Gamondi ashauriwe aache kiburi na chuki binafsi kwa Wachezaji!

Aucho mnamuonea bure tu umri umeenda, wenzake wa rika lake wapo vijijini saizi ikifika jioni wanakusanyika wanapiga mbege huku wakiongea mawili matatu kuhusu mustakabali wao wa maisha kiujumla.
 
Hoja unayo ila Gongowazi wenzio watakushambulia.
 
ndio maana huwezi kuwa kocha kwa mawazo kama haya
 
Nilipomuona Boka kwa mara ya kwanza nilisema si Mchezaji wa kuichezea yanga na kuwa na productivity inayohitajika, huku jf nilichekwa nikadhihakiwa.

Nafasi ya Farid Mussa Malik ilikuwa azibe pengo la namba 3 mbadala wake awe Kibabage, Boka hana uwezo wa hawa watu wawili, kuhusu Azizi ki, anahitaji muda wa kupumzika kwa sasa acheze mechi kwa muda mchache msimu uliopita alifanya kazi kubwa sana amechoka, vivyohivyo kwa Aucho.

Katika safu ya ushambuliaji yanga ingekuwa na consistency ya kumchezesha mzize kama winger, Jean baleke center forward, maxi nzengeli winger.
Side ten yao pacome zozoua, kwenye sub uwe na Musonda, Dube, Chama na Azizi ki.

Unatwist kikosi vizuri na production ya magoal lazma iwe juu sana.
 
Boka haeleweki anakaba au anashambulia ye mda wote yuko marathon ya 100m.
Cross mbovu isipotoka, basi beki kablock au imevuka goal imeenda upande wa pili.

Hakabi hashambulii haeleweki.
 
Siku zote mvua ikinyesha ndiyo hukuonesha sehemu zinazovuja!! Mvua iheshimiwe kwa kutushtua ili tufanye ukarabati!! Kwa hiyo Azam aheshimiwe!! Kusema kweli yanga ya sasa ilikuwa ni suala la muda tu wananchi waanze kuvujiwa na mvua!! Ila tusifumbie macho ukweli kuwa ligi yetu ni ngumu sana na imeboreka sana!! Zile ndoto za Simba na Yanga kujizolea pointi 3 kila zinapokutana na timu nyingine zimeshapitwa na wakati!! Simba na Yanga wajiandae kisaikolojia kuangukia pua mara kadhaa!!
 
Una hoja sana,
Uliyoyaongea kila mtu anayaona, binafsI Naona uwezo wa Gamondi umefikia mwisho.
 
le Professeur Gamondi anawatumia tu haya magalasa yaliyookotwa na uongozi makini wa Uto.. Dube: Mechi 9, Magoli 0, Asist 0; Baleke: Mechi 4, Magoli 1 (la offside), Asist 0.
 
Reactions: Tui
Umeongea kama shabik wa kweli wa mpira wa miguu, sio takataka zingine humu wanaovimbishwa kichwa na msemaji wao alikamwe kwamba wajipigepige vifua na kutemmbea mbele na kuambiwa vimba mwananchi..
Mpira umebadilika , ligi inaenda kuimarika siku hadi siku, yale masuala ya kwamba unaenda kucheza na timu flani unaenda kujipigia magoli ya bwerere hakuna, wachezaji pamoja na makocha wanatumia mbinu, kuna mashushushu wa timu wako wanasoma wapinzan wao mechi zao wanazocheza na mbinu za mpira wanazotumia, wanajua kila mchezaji na stail yake anayocheza kiwanjani, mwanzon zilikuaga ni timu 2 tu zenye ushindani saiv zimeongezeka na zinaenda kuongezeka zaid, kwaio watu waache kuvimba na kunywa supu, wacheze mpira [emoji23]
 
Na wewe unaamini kabisa msimu huu Kwa Uchezaji huu wa Yanga Kuna kikombe watabeba?
Sio Kikombe nazungumzia Makombe ata takwimu zake zinaonyesha Gamond ni mwamba kabisa.
 
Mpira wa bongo raha yake ndio hii

Kocha anafanya kila anachoona kinafaa, akikosa matokeo ndio alaumiwe.

Mngeweza kweli kumvumilia hata Pep nyie? Maana yeye anaweza hata kumchezesha mzize namba 6.
 
Umeeleza vyema mkuu 🙏

Tupate wadhamini kidogo..
 
Boka anaweza akaaminiwa na kupewa majukumu mapya, ila siyo aina ya mchezaji wa kumuondoa Lomalisa, kwa kumleta Bokaa achukue nafasi ya Lomalisa, hakika Yanga wameikosea adabu familia ya soka.

Ni kweli, Aziz k alipaswa awekwe bench ili afanyie kazi kiwango chake, ni mchezaji mzuri sana lakini ninaamini kwa sasa ana mambo mengi ya nje ya uwanja na hii ni tangu msimu ulipoanza alivyokuwa akiambatanishwa na Hamisa Mobeto, ulikuwa ni upumbavu wa viwango vya juu sana kuruhusu hali ile.
Baleke anahitaji mfululizo wa mechi tatu, Mkude ni mchezaji aliye tayari muda wowote akipewa nafasi.

Sure boy na Farid Mussa wana majibu ya namna ya kuipatia ushindi Yanga hii ambayo watu ni kama wameshaisoma, na ndiyo maana timu yoyote ikicheza na Yanga sasa hivi, mechi hiyo lazima iwe na mvuto na timu kuonekana kali sababu hujitahidi kucheza katika mfumo maalum wa kucheza na Yanga na kwa kuwakariri zaidi wachezaji matokeo yake Max anazidi ku shine sababu kumfunika ni ngumu, kwanza ana kiwango, pia hachezi nafasi moja na ni lazima uwe na mapafu ya mmbwa na mbavu za mnyama kiboko.
 
Tuanze na hapa! Una taaluma ya ukocha mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…