Fuvu na Mifupa(Skull and Bones) Jamii ya Siri ya Kishetani inayoongoza Matukio ya Duniani

Vp kuhusu Aliens mkuu? Wanajihusisha na hizi societies au hawana mpango na kucontrol dunia?
Baadhi ya vyanzo vya habari vinasema kwamba Aliens wanakuja kutoka nje ya dunia lakini hiyosiyo kweli.Aliens wapo hapa na hawajawahi kutoka nje ya dunia na hawajawahi kuja kutoka nje ya dunia hata mara moja...

Aliens ni viumbe ambao walitengenezwa mahususi na fallen angels kuwasaidia binadamu katika sayansi ili binadamu awe na uwezo fulani hivi kwasababu maalum....

Aliens wapo kwenye D.U.M.Bs [Deep Underground Military Bases] nyingi zilizoko maeneo mbali mbali duniani ambako kuna majiji makubwa hatari kabisa.robo tatu ya jiji la New York kwa mfano lipo juu ya jiji lingine lililoko chini ya ardhi.Ni watu wachache sana ambao wana access huko lakini majority ya walioko huko ni Aliens na wanafanya mambo mengi sana huko...

Kuna tren inayokwenda kasi kwa speed ya mwanga huko.Kuna majiji makubwa sana kuliko haya yaliyoko huku juu.Kuna silaha za hatari kabisa huko kiasi kwamba huwezi kuamini kama kuna silaha za namna hiyo.Jamaa wana choper ambayo inaweza kuruka umbaliwa mita 3000 hadi 6000 na bado ikaweza kujua ndani ya nyumba yako kuna nani na mko wangapi na wenye jinsia gani na jeshi la Marekani lina chper hizi 60,000 lakini hazijaanza kutumika bado....

Kuna sayansi ya hatari huko acha kabisa na hii inafanywa na Aliens...

Hatuko salama kabisa kama tunavyodhani....
 
Majibu yapo ukitakakuyapata lakini unatakiwa utoke jasho...

Polesana naona umeogopa vitisho vya hawa watu kiasi kwamba umejikatia tamaa na hilo ndilo lengo lako....

Wake up,Mungu alishasema hakuna kilicho sirini ambacho hakitawekwa hadharani,hapa tunasaidiana tu kuuelewa ukweli ili utusaidie.....
 
samahani eiyer naomba pia kama hutojali unielezee hata kwa kifupi kuhusu Anunnaki race na secret war inayoendelea
 
Nimekuelewa vizuri sana mkuu, ulichoeleza ndio nilitaka kujua, thanks!
 
Mkuu Eiyer ningependa kujua hasa ya watu weusi kutokuhusishwa na hawa majamaa ukilink na Yesu kuwa mweusi
 
Duu hizi habari unazipata wapi na mimi nipitie ? Nione maajabu ya huo mji ambao upo chini ya New York
 
samahani eiyer naomba pia kama hutojali unielezee hata kwa kifupi kuhusu Anunnaki race na secret war inayoendelea
Anunnaki ni viumbe ambao siyo binadamu ambao waliitembelea dunia miaka mingi sana iliyopita na kuja kuwafundisha wanadamu mambo mengi sana ambayo hayakujulikana kabla na mwanadamu....

Kama utakumbuka nilisema kuwa malaika waasi walikuja na kuwafundisha wanadamu elimu ambayo hakuwa nayo.Walikuja na ujuzi wa hali ya juu sana na kusababisha mwanadamu awe na maendeleo ambayo yalishangaza sana.Jambo hili linafanana sana na ishu ya Anunnaki na hawa ni wale wale tu...

Kwa wale ambao ni wapagani kwa wakati ule waliwaita hivyo kwa kuwa hawakujua walipotoka,lakini pia waliabudiwa na ndipo ilipokuja dhana ya "gods" yaani miungu kwasababu walikuwa wengi.Sio hao tu,hata wale watoto wao waliowapata baada ya kuingiliana na wanadamu wanawake nao walikuwa wakiabudiwa...

Anunnaki walikuja duniani na walishukia mlima Hermon na leo kwenye kilele cha mlima huo kuna base ya UN...

Kuna dhana tofauti tofauti kuwahusu hao Anunnaki.Kwa mfano Zacharia Thitchin aliwaeleza kama viumbe waliofuata madini ya dhahabu duniani na ndiyo waliokuja hapa na kwakuwa walihitaji nguvu kazi kubwa walitengeneza au kuwaumba binadamu ili wawasaidie kuchimba dhahabu na ndipo baadaye binadamu walisaidiwa na baadhi ya Annunaki ambao hawakupenda binadamu kufanyishwa kazi....

Michael Tellinger naye ana dhana yake kuwahusu.Dhana ni nyingi sana lakini hazi make sense kwasababu zote hazielezei hao Annunaki walikuwa wakihitaji hiyo dhahabu ili iweje na waliihitaji kuipeleka wapi na kwanini huko kwao haikuwepo....

Ni kweli Anunnaki [fallen angels] ndiyo waliomfundisha binadamu matumizi ya madini mbali mbali na hata kule Afrika kusini yalishagundulika machimbo ya madini ya kale sana ambayo yaliwashangaza wengi.Annunaki ndiyo walijenga mapiramidi wakisaidiana na watoto wao Nephilims.Hao hao ndiyo waliojenga miji mitano ya mwanzo Marekani kwa line moja ikiwa sawa na line ya yale mawe maarufu huko Britany yanayojulikana kama "Stone age".Hii miji majina yamenitoka lakini ndiyo hivyo....

Kuna mengi sana kuwahusu hawa Anunnaki lakini kimsingi Anunnaki ni wale fallen Angels...
 
Elimu nzito sana hizi. Binafsi ningependa kuelimika juu ya hili suala la sisi watu weusi kuaminishwa kwamba sisi ni kizazi kilicholaanika mkuu. Ilhali kwenye baadhi ya maandiko ya kale na historia inaelezea tofauti kizazi cha watu weusi.
Naomba ufafanuzi kidogo mkuu Eiyer.
 
mhuuuuuu!
 
Mkuu Eiyer ningependa kujua hasa ya watu weusi kutokuhusishwa na hawa majamaa ukilink na Yesu kuwa mweusi
Kwanza unatakiwa ujue tu kuwa yote haya ni vita kati ya jeshi lililoangushwa hapa duniani la malaika waasi baada ya kuasi na jeshi la Mungu....

Binadamu wa kwanza alikuwa mweusi,hizi rangi tofauti unazoziona ni kwasababu ya dhambi,jambo hili lina maelezoyake marefu sana na tuliache kwa sasa....

Ibrahimu,Isaka,yakobo na wengine na hata wale Wamisri wa kwanza na wenyeji wote wa eneo linaloitwa mashariki ya kati leo walikuwa ni weusi kama sisi na eneo hilo lilifahamika kama North east Africa yaani ilikuwa ni sehemu ya Afrika....

Kwa maana hiyo Waisraeli walikuwa ni weusi kama mimi na wewe na ndiyo maana kuna vita kubwa ya kumfanya mtu mweusi awe duni kwasababu wanajua ukaribu wake na Mungu.Chosen people walikuwa na bado ni weusi na kuna ushahidi ni Wabantu....

Wanachokifanya ni kwamba wanataka kufuta au kukidhalilisha kizazi ambacho ndicho cha asili ya uumbaji wa Mungu....

Sijui kama nimeeleweka maana naandikahuku nafanya mambo mengine,utulivu siyo mzuri....
 
Duu hizi habari unazipata wapi na mimi nipitie ? Nione maajabu ya huo mji ambao upo chini ya New York
Soma vizuri mkuu ili uelewe...

Sijasema hizi D.U.M.Bs ni moja bali ziko nyingi maeneo mengi sana duniani na zinamuingiliano wa njia za reli na wanatumia treni za kisasa mara kumi kuliko hizi zilizoko huku juu duniani....
 
Soma hapo juu mkuu....
 
Soma vizuri mkuu ili uelewe...

Sijasema hizi D.U.M.Bs ni moja bali ziko nyingi maeneo mengi sana duniani na zinamuingiliano wa njia za reli na wanatumia treni za kisasa mara kumi kuliko hizi zilizoko huku juu duniani....
Nimekuelewa vizuri Mkuu ndio maana nikauliza napata wapi hizi habari ili nijisomee nikiwa na maana ya vitabu ama online libraries nk
 
Hawa watu hawawapendi sana watu weusi na hii ni kwasababu hata Yesu alikuwa mweusi,kuna mengi kwenye hili na tuliache kwa sasa...

Lakini wapo kwenye vyama hivi ila hawapo kwenye maeneo muhimu sana....
Mkuu yesu alikuwa mweusi ? tunaomba ufafanuzi kwa maana neno mtu mweusi siku hz hata Obama anaitwa mweusi wakati kiukweli si mweusi
 
Mkuu yesu alikuwa mweusi ? tunaomba ufafanuzi kwa maana neno mtu mweusi siku hz hata Obama anaitwa mweusi wakati kiukweli si mweusi
kuna mahali nimesema "alikuwa mweusi kama mimi na wewe" yaani na nywele kama kipilipili....

Nadhani umenielewa....
 
Umepapasa tu kuhusu ukweli wa dunia na anayeiendesha....

Endelea kujifunza na utajua hao Skull and Bones ni sisimizi tu,hata Freemason na Illuminati ni sisimizi tu...

Jifunze kuhusu Pindar utapata mwanga kidogo....
Tupe hiyo habari ya Pindar tupate mwangaza!
 
Naomba uitume tena mkuu hiyo chat sababu haisomeki vizuri tafadhali
 
Hapa naona umezidi mkuu, pamoja na watu kukusifu kwa uelewa wako wa haya mambo ila hapa hapana, siamini kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…