Yaani ukitaka kuona uchanga wa mtu kwenye siasa za Tanzania basi msikilize anaongea nini kuhusu Samia na 2025!!
Guys, moja ya sababu ambazo ma-CCM huwa wanatupiga sana bao ni namna wanavyo-handle mambo yao!!!
Huku nje unaweza kuona huko CCM kuna mtimbwalanyiko kweli kweli lakini haya majamaa yakishakutana tu Chimwaga, yanakuwa kitu kimoja!!
Hizi simulizi za CCM kuparaganyika, CCM kufa kibudu zilienea sana wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa CCM mwaka 2012!!!
Tena wakati ule kulikuwa na vigogo kweli kweli waliokuwa wanaonekana ndo wanaenda kuichinja CCM... hawa ni pamoja na Lowassa, Chenge, na Rostam Azizi!!
Kuna wengine wakafikia hadi kusema JK anapigwa chini uenyekiti... sie wengine tukawa tunacheka tu!!!
Pamoja na rabsha zote hizo, wafuatiliaji wa siasa watakumbuka kilitokea nini!!
The Main Villain Himself, Edward Ngoyai Lowassa wakaja kumchinja na kumzika kabisa 2015!!!
Hayo ndo ma-CCM!!
Ma-CCM yataondoka tu madarakani pale Watanzania watakavyoacha kuwa mazombi lakini eti tutarajie migogoro ya watu kama akina Ndugai inaweza kuwaondoa hawa jamaa, itakuwa mnajidanganya!!!