakunifungua macho tuko pamoja.
 
Mkuu hebu tumegee kidogo juu ya kupotea kwa hilo bara la Atlantis,na kwann wanataka lirudi?...umegusia sananda na saint kumara ni nani hawa?mkuu Eiyer mwaga vitu tupate elimu
 
Dah! We jamaa noma umenifanya mpaka nimewaamsha watoto kwa kucheka kkkkkkkkkk ,Pwani oyeeee
Nalog off
 
Mkuu hebu tumegee kidogo juu ya kupotea kwa hilo bara la Atlantis,na kwann wanataka lirudi?...umegusia sananda na saint kumara ni nani hawa?mkuu Eiyer mwaga vitu tupate elimu
Nitajitahidi kufupisha kwa namna nitakavyoweza ili nisiandike maandishi mengi japokuwa siyo jambo zuri maana kuna mengine hutayajua...

Bara la Atlantis ni bara lililokuwa kwenye bahari ya atlantic baina ya bara ulaya na Amrerica ya kaskazini.Bara hili lilijulikana kama kitovu cha maendeleo duniani na wakati huo dunia ilikuwa na maendeleo makubwa mara kumi ya sasa.Jambo hili linafichwa sana kwa sababu maalum.Bara hili waliishi magiant [Nephilims] ambao waliendesha utawala duniani utawala ambao ulimuumiza sana binadamu wa kawaida.Kulikuwa kukifanyika kafara za binadamu na viungo vya binadamu vilikuwa vikitumika kwa shughuli mbali mbali za nguvu za giza.Ilifikia mahali damu ya binadamu ilikuwa ikitumika kama kinywaji cha kawaida kwa hawa viumbe..

Unaweza kujiuliza hawa Nephilim ni nani au akina nani.Nephilims ni viumbe ambao walikuwa nusu binadamu na nusu malaika ambao walipatikana baada ya malaika waasi kufanya ngono na wanawake wanadamu.Malaika waasi ndiyo waliowafundishwa wanadamu elimu za unajimu,utoaji wa mimba,kutengeneza silaha na teknolojia nyinginezo ambazo ni za hali ya juu sana.Binadamu baana ya kupata ujuzi huu walianza kuuana wao kwa wao na ndipo Mungu alipoingilia kati na kuleta gharika lililowasambaratisha viumbe wote na kuwasalimisha walioingia kwenye safina...

Maisha ya wakati huu yalikuwa ya kishetani haswa.ni maisha ya kutisha sana maana binadamu alikuwa akiishi kama vile mbuzi leo maana alikuwa akiwindwa vilivyo hadi pale ambapo Mungu alipoamua kuingilia kati.Anayetaka kulirudisha bara hili na ustaarabu ule ni Semjaza,miongoni mwa malaika wakuu walioasi wanataka kuuleta ufalme wao hapa duniani wakishirikiana na binadamu wachache wasiojua ukweli na wanaoujua wachache sana lakini kwa umakini na udanganyifu mkubwa sana wa kisayansi....

Wanataka watawale dunia na jambo hili litatokea siyo miaka mingi kutokea sasa maana wanamalizia tu na wanataka kuwaleta tena hao malaika kutoka walipo kupitia kinachoendelea kule kwenye mitambo yao ya LHC [Large Hadron Collider] kwenye project yao maarufu ya Cern ambapo wanataka kufanya kitu ambacho dunia haitakuja kusahau kamwe...


LHC

Sananda ni kiumbe wa roho ambaye anajifananisha na Yesu,picha inayotumika kwenye makanisa na ambayo watu wanaamini kuwa ni ya Yesu ni ya Sananda,kuna mengi kumhusu huyu lakini kwa hapa inatosha kusema hivyo.Watu wanadai ni picha ya Cecare Borgia lakini ukweli ni kwamba ni picha ya Sananda.Kiumbe huyu ni miongoni mwa wale malaika waasi na huyu atatumika kudanganya watu wakati watakapo fake ujio wa Yesu.....


Sananda...

Sanat Kumara ni Azazel ambaye hujulikana kama Satan Kumara maana jina lake la kwanza limebadilishwa tu herufi.Huyu inasemekana ni Shetani mwenyewe au ni second in command kwenye himaya yao hawa malaika waasi....

Nadhani nimekupa mwanga angalau kidogo....
 
Ahsante mkuu ,umenipa mwaga,km kuna nyongeza nitarudi ,namupitia kumsoma huyu Pindar na wenzake
 
Wakuu Guru Master na "Eiyer, umenipa somo murua sn. nimeanza kuwafatilia hawa watu since september 2009, lakini sikutaka jitanua zaidi ya freemason. na kweri nilikua mahili miongoni mwa wezangu, kumbe hata shule ya vidudu kuwajua hawa watu nilikua sijaanza. I see asante sana Mkuu. plse niongeze kwa tag list yako in case utatoa andiko kuwahusu hawa wapinga Kristu.
 
kaka samahani naomba kama hutojali unielezee kwa kirefu kuhusiana na visa vya semiramis na nimrod
 
kaka samahani naomba kama hutojali unielezee kwa kirefu kuhusiana na visa vya semiramis na nimrod
Nimrodi ni mjukuu wa Ham mtoto wa Nuhu.Alikuwa ni mtuhodari sana na muwindaji mahiri sana.Vyanzo vingine vinaeleza kwamba,kwasababu ya watu kuanza kuenea baada ya gharika na wanyama kuazaliana kuliibuka kitisho kwa binadamu wa eneo la Babeli la kudhuriwa na wanyama wakati na Nimrod alikuwa akipambana na wanyama vilivyo na kuwa mtu muhimu sana katika jamii iliyomzunguka...

Alianza kua mtawala wa Babel hadi Ninawi na maeneo mengine ya jirani.Alimuoa Semiramis ambaye vyanzo vingine vinasema kwamba alikuwa ni mama yake.Alianzisha dini ya kuabudu sayari ambayo ilikuwa maarufu sana maeneo mengi ya dunia baadaye.Imani hii aliipata baada ya kuwasiliana na viumbe wa roho ambao ni wale malaika walioasi.Dini hii ilikuwa maarufu sana katika Babeli....

Baada ya watu kuwa wengi aliamua kujenga mnara ambao kama itatokea tena gharika basi watu wasife.Alijenga mnara mkubwa sana ambao ulikuwa ni mnara mrefu zaidi duniani kwa wakati ule.Pia hakutaka watu wasambae duniani kote bali wabaki pale pale ili kujenga jamii moja na yenye nguvu ikiwa na dini moja.Maelekezo yote haya aliyapata kutoka kwa malaika waasi ambao alikuwa akiwasiliana nao kwa njia mbali mbali kama vile maono na ndoto....

Dhana hii ya kuunda jamii moja yenye nguvu inayozungumza lugha moja na yenye dini moja ndiyo ipo hadi leo na ndiyo maana hata jengo la umoja wa ulaya limejenga likionekana halijamaliziwa wakimaanisha kudhamiria kukamilisha alichoshindwa kukikamilisha Nimrod.Pia,kitendo kilichotokea sept 11 kule Marekani ni ishara ya kuondoa mamlaka mbili zilizokuwa zikishindana na kubakisha moja ya shetani na ndiyo maana likajengwa jengo moja tu na likaitwa One World Trade center...

Turudi kwa Nimrod..
Babu yake ambaye ni Ham hakufurahishwa na imani hii,aliamua kumuua mwanae huyu na kumkatakata vipande vipande na kuvisambaza katika maeneo yote aliyokuwa akitawala Nimrod na kutoa agizo kuwa yoyote atakayeendelea kufanya ibada alizokuwa anazifanya Nimrod basi atafanywa kama kiongozi wao alivyofanywa...

Suala hili liliwafanya wakazi wa Babel wakaogopa lakini kwa muda tu.Mkewe Nimrod ambaye ni Semiramis alikusanya vipande vya mwili wa mumewe na kuvizika lakini kiungo cha uzazi cha Nimrod hakikupatikana na Semiramis akasema kuwa Nimrod amepaa kwenda kuishi juu na alama yake ni jua [Sun] na tangia hapo alama ya Jua ikawa ni alama ya Nimrod na akaanza kuabudiwa kama mungu na ndipo ibada ya kuabudu jua ilivyoanza na ikaonekana kuwa kiungo cha uzazi ni kitakatifu hivyo wakakitengenezea alama ya kukiheshimu kama alama ya imani yao na ndipo ilipotengenezwa Obelsk..

Obelisk hizi zipo maeneo mengi sana duniani kama vile St. Peter's square kule Vatican,Washingnton DC,Paris,Ufaransa na maeneo mengi kuonesha ni imani gani waliyonayo...

Baada ya miaka kupita Semiramis alipata ujauzito kwa namna ambayo hadi leo haijulikani lakini yeye akasema kwamba alikuwa amekwenda kumtembelea Nimrod mawinguni na akampatia ujauzito kwa njia ya ajabu hivyo hata atakachokizaa kitakuwa ni kitakatifu.Baada ya muda alimzaa mwana aliyejulikana kama Tamuz....

Tamuz,kama alivyokuwa "baba yake" naye alikuwa muwindaji mahiri sana lakini alikuja kuuawa na nguruwe pori siku ya ijumaa na waumini wa dini ile wakaamua kila ikifika ijumaa hiyo kwenye mwaka walikuwa hawali nyama kabisa kuenzi kifo cha Tamuz.Tamuz alichukuliwa kama |mwana wa mungu" [son of god] kwasababu ya maelezo ya mama yake ambaye alisema kuwa alikwenda mawinguni na kupewa ujauzito na Nimrod hivyo naye wakawa wanamuabudu...

Semiramis alikuja kufa na waumini wake waliamini naye kama ilivyokuwa Nimrod alikuwa ameenda kuishi na mumewe mawinguni na kuanzia hapo alama yake ikawa ni mwezi,mwezi ukawa kama mke na jua likawa kama mume kwakuwa lilikuwa linawakilisha watu hao muhimu mawili katika imani ya Babeli na ndipo ilipozaliwa ibada ya kuabudu vitu hivyo na kuviweka kwenye majumba ya ibada.....

Walitengeneza utatu wao ambao ulikuwa ni wa Nimrod,Semiramis na Tamuz,semiramis akajulikana kama malkia wa mbingu [queen of heaven]

Baadaye ilipoanguka mamlaka ya Babeli imani hiyo ilisambaa duniani kote na watu hao watatu walikuwa wakiabudiwa kwa majina tofauti tofauti.Mfano kule Misri waliitwa Isis [Semiramis] Osiris [Nimrod] Horus [Tamuz]....

Ni hayo kwa ufupi sana mkuu...
 
mimi naona kama kuna Ibada inayoweza kumpa mtu utajiri, haiba,kukubalika na jamii, power na mali halafu usidhuruke mwili wala kudhuru wengine inafaa. Bora tu hao kwa sababu kila binadamu anataka afya, utajiri, madaraka , mali, haiba na kukubalika. Maisha ni hapa hapa duniani kwingine ni imani tuu.
 
Umepapasa tu kuhusu ukweli wa dunia na anayeiendesha....

Endelea kujifunza na utajua hao Skull and Bones ni sisimizi tu,hata Freemason na Illuminati ni sisimizi tu...

Jifunze kuhusu Pindar utapata mwanga kidogo....
Mkuu away from Google una source yeyote ile inaweza upload
 
Asante kwa lishe
 
Mkuu dondosha vitu wengine tupo ñyuma yako tatizo lugha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…