Gari nimenunua Afrika Kusini Milioni 4, kodi Tanzania Milioni 18!

Jamani mimi naulizia kwa hapa bongo ni wapi wanakouza pikipiki used zilizo katika hali nzuri kutoka Japan.Au ushuru wa TRA kwa pikipiki upoje?
 
Kuna ndugu yangu juzi kaingiza mzgo wa laptops kutoka SA zipo km 20 hivi pamoja na cameras. Jamaa wamempiga kila item moja 100,000/= amebaki analia tu.
 
Kama nimemuelewa vizuri ni kwamba jamaa ni kama alikua anaishi ZA for sometimes na hiyo gari aliinunua kwa matumizi yake huko huko ZA so kaamua kurudi nyumbani na ndio kakutana na hayo makitu! Kwa ufupi, Tanzania bado inatenda miujiza.
Kwenye kampuni moja niliokua nafanya nayo kazi, jamaa mmoja kutoka West Africa huko alikujaga kwenye hiyo Kampuni yetu, nadhani alikua anatokea Guine huko (is one of the French speaking country in Africa ) so mimi pamoja na wenzangu tukawa tunatafuta magari USED from Japan, kuna PRADO moja hivi tulilipenda (tulikua tunafurahisha macho tu) lilikua linagharimu ka $ 5000 hivi kwa maana ya CIF,tulipokwenda kwenye calculator ya TRA ilionesha KODI kama Tsh 18M plus na change hivi, yule jamaa akatuuliza, "In Tanzania, are you having vihecle industries!?" Tukamuuliza, Why Mr Camara (Camara jina lakutunga). Yeye alishangaa kwanini KODI kubwa namna hiyo ilihali hatuna kiwanda/viwanda vya magari. Kwake yeye, KODI kubwa sometimes inawekwa iliku discourage importations ya vitu vinavyo weza kutengenzwa locally.
 
Lakini Mkuu, hizo gari unafahamu bei yake hapo Bongo ? Na, je kama ukiiagiza kutoka Japan itasimama shilingi ngapi ? Kama ulinunua 4.5 mil. + 18.5 mil ni sawa na 22.9 mil ambayo ni bei ya kawaida kwa T/Hilux.
 
Heavy Tax katika ku import magari pia inasaidia kucontrol miundo mbinu ya nchi kama traffic jam. kwahiyo on other way wanafanya hivyo ili kucontrol movement ya magari.
 
Mimi nimewahi fanya kazi na hao watu wa west Africa kwao kodi ni kubwa kuliko huku kwetu,
 
Kodi za tanzania ni kukomoana tofauti na kenya.Ndiyo maana watu wengi wanakwepa kulipa kodi
 
Gari ya mwaka gani?gari used ndio zina ushuru mkubwa zaidi mkuu
Calculator haingalii umri tu kuna vitu vingi vinajumuisha so kinachoathiri bei ya ushuru ni bei ya gari, ikiwa na bei kubwa na ushuru unakua mkubwa pia!
 
 
nimegifunza kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…