Gazeti la Uhuru: Rais Samia hana wazo la kugombea Urais 2025

Akigombea atashinda kwa sababu state apparatus zitamshindisha. That is obvious.

Lakini hana merits za kisiasa.

Hana kismati cha kisiasa. Hana Karama.

Ni ngumu "kumshindisha" mtu ambaye hajiwezi yeye binafsi.
Unakielewa unachotaka kukieleza?Ni lini wanashinda kwa haki hao CCM?
 
Unajua maana ya Hawezi?

Hata wewe unaweza kugombea according to Katiba ya nchi, unless ni Mharifu, haujafikia umri au hauna akili timamu (jambo ambalo sidhani unless am mistaken)
 
Kosa kubwa la Mama ni kukubali watu wamdhihaki Dkt Magufuli kutokana na kifo, yaani anaenda mpaka kupiga picha na Mange kimambi ambaye alikuwa ana ratibu mauaji ya Dkt Magufuli na baada ya kifo alifurahia.

Yaani Mama kumsafisha inazidi kuwa ngumu sana. Yaani angejua alipaswa achukue ushauri kwa TISS badala ya kukurupuka kama alivyofanya. Yaani chuki huku mitaani ni kubwa mno.
 
Chuki ya nini na imesababishwa na nani?Na kwa nini tuanzishiane chuki?
 
Hajitambui.
 
Samia hana merits.

Ukitaka kubebwa lazima ubebeke.

Huwezi kubeba gunia la misumari.

Magufuli alikuwa ana "soko" kisiasa.

Ni mtu aliyekuwa anaweza kuuzika. Ni rahisi kumshindisha. Ana merits.
Umeulizwa mara nyingi hapo juu.Kwa nini huyo unayemueleza kwamba aliweza "kuuzika" alibaka chaguzi zote(serikali za mitaa na uchaguzi mkuu)?Huko kuuzika kunaonwaje na watu wengine?
 
Chuki ya nini na imesababishwa na nani?Na kwa nini tuanzishiane chuki?
Tozo, chanjo, kurudisha serikalini wasaliti wanaojulikana kama waunda genge la mafisadi, kuanza kuhujumu miundombinu ya umeme na maji ili pawe na mgao halafu na kuja kusingizia ukame na wakati huo huo yeye akakubali kudanganywa eti kuna ukame na yeye akautangazia umma eti kuna mgao wa maji na umeme na maji na watendaji wake wakakanusha kwa kusema no mgao maji yapo, kukubali kudanganywa kwa kumtukana waziri wake ni nonsense kwa kitu ambacho ni cha kisheria na si matakwa ya waziri. Yaani Mama tumuombee Mungu airejeshe nchi kwenye misingi ya Dkt Magufuli. Yaani watu wale bata ila pawe na uadilifu na kujali maslahi ya wananchi
 
Mstari wa pili kutoka mwisho ndiyo umeharibu utetezi wote!Hata hivyo,hayo ma-hovyohovyo yanafanywa na serikali ya CCM na si wengine.Mnahitaji kujitafakari au mbebe makorokoro yenu muondoke?
 
Tunaenda na Samia no way out sukuma gang mtarudi madarakani.

Kama hayo ulivyosema ndio tatizo kuna miaka 4 mbele mkuu na ana washauri na Serikali na chama.

Mwisho huko Upinzani unadhani takataka gani watu wanaweza ichagua?
 
Umenena kweli tupu,

Utaratibu wa aina ya kiongozi kama huyu ufutwe mara moja.....................

Wanaomshabikia na kumsifu kila kukicha ni kwa sababu ya matumbo yao; wakati walio kimya wana hasira zisizoelezeka
Katiba irekebishwe pawepo na vipengele vinavyotizama haya mambo kwa upana wake.

Unaweza ukaweka makamu wa Rais kama Kanyaboya halafu paap akawa Rais. Hili ni tatizo.

Katiba ya nchi lazima iwe na macho mapana sana. Vinginevyo ni rahisi sana mafisadi na watu waovu kujiingiza serikalini kwa mbinu za ajabu ajabu.
 
Amalizie awamuyake hii ya 5 apumzike hataivyo amefanya kazi vyakutosha akimaliza itakuwa miaka 10 yupo mjengoni, so its more than enough!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…