Gari hizi trafiki wanazipenda kuzipiga mkono

Ist now bampa kubwa 22m
Wakati hapo ukiongeza 3m unapata dualis chases no au ukiongeza 7m unapata outlander
 
Toyo sijui ziliwakosea nini trafiki,yan ikikatiza mbele yao lazima waisimamishe!
 
Suzuki Jimmy gari za Afsa Watendaji wa Mitaa😫😂
 
Colora = X
Corolla = 👍
 
Bila kusahau kirikuu
Kwan kili kuu sio canter?? Ukizungumzia Canter umetaza magari aina ya kilikuu yote mkuu, maana hamna brand inayoitwa kili kuu, wanaita Kilikuu kwa kulingana na umbo lake na ni jina la wabongo tu.
 
Mnapenda kuwapa hela na ndo maana wanawakamata na kuwatoa hela mpaka mnatembea na change. Gari la ofisi na halina shida kwanini uwape hela? Hizi Kirikuu zingine za biashara wanajuana maana hata hao madereva huwa Wana faulo zao hivyo walishajengeana mazingira huku madereva wakidhani kukiwa kuna msala mkubwa itakuwa rahisi kufanya namna

Nina corolla ya 1995 ile ya alitumia Babu mpaka mjukuu na rangi imechunika tena namba A na huwa sipigwi mkono na nikipigwa mkono ni ukaguzi wa kawaida tu na naendelea na safari.

Yaani una driving licence, fire extinguisher, kadi ya gari na reflector. Taa zote yaani indicator zipo fresh, tyre sio kipara plus umefunga mkanda na abiria wako wa mbele nae amefunga mkanda ukitoa hela umependa kutoa sadaka kwa askari labda kama umefanya kosa nje ya hapo.

Shida watu wengi wamezoea kusema askari akiamua lazima atakukuta na kosa wakati si kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…