Gari kutetemeka

Gari kutetemeka

Hili tatizo liliwahi kunitesa sana kwenye MAZDA PREMACY nilibadilisha plugs sijui cables,lambwa sana hela na mafundi lakini tatizo likawa pale pale.
Kuna jamaa yangu akashauri tufungue sensa ya air cleaner kufungua tukakuta maji kibao,kumbe wakati wa kuosha injini yaliingia.Tuka kausha maji kurudishia mpya !! sijajua kama glanza ina hiyo sensa !!
Kutokana na michango ya wengi hapo juu na majibu ya mtoa mada, hili ndilo tatizo halisi linaloisibu hiyo gari. Kwa kawaida silencer ni kitu cha mwanzo mafundi wanachoangalia pindipo gari ikiwa inatetemeka ila hiikitu huwa wanaipuuzia. Mtoa mada fanya hivi fari itakuwa okay
 
Wadau naomba mnisaidie na mimi pia. gari yangu ikifikia speed 90 inatetemeka lakini ukivuka hiyo speed inatulia. je tatizo lawezakuwa nini?
Wee tatizo lako ni mipira ya tairi hizo. Badilisha tairi zote au nenda kwa fundi aangalie tairi zenye tenge, tatizo lako litaisha. By ze way ni gari gani
Mkuu?
 
Mkuu kilikuja kikiwa shwari tu nikapigia msele kama miezi saba after there ndo kikaanza huo mchezo, lkn kumbuka ukikweka neutral mtetemo unapotea ama ukishusha silensa pia mtetemo unapotea kiujumla epuka kudanganywa na mafundi kua spea fulani imeisha, maana mimi niliambiwa engine mounting nikachenj, ikawa vilevile, nikaambiwa plugs -ikawa no, nikaambiwa rims nikabadili so nilijikuta nafanya kila nililoambiwa na mafundi bila mafanikio. mwisho niliamua kukaaa nayo hivohivo na hata niliyemuuzia yuko Tbt anayo iko hivohivo inachapa mwendo hadi leo na hata akinipita road huwa ananipita kama nimesimama kiukweli kinakimbia na exhaust inamakelele so hua natamani nikirudishe but kishatoka. so we tulia nacho ukifika foleni put on neutral then engage D unasepa broo. Pamoja sana we kikikuchosha nisukumie bado natamani kiwe kwenye himaya yangu, i like it and i enjoy its move and size so keep it.

Big up kamanda. Nimependa comment na advice yako. Hakuna ya kuumiza kichwamkwa tatizo dogo kama ilo. After all hakuna mtu aliyemje atakayesikia hilo tatizo. Sana huwa ni la kisaikolojia tu kwamba, mbona inatetemeka. Livumilie, chapa nalo mwendo. Ukiona linakukera zaidi weka sokoni wasukumie watu wengi. Tatizo kwisha.
 
Big up kamanda. Nimependa comment na advice yako. Hakuna ya kuumiza kichwamkwa tatizo dogo kama ilo. After all hakuna mtu aliyemje atakayesikia hilo tatizo. Sana huwa ni la kisaikolojia tu kwamba, mbona inatetemeka. Livumilie, chapa nalo mwendo. Ukiona linakukera zaidi weka sokoni wasukumie watu wengi. Tatizo kwisha.
Ushauri huo kama ingekuwa mikoani kusiko na foleni, lakini kwa miji kama Dar si ushauri mzuri kwani gari inapokuwa inatetemeka sana possibility ya kuzima ni kubwa na hivyo kuweza kuwanufaisha mateja na polisi mara kwa mara.
 
Yaani ilikuwa ukipiga lesi unatoka moshi mwingi mweusi,pia wese lilikuwa likitafunwa kwa sana tu !!
 
pole, angalia plug na cable zake, mojawapo inawezekana imeisha, i have the same before.
 
Itakuwa inasumbuliwa na malaria sugu hiyo.
Tuache utani wakati wa kuelimishana. Mtu mmoja anaweza kuuliza swali kwa manufaa ya wengi na majibu yakapatikana kwani JF ina watu wa fani mbali mbali hivyo kama hujapendezwa na swali au hujui jibu achana naye lakini kuleta utani kwenye serious issues kunaonesha mapungufu makubwa sana kwako. Kumbuka kila mjinga na kazi yake. Kuuliza si ujinga na hakuna mtu mwenye elimu zote yaani anayefahamu kila kitu! Tujifunze kuwa wavumilivu kwa shida za wengine badala ya kuzigeuza utani. Utajisikiaje wewe kesho ukiuliza swali ambalo kwa dhati yako unahitaji msaada wa wana JF halafu mtu mmoja asiye na busara akalifanyia utani. Kumbuka humu JF kuna kona ya utani, kama ingekuwa swali lake ni la utani angelipeleka huko lakini yeye kalileta huku kwa madhumuni maalumu kuwa sio utani!
 
Kutokana na michango ya wengi hapo juu na majibu ya mtoa mada, hili ndilo tatizo halisi linaloisibu hiyo gari. Kwa kawaida silencer ni kitu cha mwanzo mafundi wanachoangalia pindipo gari ikiwa inatetemeka ila hiikitu huwa wanaipuuzia. Mtoa mada fanya hivi fari itakuwa okay

Poa kamanda ngoja nikalijaribu
 
Huenda ikawa engine inapandisha oil zinazosababisha plug kuloa au kufa kabisa, au sensor ikawa imekufa
 
Huko kwingine sawa mkuu,ila matope kwenye rims.....ha!

Mkuu sikuandika kitu ambacho sina experience nacho...,Gari yangu mkuu ilikuwa inayumba ukiendesha from 80 to 100 Km/hr yaani utadhani engine mounting zimeisha, nilicheck kila mahali hata mafundi tena kwa kutumia computer lkn hamna kitu, kama joke tu nikafungua tires za mbele zote na kulikuwa na matope maana some days before nilikwama sehemu, nikasafisha halafu nikatest, gari ikatulia kabisa, am using fiat bravo 2010...na nilinunua brand new kabisa....anyway ilikuwa ni ushauri tu na muulizaji aliuliza nini kinaweza kuwa tatizo....
 
Wadau wamesema mengi ya muhimu,nami naomba kuongezea japokuwa mimi siyo fundi magari,niliwahi kupata tatizo kama hilo japokuwa gari haikuwa inatetemeka sana lkn nilipoenda kwa fundi akabadilisha spark plugs na tatizo likaisha.
Kama gari yako inatumia petrol,wakati likiwa kwenye silence jaribu kuangalia kama zote zinachoma,kwa kuchomoa moja baada ya nyingine.


pamoja na hayo aangalie pia siencer inawezekana ipo chini
 
Kama ukiendesha pia hutetemeka,Jaribu kufungua tailisafisha amachunguza taili zako yawezekana nimevimba vimba na kusababisha gari kutetema pindi itembeapo,Je gari yako ya aina gani nikupe namba ya Fundi.
 
Kaka kama 'uko Dar nenda pale backkashire garage hapo kinondoni piga 07184871657 anamashine ya kupiga (engine analysis)
 
Ha ha ha, mie nilidhani yangu ina mapepo?! Kumbe kweli ni tatizo.
 
Back
Top Bottom