Gamondi ashauriwe aache kiburi na chuki binafsi kwa Wachezaji!

Dube hapana kwa kweli. Bora angebaki Guede
Mfumo wa Yanga ulishaanza kumchezesha Guede, na yeye aliitika. Naamini dirisha dogo kuna mabadilishano yataanyika kuhusu Guede na Dube, ni vizuri Dube akafanyie kazi kiwango chake sehemu nyingine. Aziz K pia wangeangalia namna ya kumpeleka kwa mkopo katika moja ya Club kubwa zilizokuwa zikimhitaji, huenda ikamsaidia kuamka.
 
Mimi sio yanga lakini gamond tumpe maua yake,mechi nane kashinda bila kuruhusu bao hata Moja,alafu Kuna mtu anamlaumu?we sio mtu wa soka broo
Simlaumu Kwa kutokufungwa goli hata moja,namlaumu Kwa namna timu inavyocheza vibaya!

Kung'ang'ania wachezaji walewale tu hata kwenye mechi ambazo hazina presha!

Kutokufungwa Goli hata moja si kipimo Cha kocha Bora!
 
Mimi sio yanga lakini gamond tumpe maua yake,mechi nane kashinda bila kuruhusu bao hata Moja,alafu Kuna mtu anamlaumu?we sio mtu wa soka broo
Inawezekana kuna mahala amekosoa, lakini uchambuzi wake una logic sana na imeonyesha ni mtu wa soka hasa.
Gamond kama kocha ameshindwa kuzitumia vyema rasilimali alizo nazo, ingawa sehemu kubwa maswali inapaswa yaelekezwe kwa wachezaji.

Uvumilivu wa Gamondi ndiyo umempelekea Mzinze awe huyu tunayemuona, ni sababu alimpatia nafasi ambayo wengine hawapewi, pia kama kocha kwenye timu kubwa iliyopo kwenye mashindano, ni jukumu la wachezaji kugombania namba na siyo kocha kuwajaribu .
Pressure ni kubwa, ila nimefurahi kupoteza hii mechi kunaenda kuibadilisha Yanga
 
Watu wanapenda ligi iwe kama bundersliga kila siku Bayern tu
 
Mkude wa Yanga ni tofauti kabisa na yule wa Simba, Mkude amekuwa tofauti sana na yule wa kwenye story za Simba
 
Ngoja nami nikusidie hao wachezaji woote uliowataja kocha si kawakuta kwenye timu ,yeye Kuna vitu anaamini ndio mana yupo katika tim mpaka Leo,
 
Simlaumu Kwa kutokufungwa goli hata moja,namlaumu Kwa namna timu inavyocheza vibaya!

Kung'ang'ania wachezaji walewale tu hata kwenye mechi ambazo hazina presha!

Kutokufungwa Goli hata moja si kipimo Cha kocha Bora!
Poa,naheshimu mawazo yako lakini siyakubali
 
Watanzania wengi hatujui summarize maoni yetu. Tunaandika kitabu kizima kutoa maoni ambayo yangeweza kuwa paragraph moja tu, yaani sisi ni watu wa maneno mengi tena ya kuzunguka zunguka tu.
 
U
Naamini kwamba yanga pekee ndo inastahili kushinda?? Mbona huwasifii wapinzani kwa kujipanga vyema??

Maelezo mengi lakini hoja yako itajibiwa na maneno haya WAPINZANI NAO WAPO VIZURI MZIMU HUU NA WAMEJIPANGA VYEMA. YANGA HAKUNA GAME WALICHEZA VIBAYA NA UKUMBUKE SIKU HAZIFANANI. Mchezaji gani kachukiwa na kocha?? Je umefika kwenye mazoezi ukaona huyo mchezaji unayemtetea anamshawishi vipi kocha??
 
Endelea kuchunga ng'ombe huko Usukumani,Mpira tuachie watu wa mpira!
 
Reactions: Tui
Hapo kwa kibabage ni kweli tupu, wakati wa Lomalisa nilikua simuelewi kabisa ila huyu Boka hamna kitu kwa Kibabage dogo anatembea kwa akili, mipira yake ina madhara makubwa kwa wapinzani, na anawahi kurudi.

Dube amna kazi yule mtu, hamna kitu anafanya.
 
Unaonekana haumfatilii mleta mada kuna uzi wako alizungumza haya haya kabla yanga hajacheza na Azam.
 
Tumekuelewa MZIMU huu bila Marefa ungekuwa una matundu kuliko Chujio.
 
Yanga msimu uliopita alipoteza katika mechi ya nne tu... Lakini alikua kua bingwa...

Yanga hajashuka kiwango ila amebadili staili ya uchezaji na mtakuja kuelewa baadae sana..

Gamondi alichofanya ni timu kua ngumu sana hii itatusaidia kimataifa tusipoteze game kirahisi..

Yanga atakua bingwa hilo halina ubishi kama inshu n kufungwa na Azam kumbuka hata msimu uliopita bado Yanga alikandwa na Azam...

Huu Uzi nitaufufua May 2025 panapo majaliwa...

NB: kumuuza Lomalisa na kumleta Boka ni sawa na kuuza bunduki na kununua upinde
 
Baadhi ya ufafanuzi wako uko sahihi, hasa kuhusu kiwango cha Aucho na Dube. Ila kwa kocha na Aziz K natofautiana na wewe.

Mfumo wa kutumia "mshambuliaji" unamfanya Aziz K asifunge magoli kama ilivyokuwa wakati Mayele alipokuwa akicheza.

"Washambuliaji" waliokuwepo, hasa Dube, wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi za kufunga zinazotengenezwa na viungo washambuliaji, hasa Aziz K.

Ni wakati sasa wa kutumia viungo washambuliaji wa msimu uliopita (PAM - Pacome, Aziz K na Max) kuwatengezea nafasi za kufunga washambuliaji (Mzize + Baleke au Msonda + Dube) ambao mmoja nI hodari kufunga kwa miguu (Mzize/Dube) na mwingine kwa kichwa (Baleke/Msonda).

Kilichokea hivi majuzi ni udhaifu wa safu ya ulinzi (Mechi dhidi ya Azam kutolewa nje Bacca wa kadi nyekundu, na dhidi ya Tabora kukosekana kwa Bacca na Job).
 
Yanga ni ile ile ila wapinzani wamejifunza kucheza nae. Ni suala la muda Kocha asipojifunza kubadilika kimbinu atafungwa mfululizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…