Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #381
Sajo...mtu yeyeto anayeipenda Tanzania lazima atagadhabika na uchochezi unaoufanya
Mimi naipenda nchi yangu na naithamini historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Naipenda historia hii kwa sababu kubwa moja kuwa ni historia ya wazee wazee wangu walivyosimama kupambana na ukoloni hadi wakashinda na uhuru ukapatikana tarehe 9 Desemba 1961.
Nimeghadhibishwa kuja kuona kuna watu wameifuta historia hii na kuweka ya kwao.
Huu si uchochezi.
Kitabu kilipotoka kilishtusha wanahistoria wakubwa wataalamu katika African History na wakafanya pitio la kitabu changu.
John Iliffe, James Brennan na Jonathon Glassman walikipitia kitabu na wote wakachapwa na Cambridge Journal of Africa History.
Hakuna hata mmoja wao aliyesema hiki kitabu ni uchochezi.